Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
H. 1 Safar 1447 | Na: H 1447 / 004 |
M. Jumamosi, 26 Julai 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir Chazindua Kampeni ya Kimataifa
“Vita vya Sudan: Hadithi ya Ukoloni, Usaliti na Udanganyifu”
(Imetafsiriwa)
Mgogoro wa kikatili nchini Sudan kati ya Wanajeshi wa Sudan (SAF) wanaoongozwa na mtawala mkuu wa Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) kinachoongozwa na Mohamed Hamdan Dagalo (Hemedti), ambaye hapo awali alikuwa naibu wa al-Burhan katika Baraza Kuu, sasa umeingia mwaka wake wa tatu, na kusababisha vifo vya maelfu ya raia. Baadhi ya makadirio yanaweka idadi ya waliofariki katika vita hivi vya kipumbavu kufikia 150,000, huku kukiwa na ukatili wa kutisha uliofanywa na pande zote mbili, ikiwa ni pamoja na mauaji ya kinyama, mateso, ubakaji mkubwa na uhalifu mwingine wa kingono dhidi ya wanawake na wasichana. Mauaji ya kikabila pia yameripotiwa, huku jamii nzima zikiteketezwa kwa moto na kuangamizwa, na mauaji ya halaiki katika miji mbalimbali, vijiji na kambi za watu waliokimbia makaazi yao. Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Turk, alisema kuwa “hofu inayoendelea nchini Sudan haina kikomo”. Mzozo huo pia umesababisha mgogoro mkubwa zaidi wa kibinadamu ulimwenguni, na zaidi ya watu milioni kumi na nne wamelazimika kuyahama makaazi yao, na kusababisha mgogoro mkubwa zaidi wa watu kuhamishwa ulimwenguni. Zaidi ya hayo, nusu ya wakaazi milioni 50 wanakabiliwa na njaa, huku Shirika la Mpango wa Chakula Duniani likithibitisha kuwa kuna njaa katika maeneo 10, ikiwa ni pamoja na kambi ya Zamzam, ambayo ni makaazi ya watu 400,000 waliokimbia makaazi yao, na kuonya kwamba inaweza kuenea zaidi, kuweka mamilioni katika hatari ya njaa, na kusababisha "janga kubwa zaidi la njaa duniani". Pande zote mbili zimetumia njaa kama silaha ya vita kwa kuzuia kuingia kwa chakula kwenye maeneo yanayoshikiliwa na mwengine. Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Catherine Russell alielezea maafa ya kibinadamu nchini Sudan kama, “sio tu mgogoro, ni mgogoro wa aina nyingi unaoathiri kila sekta, kuanzia afya na lishe hadi maji, elimu na ulinzi.”
Hata hivyo, umwagaji damu na maafa ya kibinadamu yanayotokana na mzozo huu haujapata usikivu wa kimataifa na utangazaji wa vyombo vya habari vya kimataifa unaostahiki, wala jitihada za dhati hazijafanywa kukomesha umwagaji damu. Ni vita ambavyo vimetengwa, kusahauliwa au hata kupuuzwa kutokana na mizozo katika sehemu nyingine za dunia - na kutajwa kama “mgogoro usioonekana na uliofichika”. Hivyo basi, Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kimezindua kampeni ya kimataifa ya kuleta angazo la kimataifa juu ya kuzorota kwa maafa ya kibinadamu na kiwango cha kutisha cha mateso, ugaidi, na unyama unaowasibu watu wa Sudan. Kampeni hii, yenye kichwa: “Vita vya Sudan: Hadithi ya Ukoloni, Usaliti na Udanganyifu”, pia itashughulikia siasa na ajenda zilizofichwa nyuma ya mzozo huu wa sasa, pamoja na dola za kikanda na kimataifa zinazohusika katika kuanzisha na kufadhili vita kwa maslahi yao ya kibinafsi ya kisiasa na kiuchumi, wakitumaini kufaidi kutokana na rasilimali tajiri na umuhimu mkubwa wa kisiasa za kijiografia wa Sudan. Kampeni hii pia itaelezea historia ya Sudan na sababu, ikiwa ni pamoja na uingiliaji kati wa wakoloni katika ardhi hiyo na utawala wa kidikteta uliopandikizwa na nchi za magharibi, ambao uliweka msingi wa migawanyiko ya kikabila, kijamii na kidini kati ya watu wake ambayo yalianzisha vita mbalimbali ambavyo vimeharibu nchi hiyo kwa miongo kadhaa, pamoja na kusababisha kufeli kwa uchumi wa dola hiyo.
Na hatimaye, kampeni itaangazia jinsi matatizo ya kisiasa, kiuchumi, na kijamii ya Sudan, pamoja na mzozo huu wa sasa kamwe hayawezi kutatuliwa na mfumo wa Kidemokrasia ambao umethibitisha kushindwa kupata kwa ufanisi mahitaji ya watu katika nchi zote kote ulimwenguni, pamoja na kutulia tuli au hata kushiriki katika mauaji mbalimbali ya halaiki, ikiwemo Gaza, Kashmir, Myanmar na Syria. Bali, matatizo mengi ambayo Sudan na ulimwengu wote wa Kiislamu unakabiliwa nayo, yanaweza tu kutatuliwa chini ya sheria, mifumo, na taasisi za Dola ya Khilafah ambayo imethibitisha kihistoria uwezo wake wa kuleta ustawi, maendeleo na mifumo ya afya na elimu ya hali ya juu pamoja na kuhakikisha uwiano kati ya makabila, jamii na imani za kidini tofauti tofauti ili kujenga dola yenye mafanikio na ufanisi.
Kampeni hii inaweza kufuatiliwa katika: https://www.muslimworld.today/en/index.php/hizbuttahrir/27941.html
Facebook: Ht-cmo-ws
Instagram: WomenShariah5
X: @WSCMOHT1924
Link ya video ya kampeni: https://dai.ly/k6nOUveV7mmeAODubVW
﴿يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ﴾
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Surah Al-Anfal: 24]
Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.muslimworld.today |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@muslimworld.today |