- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Jibu la Swali
Vita dhidi ya Iran
(Imetafsiriwa)
Swali:
Je, ni nini maana ya kauli za Trump zenye kusitasita—kutoa Iran masaa 48, kisha siku 5, kisha siku 10—na pendekezo lake la mpango wenye nukta 15? Namna gani ujanja wa kauli, nyingi kutoka kwa Trump na chache kutoka kwa Iran, na tangazo la televisheni ya Iran kukataa pendekezo la Trump? Matokeo ya hayo yote ni nini? Je, Trump atafikia malengo yake ya kuizuia Iran kuwa na silaha za nyuklia na makombora mazito, na kufanya Iran irudi katika duara la Marekani au iwe taifa tegemezi, au itabaki huru? Je, umbile la Kiyahudi inataka kwa idhini ya Marekani kupanua eneo lake kwa kumiliki kusini hadi Mto Litani kama Waziri wa Ulinzi wa serikali hiyo alivyotangaza? Kwa nini Waislamu hawatambui kwamba Dola ya Kiislamu—Khilafah Rashida—ndio itakayomvuta Trump na wafuasi wake kama ilivyowavuta Wakaizari wa Roma na Wakhusro wa Uajemi, na kuwapiga kwa nguvu, na kukataa njama zao juu ya shingo zao, hivyo izza ya Uislamu na Waislamu, na udhalilifu wa ukafiri na makafiri?
Jibu:
Ili kufafanua jibu la sehemu tatu za swali hilo, tunachambua mambo yafuatayo:
Kwanza: Sehemu ya kwanza ya swali kuhusu lengo la Trump la kuifanya Iran kuwa taifa tegemezi, kuiweka katika duara lake, au kuiacha huru:
1- Asubuhi ya Jumamosi, 28 Februari 2026, Rais Trump wa Marekani alichapisha video kwenye jukwaa lake la kijamii la Truth akitangaza kwamba vikosi vyake vilivyoko Mashariki ya Kati vilianza shambulizi kubwa la kivita nchini Iran. Netanyahu, mshirika wake, alijiunga naye. Hii ilionyesha ukaidi ndani ya Iran, haswa ndani ya Walinzi wa Mapinduzi, kuhusu uhusiano na Marekani. Utawala wa Trump ulikuwa umeanza kudai makubaliano makubwa kutoka kwa Iran ili kuifanya kuwa taifa tegemezi kabisa—kumaanisha kuiondoa kwenye mzingo wake wa kujitegemea, kwa sababu kuchanganya mauaji ya viongozi na kukaa katika mzingo ni jambo lisilowezekana. Marekani haikuanzisha vita dhidi ya Iran ili kuiondoa kwenye mzingo wake na kuiacha huru. Badala yake, ilikuwa na hakika ya kuifunga kwa haraka na kuifanya taifa tegemezi kwa mshtuko wa kwanza. Hii ina maana moja: utawala wa Trump ulikuwa unaratibu na watu ndani ya serikali ya Iran kuchukua madaraka mara baada ya mshtuko wa kwanza—baada ya kuua viongozi wakuu wanaokataa. Lakini hii haikutokea; Walinzi wa Mapinduzi waliweza kudhibiti hali.
Kwa hiyo, Trump na umbile la Kiyahudi walishangazwa kwamba utawala wa Iran ulikuwa imara, ukirusha makombora na droni kwa ukali usio wa kawaida na ujasiri wa kushangaza. Mashambulizi ya Iran yalilenga umbile la Kiyahudi na kambi za Marekani katika Ghuba na eneo lote. Trump alisema kwamba baadhi ya watu aliotarajia wataweza kuchukua madaraka waliuawa bila kukusudia! Marekani ilidhani majibu makali ya Iran yalitokana na athari za kihisia za baadhi ya viongozi baada ya kuuawa kwa Kiongozi Mkuu, na ilisubiri kuteuliwa kwa kiongozi mpya. Lakini baada ya kuteuliwa kwa Mojtaba Khamenei kama mrithi wa baba yake na baada ya wiki kupita, utawala wa Iran ulitulia chini ya udhibiti wa wale wanaomchukia Marekani, haswa kwani uchokozi wa Marekani ulikuwa umevuka mipaka yote.
2- Inaonekana kwamba hesabu za Marekani na umbile la Kiyahudi zilikuwa potofu. Walipoanza uchokozi wao dhidi ya Iran, walikuwa wameweka muda mfupi wa vita—uliokadiriwa kuwa siku nne—kwa shambulio la haraka na kubwa lililolenga viongozi wakuu, vituo vya nyuklia, na vituo vya uzalishaji na kurushia makombora. Walidhani kwamba mara baada ya kuua viongozi wakuu na ngazi ya kwanza ya uongozi, ngazi ya pili itajisalimisha na kukubali masharti yao, kama ilivyotokea Venezuela wakati vikosi vya Marekani vilipomteka nyara rais wake, na naibu wake na waliokuwa pamoja naye wakajisalimisha kwa Marekani. Lakini hilo halikutokea Iran. Baada ya kuuawa Kiongozi Mkuu Ali Khamenei na baadhi ya viongozi wa utawala, Walinzi wa Mapinduzi waliimarisha msimamo wao na kuamua kukabiliana na uchokozi na kushambulia maadui. Kwa hiyo, mapengo yalitokea kati ya Marekani na Iran, ambayo hapo awali ilikuwa katika mzingo wake. Marekani ilitaka kubadilisha uhusiano huu; vyenginevyo, isingezindua uchokozi huu na kisha kuliruhusu umbile la Kiyahudi kuua viongozi muhimu zaidi wa utawala, wakiwemo Kiongozi Mkuu. Hii inaonyesha kwamba Marekani inalenga kubadilisha sera ya utawala kutoka taifa la mzingo hadi taifa tegemezi, kuiwezesha kuamuru masharti yake katika mazungumzo na Iran. Hata hivyo, ilishindwa na kuamua kuendelea na vita.
3- Kinachothibitisha kwamba lengo la Marekani lilikuwa kubadilisha sera ya utawala wa Iran na kwamba haikutarajia utawala kustahamili uchokozi na kujibu licha ya kuuawa kwa viongozi wake wakuu ni taarifa ya Waziri wa Ulinzi wa Marekani Hegseth mnamo Machi 10, 2026: “Siwezi kusema kwamba tulitarajia hilo kuwa hasa jibu lao.” Pia, kile ambacho ‘New York Times’ ilinukuu kutoka kwa vyanzo vyenye ufahamu mnamo Machi 12, 2026: “Trump na washauri wake walibaki na hakika kwamba kuua viongozi wakuu kungesababisha viongozi wenye vitendo zaidi ambao wanaweza kutafuta kumaliza vita”—yaani, kujisalimisha kwa Marekani na kukubali masharti yake! Walipokosa matumaini yao ya kujisalimisha haraka, Trump alianza kuzungumza kuhusu wiki mbili kumaliza vita, labda wiki nne. Anataka kumaliza vita kwa njia yoyote itakayomfanya aonekane mshindi, si kumaliza vita akiwa ameshindwa au aibu, kama ilivyotokea wakati vikosi vya Marekani vilipotoka Afghanistan mwaka 2021. Anataka kumaliza vita kabla ya mambo kuwa mabaya na kumuathiri yeye na chama chake ndani ya nchi, haswa kwa kuchaguliwa kwa nusu ya muda kwa Congress vuli ijayo; kupoteza huko kutaathiri uchaguzi mkuu wa urais wa 2028. Trump anajaribu kudai ushindi wa maneno, akiiambia tovuti ya Marekani Axios mnamo Machi 11, 2026: “Hakuna kitu chochote kilichobaki Iran kinachoweza kulengwa. Mashambulizi dhidi ya Iran yamesababisha uharibifu mkubwa tangu awamu ya kwanza kuliko walivyofikiria inawezekana.” Trump anatoa kauli akichezea maneno kana kwamba ameshinda. Hii inaonyesha kwamba msimamo wa Marekani ni wa wasiwasi, kwa kuwa imeshindwa kufikia malengo yake haraka na bila hasara.
4- Baada ya hayo, Trump aliamua kutumia ujanja wa kuongeza muda kama mkakati mpya. Mnamo Machi 22, alitangaza muda wa masaa 48 wa mwisho. Kisha mnamo Machi 23, aliongeza muda kwa siku tano kwa kisingizio cha kufanya “majadiliano yenye kujenga.” Kisha mnamo Machi 26, alitangaza kuongeza muda kwa siku kumi, yaani hadi Aprili 6, 2026, pamoja na kauli zake nyingine zinazogongana. Kupitia mkakati huu, analenga kutumia shinikizo la kisaikolojia na kisiasa kwa Iran ili kulazimisha kujisalimisha. Nyongeza hizi za muda zinaweza pia kuwa kifuniko cha kupeleka vikosi vya Marekani katika eneo kwa ajili ya operesheni ndogo ya ardhini dhidi ya Iran au Kisiwa cha Kharg. Amefanya hivyo hapo awali katika mashambulizi yake yaliyopita. Anajaribu kutumia ujanja kupeleka vikosi vipya (iliripotiwa kwamba Ikulu ya Marekani na Wizara ya Ulinzi wanazingatia kupeleka angalau wanajeshi 10,000 wa mapigano wa ziada Mashariki ya Kati katika siku zijazo...” (Mepa News, Machi 27, 2026). Hivyo, nyongeza hizi za muda ni mbinu za udanganyifu, kama hapo awali.
5- Kutokana na ukaidi wa Trump, hakuna kilichobaki isipokuwa anachokiita “amani kwa nguvu”—mazungumzo chini ya moto. Alitangaza mpango wenye nukta 15 aliowasilisha kwa Iran kupitia Pakistan ili kumaliza vita. Mpango huo unajumuisha: kuvunjwa kabisa kwa uwezo uliorundikana wa nyuklia; ahadi ya kutotafuta kamwe silaha za nyuklia; kusitisha utajiri wa uranium katika ardhi ya Iran; kuwasilisha nyenzo zote zilizotajirishwa kwa IAEA ndani ya muda mfupi; kuzima na kuharibu vituo vya Natanz, Isfahan, na Fordow; kutoa ufikiaji kamili wa habari ndani ya Iran kwa IAEA; Iran kuachana na “sera ya vikosi vya wakala”; kusitisha msaada wa kifedha na kijeshi kwa washirika wake katika eneo; kuweka Mlango-Bahari wa Hormuz wazi na huru kwa usafiri wa baharini kwa wote; kushughulikia suala la makombora baadaye, kwa kuweka vikwazo kwa idadi na umbali, na kudhibiti matumizi yao kwa ulinzi halali” pekee (Al-Araby Al-Jadeed, Machi 25, 2026). Masharti ya mpango huu yanaonyesha wazi kwamba lengo la Trump ni kuiondoa Iran kutoka kuwa dola ya mzingo na kuigeuza kuwa dola kibaraka inayotekeleza kila kile Marekani inachoagiza. Hata katika vyombo vya habari vya kimataifa, hati hii imesifiwa kama hati ya kujisalimisha—hati ambayo kwa uthabiti inaigeuza Iran kuwa dola tegemezi.
“Lakini mpango uliowasilishwa na utawala wa Trump kupitia hatua za Pakistan, kiuhalisia, ni chombo cha kusalim amri.” (Taasisi ya Doha, 26/3/2026). Mnamo 24 Machi 2026, alikuwa na maongezi ya simu na mkuu wa jeshi wake anayempenda, Jenerali Asim Munir, mkuu wa jeshi la Pakistan, akimhimiza kuilazimisha Iran kukubali makubaliano hayo kwa masharti ya Trump. Hakufaulu. Iran ilikataa mpango huo kupitia televisheni ya serikali hiyo, kukataa ambako kuliashiria kukataa kwake kuwa “dola tegemezi”. Katika kujibu, Iran iliwasilisha mpango wake yenyewe wenye nukta tano: kusitisha mauaji yanayolenga maafisa wa Iran, kupewa dhamana dhidi ya vita vipya dhidi ya nchi hiyo, malipo ya fidia kwa vita hivyo, kukomeshwa kwa uadui, na kutambuliwa kwa ubwana wa Iran juu ya Mlango-Bahari wa Hormuz… (Euronews, 25/3/2026). Huku ofa hii ya Iran ikiwa haizungumzii programu za nuklia na makombora, haikuwiana na mpango wa nukta 15 wa Amerika. Hivyo, mazungumzo yakabakia yamekwama.
6- Hata hivyo, mawasiliano hayajakatika, ingawa kwa njia zisizo za moja kwa moja. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi alisema katika maongezi na Al Jazeera mnamo Machi 31, 2026: “Kinachotokea sasa si mazungumzo ya moja kwa moja, wala kupitia wapatanishi. Anapokea ujumbe moja kwa moja kutoka kwa mjumbe wa Marekani Witkoff, kama hapo awali. Hii haimaanishi kwamba tunazungumza. Hakuna ukweli katika kuzungumza na upande fulani ndani ya Iran. Ujumbe huja kupitia Wizara ya Mambo ya Nje, na kuna mawasiliano kati ya mashirika ya usalama, chini ya usimamizi wa Baraza la Usalama wa Taifa.” Alisema: “Hatujachukua uamuzi wowote kuhusu mazungumzo. Tuna walakini kuyahusu, na masharti yetu ya kumaliza vita ni wazi. Hatutakubali kusitisha mapigano; tunatafuta kumaliza vita kabisa, siyo Iran tu, bali katika eneo lote.” Alisema: “Masharti ya Iran ni dhamana dhidi ya kurudiwa kwa uchokozi na fidia kwa hasara.” Kauli hii ina sura mbili: kuna mawasiliano lakini hakuna mazungumzo! Kwa vyovyote, inaonyesha kwamba ndani ya serikali ya Iran, wapo walio tayari kuzungumza, na kwamba Marekani inaweza kusitisha vita na kuanza mazungumzo wakati wowote, kwani mawasiliano yanaendelea kati yake na utawala, kulingana na Araghchi. Hata hivyo, Walinzi wa Mapinduzi ni wakali zaidi kuliko watawala; wanaendelea kushambulia maslahi ya Marekani katika Ghuba na maeneo jirani na katika maeneo yaliyokaliwa kimabavu, na wanakataa kuzungumza.
7- Kwa kuzingatia kwa makini na kutafakari mambo yaliyotajwa hapo juu, hitimisho la jibu la sehemu ya kwanza ya swali ni kama ifuatavyo:
a- Walinzi wa Mapinduzi wanapinga kwa bidii ili kuikomboa Iran kutoka kwa ushawishi wa Marekani, wasirudi kwenye mzingo wake, bali wawe dola huru: (Walinzi wa Mapinduzi wa Iran: Harakati yoyote ya maadui katika Mlango-Bahari wa Hormuz itakabiliwa na jibu la kali kutoka kwa vikosi vya majini... MTV Lebanon, Machi 4, 2026); (Msemaji wa Walinzi wa Mapinduzi wa Iran Ibrahim Zolfaghari alithibitisha Alhamisi kwamba vita vitaendelea mpaka maadui wadhalilike na kujisalimisha, akisisitiza kwamba mashambulizi yataendelea kwa kasi kubwa na pana zaidi... Al-Ayyam News, Aprili 2, 2026); (Walinzi wa Mapinduzi wa Iran walithibitisha mnamo Jumatano kwamba Mlango-Bahari wa Hormuz wa kimkakati utabaki imefungwa kwa maadui wa nchi, wakati Trump alisema hatazingatia kusitisha mapigano isipokuwa ufunguliwe tena... Akhbar Al-Youm, Aprili 1, 2026); “Walinzi wa Mapinduzi walisema kupitia chaneli ya Telegram inayohusishwa nao: ‘Kuanzia sasa, kila operesheni ya mauaji itakabiliwa na kuangamizwa kwa kampuni ya Marekani’... (Al-Arabiya Net, Aprili 1, 2026).
b- Maafisa wa utawala wa kiraia nchini Iran wanayumba kati ya nguvu na udhaifu; wanaotaka (kwa matumaini) Iran ibaki ndani ya mzingo wa ushawishi wa Marekani ikiwa wataweza. Kwao, Iran kuwa dola tegemezi ya Marekani, kama nchi nyingi katika eneo, si jambo kubwa. Inaonekana Trump ana watu (wafaao) wa kuzungumza nao Iran: (Rais wa Marekani Donald Trump alisema mnamo Jumanne jioni kwamba ‘anashughulika na watu sahihi nchini Iran.’ Alipoulizwa ni nani anayezungumza na Marekani, Trump alijibu: ‘Kwa sababu sitaki wauawe’... France 24 English, Machi 23, 2026); “Chanzo kimoja cha Pakistan kilifichua kwa Reuters kwamba Israel ilimwondoa kwa muda Waziri wa Mambo ya Nje Abbas Araghchi na Spika wa Bunge Mohammad Baqer Qalibaf kwenye orodha yake ya mauaji baada ya Pakistan kuiomba Washington isiwalenge, ikiijulisha kwamba ‘ikiwa nao watauawa, hakutakuwa na mtu yeyote wa kuzungumza naye’... Al Jazeera Net, Machi 26, 2026).
c- Kwa upande wa Trump, lengo lake katika vita hivi ni kuifanya Iran iwe tegemezi kwake, ikitii amri zake, kudhibiti mafuta yake na gesi yake, na kushiriki ushawishi katika Mlango-Bahari wa Hormuz na sehemu kubwa kwake! Marekani inataka kuendesha vita kwa njia itakayofikia upeo wa malengo yake. Inaweza kuamua kuongeza kasi kwa kushambulia vituo vya nishati vya Iran, hata kama Iran itashambulia vituo vya nishati vya Ghuba na bei ya mafuta kupanda kwa kiwango cha juu. Marekani inaweza kuweka kizuizi kwenye Mlango-Bahari wa Hormuz bila kuufungua—yaani, kuzuia meli za mafuta za Iran au zile zinazoruhusiwa na Iran kuvuka Bahari ya Arabia.
* Ndoto za Trump za kuivuta Iran ndani ya utegemezi hazitakwisha mradi tu ana watu ndani ya serikali walio tayari kushirikiana. Ikiwa watu hao watachukua madaraka, ndoto za Trump zitatimia.
* Lakini ikiwa matumaini ya Trump kwa watu hao yatakatika kutokana na maendeleo ya vita, na Walinzi wa Mapinduzi wakabaki imara kijeshi kama walivyo na kuirejeshea nchi mshikamano, basi Iran itaelekea kwenye uhuru. Vita hivi vinaweza kuwa vimekata uzi wa mwisho ulioiweka Iran katika mzingo wa Marekani.
Pili: Sehemu ya pili ya swali kuhusu Lebanon na iwapo umbile la Kiyahudi linataka kumiliki kusini hadi Mto Litani kwa idhini ya Marekani:
1- Kuhusu Lebanon, Al Jazeera iliripoti mnamo Machi 26, 2026, ikinukuu vyanzo kwamba “Iran iliwaarifu wapatanishi kwamba Lebanon lazima iwe sehemu ya kusitisha mapigano yoyote.” Mnamo Machi 24, 2026, Yisrael Katz alitangaza kwamba vikosi vyake vitadhibiti eneo kusini mwa Lebanon hadi Mto Litani, akisema:
“Wakaazi waliohamishwa hawatarudi kusini mwa Litani kabla ya kuhakikisha usalama wa wakaazi wa kaskazini mwa Israel.” Pia alisema: “Vikosi vyake vimelipua madaraja yote matano juu ya Mto Litani yaliyotumiwa na Hezbollah... na vitadhibiti madaraja yaliyobaki na kuanzisha eneo la usalama linaloenea hadi Mto Litani” (Asharq Al-Awsat, Machi 24, 2026). Waziri Mkuu wa Lebanon alitangaza mnamo Machi 19, 2026 kwa CNN kwamba alituma ujumbe kwa Trump: “Ningependa kumuhakikishia Rais Trump utayari wetu wa kuingia katika mazungumzo ya haraka na upande wa Israel.”
2- Kwa hiyo, kauli za umbile la Kiyahudi zinaonyesha nia yake ya kuanzisha eneo la kusitisha mapigano hadi Mto Litani kusini mwa Lebanon na kuzungumza juu ya kuwafurusha wakaazi wa Kilebanon wa eneo hilo. Hili si rahisi kwa jeshi lake kulifikia kutokana na upinzani kusini. Zaidi ya hayo, umbile la Kiyahudi halina uwezo wa kupigana isipokuwa kwa kutegemea wengine, kwa kuwa limejitenga na kamba ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo, uchokozi wa Marekani unapokwisha, wao watakwisha kiotomatiki.
Tatu: Sehemu ya tatu ya swali kuhusu Dola ya Khilafah—ndiyo itakayorejesha izza kwa Uislamu na Waislamu na kudhalilisha ukafiri na makafiri:
1- Hakuna kheri katika watawala wa nchi za Waislamu; haitarajiwi kwamba watarudi katika njia iliyo sahihi. Tunaweza kutumaini tu Ummah wa Kiislamu utakaposimamisha dola yake, wakiwa wameungana katika dola moja iliyojumuishwa ndani ya Khilafah Rashida chini ya uongozi wa kisiasa wenye ufahamu wenye azma ya imara isiyoyumba. Mafanikio yao yameandikwa kwenye kurasa za historia: walizishinda himaya mbili kubwa—Fursi na Rumi—ndani ya miaka michache. Waliendelea na ushindi wao mashariki na magharibi mwa dunia mpaka mataifa yakajisalimisha kwao, majeshi makubwa yakashindwa mbele yao, na mataji ya wafalme, wakaizari, na wakhusro yakaanguka chini ya nyayo zao. Huo ndio mwisho wa Marekani, ambayo itavunjwa, kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, kulazimishwa kufunga kambi zake na kuwarudisha wanajeshi wake nyuma kuvuka Atlantiki, wakiburuza mikia ya kushindwa na aibu, ambapo pua za Trump na wafuasi wake zitainamishwa kwenye mchanga.
[قُل لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ سَتُغْلَبُونَ وَتُحْشَرُونَ إِلَى جَهَنَّمَ وَبِئْسَ الْمِهَادُ]
“Waambie walio kufuru: Karibuni mtashindwa na mtakusanywa, mtiwe kwenye Jahannam; nako huko ni makao mabaya kabisa.” [Aal-i-Imran: 12]
2- Ni kweli kwamba Iran inashambulia kambi za kijeshi za Marekani katika Ghuba, na ni kweli kwamba inashambulia umbile la Kiyahudi. Ni kweli pia kwamba mashambulizi haya yana miliki kiwango kiwango cha nguvu. Lakini watawala wa Iran hawawezi kumshinda Marekani na kumrudisha nyuma isipokuwa Khilafah itakaposimamishwa—ambayo itamnusuru Mwenyezi Mungu na kutekeleza hukmu Zake, ili kupata ushindi kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, ikiiangaza dunia kwa uadilifu wake na jihad, na kukirimiwa na Mwenyezi Mungu kwa ushindi (nasr) Wake:
[إِنْ تَنْصُرُوا اللهَ يَنْصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]
“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Muhammad: 7]
Hapo ndipo itaifundisha Marekani somo baada ya somo hadi kifuniko chake kitakapovuliwa. Marekani inapigana na Waislamu leo kutoka katika ardhi zao na viwanja vyao wenyewe vya ndege, na inawatumia vibaraka wake kuzuia mashambulizi dhidi ya umbile la Kiyahudi. Dola ya Khilafah itavamia ngome za vibaraka hawa, kuwafukuza kabisa, na katika njia yake, itawahamasa Waislamu, na kuongeza nguvu zake hadi iwe mafuriko yenye kuangamiza yanayofikia kambi za Marekani nje ya nchi za Waislamu. Kisha mafuriko makali yataibuka, yakiangusha viti vya enzi vya watawala njiani, kuitakasa Palestina, na kukanyaga serikali ya Kiyahudi. Hili ni rahisi na linawezekana kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, ingawa wengi wanaona ni ndoto. Ummah una imani inayosukuma kama mto, na una chuki dhidi ya Marekani na Mayahudi kwa ukali na ukubwa wa udhalimu wao. Mtazamo wa ushindi huu sio wa mbali, kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu Atakaporuhusu ushindi Wake mkubwa. Kile Ummah wa Kiislamu utakachofanya baada ya hapo, na uwanja wa vita utakavyotamka, kinaweza kuzidi kile kalamu inavyoweza kuelezea sasa. Mwenyezi Mungu ameweka Njia Yake katika dunia hii kwa kauli Yake:
[وَكَانَ حَقّاً عَلَيْنَا نَصْرُ الْمُؤْمِنِينَ]
“Na ilikuwa ni haki juu yetu kuwanusuru Waumini.” [Ar-Rum: 47].
17 Shawwal 1447 H
4/4/2026 M