Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Sera ya Elimu Baina ya Kufeli kwa Dola ya Kisasa na Ruwaza ya Khilafah Rashida
(Imetafsiriwa)

Sera ya elimu nchini Tunisia, kama moja ya nguzo za dola ya kisasa, imefeli, na mageuzi yanayorudiwa rudiwa hayajafanikiwa. Watoto wetu wamekuwa chini kabisa katika orodha ya kimataifa, na shule na vyuo vikuu vyetu viko nje ya uainishwaji, huku makumi ya maelfu ya wanafunzi wakiacha shule kila mwaka na kutupwa mitaani, ili kumezwa na ukosefu wa ajira, dawa za kulevya, mashua za vifo, na vikundi vya uhalifu, hadi kila mtu atakaposhuhudia ufisadi wa mtaala wa elimu na kufeli kwa matokeo yake, bila kusahau kutengwa kwa walimu na kuwaacha chini kabisa katika ngazi ya mshahara.

Na leo, licha ya mfululizo wa mipango, kuanzia mashauriano ya kitaifa kuhusu mageuzi ya elimu (Septemba–Disemba 2023) hadi kuanzishwa kwa Baraza la Elimu la Juu lililoainishwa katika Katiba ya 2022, kile kilichopendekezwa katika mashauriano hayo si chengine ila ni marekebisho rasmi na uimarishaji wa mradi wa kimagharibi, wa kikoloni, wa kisekula ulioanzishwa mwaka wa 1958 na Mfaransa Jean Dupiace na kutabikishwa na Waziri wa Elimu wa wakati huo Mahmoud Al-Messadi, ili kuwatenga Uislamu kutoka kwa elimu na kuathiri kitambulisho cha kihadhara cha jamii na vizazi vinavyochipuka.

Kuregesha mfumo huu uliofilisika hakutatoa chochote ila muozo zaidi, kuvunjika, na utegemezi kwa Magharibi, na Ummah hautainuka isipokuwa kwa ruwaza halisi ya kielimu inayotokana na itikadi yake. Kwani sera sahihi ya elimu ni ile inayoegemea itikadi ya Kiislamu, hivyo sera za elimu na malengo yake huwekwa kwa mujibu wa njia inayohifadhi kitambulisho cha Ummah na itikadi yake ya Kiislamu, ili kuinua shakhsiya za Kiislamu zenye fikra na mwelekeo (nafsiya) wa Kiislamu, na kuwaandaa wana wa Waislamu ili miongoni mwao wawe wasomi maalum katika nyanja zote za maisha, kama vile sayansi za Kiislamu (kutoka ijtihad, fiqh, mahakama, na nyenginezo), na sayansi za majaribio (kutoka hisabati, informatics, kemia, fizikia, tiba, na nyenginezo).

Sera ya kielimu inayotabikishwa na dola imara, inayoogopwa na kumiliki uamuzi wake, inayowaunganisha Waislamu chini ya bendera ya Uislamu (Hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu, Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu), yaani Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume, ambayo hutawala kwa Uislamu na kutatua matatizo na migogoro yote ya Waislamu na ulimwengu mzima kwa sababu inatawala kwa mfumo kutoka kwa Muumba wa wanadamu ambaye pekee ndiye anayejua manufaa yao kila wakati na mahali, ikizalisha mwamko mkubwa wa kisayansi na mapinduzi makubwa ya viwanda na maendeleo yasiyo na kifani, na kuregesha haki kwa watu wake.

Kwani mfumo wa Khilafah una ruwaza ya kisiasa iliyo wazi na huru; hufanya elimu kuwa kiwanda cha kuunda watawala wa dola wenye haiba ya juu kabisa na udongo wenye rutuba unaozalisha watu wenye shakhsiya imara wanaotamani uongozi na kutokubali utegemezi wa kudhalilisha. Unaona elimu kama hitaji muhimu na unaitoa bila malipo kwa ubora wa hali ya juu kabisa, pamoja na marekebisho ya vipaumbele kulingana na hukmu za Shariah ili kuharakisha maendeleo ya kisayansi, kutenga mapato makubwa kutoka kwa mali ya umma na kile kilicho chini ya mkono wake (kama vile madini, nishati, kilimo, na mifugo) na vyenginevyo, kwa ajili ya kujenga mifumo tanzu inayounga mkono uwezo wake wa kufikia viwango vya juu vya maarifa, miongoni mwa muhimu zaidi ni:

1. Kujenga mfumo mpana wa elimu unaokuza shakhsiya ya Kiislamu kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu, ili kuunda kizazi kinachochanganya ubora wa uongozi na ikhlasi ya muumini, na kufurahia seti tofauti ya ujuzi na nyanja za utaalamu ambazo Ummah unahitaji katika mapambano ya maisha.

2. Kujenga mfumo wa utafiti na maendeleo ili kufanya utafiti, uvumbuzi, na maendeleo katika uoanishaji kati ya vyuo vikuu na vituo vya utafiti vya serikali, ili vyote viwe chini ya idara ya serikali katika usimamizi, uhamasishaji, na ufadhili.

3. Kujenga mfumo wa kimkakati wa viwanda unaosimamiwa na serikali kwa kujitegemea, kukuza uwezo wa kijeshi kwa njia za kisasa na kutoa mahitaji ya msingi ya watu binafsi, na kuunda silsila jumuishi za viwanda vizito huku usimamizi wa serikali ukivisimamia na kupata vifaa vyote vinavyohitajika kwa ajili ya viwanda hivi, ikiwemo malighafi, teknolojia, utaalamu, uhandisi, na ufadhili.

Enyi Waislamu, katika ardhi ya Al-Zaytuna, vyuo vikuu vya zamani zaidi duniani:

Mfumo wa Khilafah, unaotabanni mtazamo wa kipekee wa Kiislamu kuhusu elimu, leo una uwezo wa kuanzisha mfumo wa kielimu wa daraja la kwanza, mfumo unaochanganya kutafuta maarifa na kutimiza masuala muhimu na maslahi ya dola na jamii vile vile, na wakati huo huo unahakikisha kujitosheleza katika kila kitu ambacho Ummah unahitaji; kitu ambacho kitakomesha utengano huu kati ya mifumo ya elimu katika ardhi zetu na mahitaji ya jamii zetu za viwanda, kilimo, kiufundi, na mengineyo, kitu ambacho kilisababisha kutegemea dola zengine. Hii, pamoja na uwekezaji mkubwa wa Dola ya Khilafah katika uwanja wa utengenezaji ili kutimiza mahitaji ya jamii kwa kujitegemea na kuifanya Khilafah kuwa dola kubwa ya kimataifa, inawezesha dola kufaidika na ujuzi na akili za kipekee za wana wa Ummah katika kuimarisha dola, ili nguvu zao za thamani zisipotee wala dola za kigeni zisiruhusiwe kuziiba.

Kwa hivyo fanyeni haraka, enyi Waislamu nchini Tunisia, kuweka mfumo huu mzuri katika utekelezaji na utabikishaji kwa kutekeleza mara moja kile ambacho Mwenyezi Mungu amewaagiza: kufanya kazi ya kusimamisha Khilafah Rashida, kwani ndio tiba pekee ya Sharia kwa masuala yenu yote.

Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:

[الَّذِينَ إِن مَّكَّنَّاهُمْ فِي الْأَرْضِ أَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ وَأَمَرُوا بِالْمَعْرُوفِ وَنَهَوْا عَنِ الْمُنكَرِ وَلِلَّهِ عَاقِبَةُ الْأُمُورِ]

“Wale ambao tukiwapa madaraka katika nchi husimamisha Sala, na wakatoa Zaka, na wakaamrisha mema, na wakakataza mabaya. Na kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo ya mambo yote.” [Surat Al-Hajj:41].

H. 20 Rabi' II 1447
M. : Jumatano, 12 Novemba 2025

Hizb-ut-Tahrir
Tunisia

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.