- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Malaysia:
Hati ya Pingamizi kuhusu “KL Headline Msimu wa 2026”
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir Malaysia (HTM) uliwasilisha hati ya pingamizi kwa Wizara ya Mawasiliano huko Putrajaya kuhusu kuandaliwa kwa tamasha la “KL Headline Msimu wa 2026”. Hatua hii ilichukuliwa ili kuihimiza serikali kufuta tamasha hilo mara moja, kutokana na madhara makubwa ambayo lingesababisha kwa jamii na ukiukaji wake wa wazi wa sheria ya Kiislamu. Hati hiyo ilipokelewa na Bi. Wan Saidatul Shafina binti Mohamed Amin, Katibu wa Idara ya Mawasiliano ya Kimkakati na Masuala ya Taasisi, kwa niaba ya Wizara. Pia alitenga muda wa kusikiliza maelezo kamili na ya kina ya sababu za pingamizi zilizowasilishwa na Hizb ut Tahrir Malaysia.
Ujumbe huo, ukiongozwa na Ustadh Abdul Hakim Othman, msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir Malaysia, ulielezea sababu kuu tano katika hati yake ambazo zinahitaji Wizara kufuta mara moja matamasha haya ya kupindukia mipaka:
1) Yanajumuisha thaqafa ya anasa na kujiingiza katika matamanio (raha) na mtindo wa maisha wa Kimagharibi.
2) Yanaleta ghadhabu na adhabu ya Mwenyezi Mungu (swt).
3) Yanasababisha uzalishaji wa mapato haramu kwa serikali.
4) Yanawakilisha usaliti wa amana ambayo Mwenyezi Mungu ameweka kwa serikali.
5) Yanaakisi ukosefu wa hisia na huruma kwa kinachoendelea Gaza.
Katika jibu lake, Shafina alithibitisha kwamba angewasilisha hati hiyo ya pingamizi moja kwa moja kwa Waziri. Pia alieleza kwamba Wizara ingechunguza pingamizi hiyo na kutoa jibu linalofaa. Kufuatia kuwasilishwa kwa hati hiyo, ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir/Malaysia, ukiongozwa na msemaji rasmi, Ustadh Abdul Hakim Othman, na akiandamana na wanachama wengine watatu, ulifanya mkutano na waandishi wa habari kufafanua maelezo ya hatua hii.
Ustadh Abdul Hakim alieleza kwamba chama kinakusudia kuanzisha msururu wa shughuli na matukio mengine ili kuendelea kuishinikiza mamlaka husika kufuta matamasha haya ya kupindukia mipaka. Alisisitiza kwamba suala hilo si jambo la pembeni au dogo, bali linawakilisha kitendo dhahiri cha maovu na maasi, kukiuka hukmu za Sharia ya Kiislamu, ambalo haliwezi kufungiwa macho au kupuuzwa.
Jumanne, 2 Muharram 1448 H sawia na 16 Juni 2026 M

- Video ya Amali -

Kusoma Taarifa kwa Vyombo vya Habari iliyotolewa na
Ustadh Abdulhakim Othman
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir Malaysia

Kwa Maelezo Zaidi, Tafadhali Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Malaysia:
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Malaysia
Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Malaysia
Ukurasa wa Instagram wa Hizb ut Tahrir / Malaysia
Akaunti ya Telegram ya Hizb ut Tahrir / Malaysia
