Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Australia

H.  3 Jumada II 1447 Na: 06 / 1447 H
M.  Jumatatu, 24 Novemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kongamano la 2025 la Hizb ut Tahrir / Australia ‘Uislamu: Mabadiliko Ambayo Ulimwengu Inahitaji Sana’ Lahitimishwa kwa Mafanikio Makubwa

(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Australia ilikamilisha kwa mafanikio Kongamano lake la 2025 katika mazingira mazuri ya tafakari ya dhati na wasiwasi wa kweli kuhusu hali ya wanadamu na mwelekeo wake wa baadaye. Kongamano hilo lilijaa hotuba zenye hisia kali na hadhira iliyotiwa moyo na lilijumuisha ujumbe wa video unaotetemesha moyo kutoka katikati mwa Gaza iliyoharibiwa.

Hadhira ilipokea hotuba nne za kina, kila moja ikitafakari matatizo ya kimfumo yanayokabiliwa leo na mwitikio wa kipekee wa Uislamu kwayo.

Hotuba ya kwanza iliturudisha zama za nyuma ili kuelewa mizizi ya kihistoria, kisiasa na kimfumo ya dhulma za kisasa. Tafakari muhimu zilijumuisha kutengwa kwa Mungu wakati wa mwangaza wa Ulaya, kuinuliwa kwa siasa za Machiavelli ambapo lengo huja kuhalalisha njia, kuibuka kwa ukoloni, uundaji wa dola ya kisasa na unyonyaji mkubwa wa kiuchumi. Dhuluma ambazo hazikufanywa tu na dola binafsi, bali zikawa za kimfumo, na baadaye za kilimwengu, na kusababisha uharibifu mkubwa kwa ulimwengu mzima.

Hotuba ya pili ilishughulikia dhulma za kiuchumi duniani, ikiangazia vyanzo vitatu vikuu vya unyonyaji wa kiuchumi ikiwemo kujumuishwa kwa biashara na siasa, mfumo wa sarafu ya fiat wa pesa za karatasi zisizo na thamani na unyonyaji wa riba na mtego wake katika kila nyanja ya mzunguko wa uchumi wa kisasa. Hotuba hiyo iliangazia njia badali ya kipekee ya Uislamu badala ya dhulma hizi tatu, ikielimisha hadhira kuhusu amri za kiwahyi za Uislamu ambazo haziko wazi kujadidishwa na maslahi yoyote, sharti la sarafu inayoungwa mkono na dhahabu na fedha na kuharamishwa kwa riba na Uislamu ambayo inahakikisha mzunguko mzuri wa utajiri na kuzuia matajiri kupata utajiri kwa kuwa matajiri pekee.

Hotuba hiyo pia iliwafahamisha hadhira kuhusu mfumo wa kipekee wa usambazaji wa mali wa Uislamu, unaotofautisha kati ya mali ya kibinafsi, mali ya umma na mali ya dola - muundo unaosimamia ipasavyo shughuli za kiuchumi ili kuhakikisha ugavi sawa wa mali kwa watu binafsi na jamii kwa jumla. Cha kushangaza, hadhira ilifanyiwa uwasilishaji muhimu wa mfumo wa kiuchumi wa Uislamu kivitendo, kwa kutumia takwimu za Australia kama mfano, ambapo mabadiliko ya kimfumo katika usambazaji wa mali yalifikiwa, na kuwaacha watu binafsi na serikali katika nafasi nzuri zaidi ya kiuchumi licha ya kuondolewa kwa majukumu ya kodi karibu yote.

Hotuba ya tatu ilizungumzia kiini cha wasiwasi wa kila mtu - kuoza kwa maisha ya kisasa na athari zake kwa mtu binafsi, familia na jamii. Ilikuwa ombi la dhati la kutafakari juu ya athari za ulimwengu unaobadilisha ibada ya Mungu kwa ibada ya nafsi. Ufahamu wa kina wa Uislamu katika kurekebisha nyoyo na akili, unaobadilisha kila nyanja ya jamii, ulikuwa wa kina sana na kuwaacha hadhira wakiwa wamebadilika kikweli. Muhimu zaidi, dokezo kuhusu utupu wa dhana za kisasa za ‘mshikamano wa kijamii’ liliwasilishwa, likifichua wito huu kama sharti la kugeukia dhulma. Mfumo wa kweli wa Uislamu wa mshikamano, ambao unasimama peke yake kama mfumo wa dhahabu wa kuishi pamoja, uliwasilishwa kwa njia tata na kuwaacha hadhira wakishangaa.

Hotuba ya nne ilizungumzia suala la Khilafah na kuibuka kwake kwa ulimwengu wa leo kuna maanisha nini. Kuondoa msisimko unaofuata mazungumzo kuhusu Uislamu, hasa mazungumzo kuhusu mfumo wake wa kisiasa, hotuba hiyo ilifichua baadhi ya propaganda za uongo zinazohusiana na Khilafah - zinazoenezwa na viongozi wa kisiasa wa Australia, ikiwa ni pamoja na hivi karibuni Mkurugenzi Mkuu wa ASIO. Hotuba hiyo ilielezea umuhimu wa Khilafah katika Uislamu, kuwepo kwake kimaumbile kwa zaidi ya miaka 1,300 katika ulimwengu wa Kiislamu, na jinsi, kimsingi, inavyowakilisha si zaidi ya hamu ya Waislamu kuishi kwa Uislamu wao.

Hotuba hiyo iliwakumbusha hadhira kwamba matatizo mengi ya kimfumo yanayokabiliwa katika ulimwengu wa Kiislamu ni matokeo ya moja kwa moja ya urithi wetu wa kikoloni. Khilafah iliwasilishwa kama tiba ya kimaumbile ya kukosekana kwa utulivu, ukosefu wa usalama, ufisadi na maendeleo duni yanayopatikana katika sehemu hiyo ya dunia. Hadhira iliulizwa kwa hisia kali ni jambo baya lilioje Waislamu kutafuta kiwango kikubwa cha uhuru wa kiuchumi, au utulivu mkubwa wa kisiasa, au usemi mkubwa zaidi kuhusu uingiliaji wa kigeni - hamu ambayo ni ya kawaida kwa watu wote.

Mwishowe, hadhira iliwasilishwa kwa ombi la dhati kutoka katikati ya Gaza iliyoharibiwa, ambapo ombi la shauku lilitolewa likiwakumbusha hadhira kwamba uharibifu wa Gaza na mauaji ya halaiki ya kimfumo ya watu wake ni dalili ya kile ambacho ni kibaya kwa ulimwengu wa leo. Nguvu zile zile zilizoharibu Gaza ndizo nguvu zile zile zinazoharibu ulimwengu mzima. Hadhira ilikumbushwa jukumu zito lililoko mabegani mwa Waislamu sio tu kukabiliana na dhulma hizi, bali pia kuongoza wanadamu kuelekea mustakabali bora. Ombi la ajabu, ambapo walio na huzuni zaidi duniani leo walionyesha hamu zaidi kuhusu hatima ya wengine kuliko wao wenyewe!

Licha ya hofu iliyotangulia kongamano hilo, iliyosukumwa na wanasiasa, vyombo vya habari na hata wakuu wa ujasusi, jamii ilikusanyika kwa fahari kuhakikisha ujumbe mzuri wa Uislamu kamwe hautamezwa na kelele za waenezaji wa vita na watetezi wa mauaji ya halaiki. Ushuhuda wa upendo wa kina wa Uislamu unaohisiwa na Waislamu kila mahali na hamu ya dhati ya kuwaruhusu wengine fursa ya kuona utukufu wake pia.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Australia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Australia
Address & Website
Tel: 0438 000 465
www.hizb-australia.org
E-Mail:  media@hizb-australia.org

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.