Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
H. 10 Muharram 1447 | Na: Afg. 1447 H / 01 |
M. Jumamosi, 05 Julai 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Utambuzi wa Urusi wa Serikali ya Afghanistan: Hatua Zaidi ya Kuzuia Kuibuka kwa Mfumo wa Kiislamu katika Kanda hii
(Imetafsiriwa)
Mnamo siku ya Alhamisi, Urusi ilitangaza kuwa imekubali rasmi stakabadhi za utambulisho za balozi mpya wa Afghanistan, na hivyo kuwa nchi ya kwanza kuitambua serikali hii inayoongozwa na Taliban.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Afghanistan inauona utambuzi huu kama sehemu ya mchakato mpana ambao kwao utawala wa sasa utayeyushwa hatua kwa hatua ndani ya mfumo wa kimataifa wa kisekula wa dola ya kitaifa. Mfumo huu, baada ya muda, utaiweka mbali serikali hii na lengo kuu la Kiislamu la kusimamisha na kubeba Dini ya Mwenyezi Mungu (swt). Zaidi ya hayo, utambuzi huo unaweza kuigeuza Afghanistan kuwa uwanja wa vita vya kiushindani kati ya dola za kikanda na kimataifa.
Tangu mabadiliko ya serikali nchini Afghanistan, Urusi imejitahidi sana kujenga mahusiano thabiti na mamlaka hizi mpya. Mabadiliko haya ya kisiasa yanatokana na wasiwasi wa usalama wa kitaifa wa Urusi na maslahi yake ya kimkakati katika Asia ya Kati. Moscow inahofia kuinuka kwa Uislamu wa kisiasa, kusimamishwa tena kwa Khilafah, na kuunganishwa kwa Ummah. Inatarajia serikali ya sasa ya Afghanistan kuwakandamiza Mujahidina katika Asia ya Kati. Kwa sababu hii, mnamo 4 Julai 2024, Rais Putin alitangaza waziwazi: "Taliban hakika ni washirika wetu katika mapambano dhidi ya ugaidi." Kauli kama hiyo inaonyesha wazi mtazamo wa kijanja na muhimu wa Urusi juu ya serikali ya Afghanistan.
Utambuzi, kwa maneno ya leo, ni ala ya kisasa ya kisiasa inayotumika kutumikia maslahi ya kitaifa ya dola zenye nguvu. Ni upendeleo wa kisiasa ambao Urusi imetoa kwa kuzingatia hesabu zake za kimkakati pekee—na inatarajia serikali ya Afghanistan kufuata na kudumisha upendeleo huu kwa kutanguliza maslahi ya kimada pekee, na kuachana na vipimo vyengine vyote, ikiwemo maadili na kanuni za Kiislamu. Huku Rais wa Marekani Donald Trump akitoa matarajio sawia na hayo kutoka kwa utawala mpya wa Syria. Wasiwasi kama huo unaofanana miongoni mwa dola zisizo za Kiislamu unaonyesha mkakati wao wa pamoja: kuudhibiti Uislamu wa kisiasa na kuzuia kuibuka kwa mfumo wa Kiislamu katika eneo hili.
Fauka ya hayo, hamu ya kupata upendeleo wa kisiasa kama huo kutoka kwa dola hasimu kama vile Urusi haitokani na imani ya Kiislamu, bali katika fikra iliyoundwa na kuwezekana kiakili na mitazamo yenye mwelekeo wa faida. Vile vile, Amanullah Khan alituma barua rasmi kwa Vladimir Lenin, akiomba uungwaji mkono wa kisiasa kutoka Umoja wa Kisovieti, ambao ukawa dola ya kwanza kuutambua utawala wake. Hata hivyo kihistoria—na hata hivi sasa chini ya Vladimir Putin—Urusi inasalia kuwa miongoni mwa maadui sugu sana wa Uislamu na Waislamu na kikwazo kikubwa kwa umoja wa Umma wa Kiislamu. Uhalifu wake dhidi ya Waislamu nchini Urusi, Asia ya Kati, Caucasus, Syria, Afghanistan na maeneo mengine ni jambo lisilopingika.
Bila shaka, mahusiano ya kidiplomasia, kisiasa na kiuchumi na dola za kikafiri yanatambulika katika Uislamu na yana mfano wa kihistoria. Tangu zama za Mtume Muhammad (SAW) hadi zama za Makhalifa Waongofu na baadaye, mahusiano ya kigeni ya Waislamu daima yaliongozwa na imani ya Kiislamu na kanuni ya al-walāʾ wal-barāʾ. Sera ya mambo ya nje ya Khilafah ilitumika kueneza Uislamu kupitia Dawah na Jihad ili kupanua utawala wa Kiislamu. Mfano mmoja wa wazi ni ule wa Mtume (saw) kutuma wajumbe kwenye makasri ya wafalme wa wakati huo.
Diplomasia katika Uislamu inategemea kanuni kama vile idhhār-u-dīn, al-walāʾ wal-barā, na uainishaji wa ardhi kama Dār ul-Islām au Dār ul-Kufr. Fahamu hizi hazina nafasi katika mfumo wa dola ya kitaifa; kwa kweli, aghlabu huchukuliwa kama hatari. Serikali ya sasa inaweza tu kufuata sera ya kigeni ya Kiislamu na diplomasia ikiwa inalenga kuasisi mfumo wa kisiasa unaokita mizizi katika Uislamu wenyewe—usio oanishwa ndani mfumo wa kisekula. Hili linawezekana tu kwa kusimamisha tena dola ya pili ya Khilafah Rashida. Vyenginevyo, dola ya sasa polepole itaingia kwenye upotovu, unaoendeshwa na uhalisia wa kisiasa na kuzongwa ndani ya mfumo wa kisekula wa kilimwengu.
Cha kusikitisha, huu ndio upotofu wenyewe wa kisiasa ambao watawala wengine katika ulimwengu wa Kiislamu wameingia ndani yake—na wanaendelea kutembea ndani yake hadi leo—na kusababisha mikono yao kufungwa na vikwazo vya mfumo wa kimataifa.
[ٱلَّذِينَ يَتَّخِذُونَ ٱلۡكَٰفِرِينَ أَوۡلِيَآءَ مِن دُونِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَۚ أَيَبۡتَغُونَ عِندَهُمُ ٱلۡعِزَّةَ فَإِنَّ ٱلۡعِزَّةَ لِلَّهِ جَمِيعًا]
“Wale ambao huwafanya makafiri kuwa ndio marafiki badala ya Waumini. Je! Wanataka wapate kwao utukufu? Basi hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu.” [An-Nisa' 4:139]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Afghanistan |
Address & Website Tel: http://hizb-afghanistan.org/ |
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org |