Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  25 Jumada II 1447 Na: H 1447 / 034
M.  Jumanne, 16 Disemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kilio cha Haraka cha Msaada, Enyi Ummah wa Kiislamu!
(Imetafsiriwa)

Wanawake na watoto wa Gaza wanalilia msaada... wanawake na watoto wa Sudan wanalalamika... wanawake na watoto wa Uyghur huko Turkestan Mashariki wanateseka na kupiga kelele... Wanawake wa Kiislamu na watoto wao kila mahali wanapaza kilio baada ya kilio, wakiita: Je, kuna mtu yeyote wa kusaidia? Je, kuna mtu yeyote wa kuitikia wito? Je, kuna mtu yeyote wa kujibu?!

Enyi Umma bora uliotolewa kwa ajili ya wanadamu: Ni nini kimewapata? Mnatazama mwili wenu unaougua lakini hamsisimki? Kila mahali mnapowaona watoto wenu wakinyanyaswa na kudhalilishwa, damu na heshima yao ikikiukwa, na nyinyi hamuinuki?!

Watu wa Gaza wanakufa kwa baridi, wanauawa, wanafukuzwa makaazi, na hulala njaa usiku kucha, huku ulimwengu ukipuuza vilio vyao vya kuomba msaada! Watu wa Sudan wanazikwa wakiwa hai, na vitendo vya ukatili vinafanywa kwa uangalifu dhidi yao na wanawake wao! Na Waislamu wa Turkestan Mashariki wanashuhudia vita vikali zaidi vya ukomunisti, ambavyo vinafanya kazi ya kuwageuza mbali na Dini yao na kuwang'oa watoto wao kutoka kwenye mizizi yao ya Kiislamu!

Kwa hivyo muko wapi? Je, mumeshayazoea matukio na habari, na je damu katika mishipa ya watoto wenu imeshaganda, kiasi kwamba udugu katika dini hauwachochei tena, wala ulinzi wa heshima, wala uhamasishaji wa kuilinda ardhi hii na nyengizo?!

Enyi Umma wa Kiislamu: Katika kila sehemu ya dunia, watoto wenu wanashuhudia vita dhidi ya Dini yao; wale wanaoendesha mfumo wa kibepari wa kimataifa wanataka kuwayeyusha katika hadhara yao wa kisekula na kufuta fahamu zao za Kiislamu. Imedhihirika kwenu kwamba vita hivi ni vita vya hadhara, na msiposhinda kwa ajili ya hadhara yenu ya Kiislamu, hali itakuwa mbaya zaidi, na mtashuhudia maumivu makubwa na hasara kubwa zaidi.

Enyi Umma wa Kiislamu: Maadui zenu wanajua vyema kwamba nguvu zenu ziko katika kurudi kwenu kwenye Kitabu cha Mola wenu Mlezi (swt) na Sunnah ya Mtume Wake (saw), na katika kuzitendea kazi chini ya dola inayowakusanya Waislamu wote na kuwalinda. Kwa hivyo, wanalinda kwa uangalifu mipaka hiyo ya kuchukiza na kuwateua wale wanaofanya kazi ya kuilinda na kuihifadhi kama kizuizi kisichoweza kupenyeka dhidi ya umoja wa Ummah na kuungana kwake.

Enyi Umma wa Kiislamu: Mnashuhudia maumivu ya kiungo kimoja baada ya chengine kutoka mwilini mwenu, huku viungo vyengine visiweze kuulinda au kukabiliana na kile kinachoutishia na vyengine kwa magonjwa na hatari, kwa sababu vimegawanyika na kuwa dhaifu, na kwa sababu vimeachana na chimbuko la nguvu na heshima yao na sheria ya Mola wao Mlezi.

Enyi Umma bora uliotolewa kwa ajili ya wanadamu: Sisi, katika Kitengo cha Wanawake cha Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, tunahisi maumivu ya kile kilichowasibu watu wetu katika nchi zote, na tunashuhudia mbele ya Mwenyezi Mungu kwamba tunahisi maumivu na tunatarajia kutoka kwa Mwenyezi Mungu kile wanachokitarajia: Ushindi Wake, Tamkini Yake, na kurudi kwa Uislamu kama mfumo kamili wa maisha yetu, kuwaangaza na kuwatawala kwa haki, uadilifu, na rehema zake.

Enyi Umma wa Kiislamu: Tunatumaini kwamba mtasikia wito wetu na kuwasukuma wana wetu miongoni mwa wanazuoni na wahubiri kusema ukweli, kuelimisha akili, na kufafanua njia ya wokovu kwa watu. Tunakuombeni muwasihi wana wetu miongoni mwa maafisa na wanajeshi kuinuka kama kundi moja ili kuinusuru Dini hii na kunyanyua ujumbe wake:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللَّهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ] “Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Muhammad: 7].

Ewe Mwenyezi Mungu, shuhudia kwamba tunajitahidi na kufanya kazi pamoja na wafanyikazi wenye ikhlasi ili kusimamisha Khilafah Rashida ya pili, ambayo itakomesha maumivu ya Ummah wetu katika nchi zote na itaulinda na wote wanaoishi chini ya kivuli chake. Tunamwomba Mwenyezi Mungu atukubalie, tuwe imara, na aharakishe kusimamishwa kwake kama rehema kwa walimwengu wote.

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.muslimworld.today
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@muslimworld.today

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.