Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
| H. 14 Dhu al-Hijjah 1447 | Na: H 1447 / 086 |
| M. Jumapili, 31 Mei 2026 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Enyi Ummah wa Kiislamu na Majeshi Yake:
Ikiwa Hamkasirishwi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mambo Yake Matakatifu,
Basi Mtakasirishwa na Kuchukua Hatua kwa ajili ya Nini?!
(Imetafsiriwa)
Mnamo Jumatano, 27/5/2026, vyombo vya habari na mitandao ya kijamii vilirusha picha zinazoonyesha vikosi vya umbile la Kiyahudi vikimshambulia kikatili mwanamke mchanga wa Kipalestina huko Bab Hutta, moja ya malango ya Msikiti mtukufu wa Al-Aqsa, vikimnyang'anya kitambaa chake cha kichwani kwa nguvu kabla ya kumkamata. Tukio hili linajiri huku kukiwa na ongezeko la ukiukwaji wa sheria na hatua za usalama ulioongezeka kutoka kwa vikosi vya uvamizi katika milango ya kuingia katika Jiji la Kale la Al-Quds na malango ya Msikiti wa Al-Aqsa, sanjari na Idd al-Adha. Waliweka vituo vya ukaguzi na kuchunguza vitambulisho vya wapita njia, wakizuia idadi kubwa ya watu kuingia msikitini.
Moyo unauma kwa maumivu na jicho linalia damu badala ya machozi kwa uhalifu wa kinyama kama huo na shambulizi la kikatili kwa mwanamke huru miongoni mwa wanawake huru wa Al-Quds. Kinachoongeza maumivu makali ni kwamba hijab yake kichwani ilivuliwa na stara yake ikaanikwa wazi mita chache kutoka Masra, eneo la Safari ya Usiku ya Mtume wetu (saw), mikononi mwa wale ambao ghadhabu ya Mwenyezi Mungu imewaangukia na ambao amewapishitia fedheha na udhalilifu. Kinachosikitisha zaidi ni kwamba hii si mara ya kwanza kwa wanawake huru wa Ardhi Iliyobarikiwa kushambuliwa kwenye malango ya Msikiti wa Al-Aqsa, ndani ya nyua zake, na katika Jiji la Kale la Al-Quds. Umbile hili la kihalifu limepitiliza na kuzidisha jinai na ukiukaji wake dhidi ya watu wa Ardhi Iliyobarikiwa kwa ujumla na wanawake huru wake haswa baada ya operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa. Pia limetoa ulinzi kamili na hifadhi kwa makundi yake ya walowezi kufanya uhalifu huu.
“Kwa jambo kama hilo, moyo huyeyuka kwa huzuni ... ikiwa kuna Uislamu au imani yoyote iliyobaki moyoni”
Enyi Waislamu: Tukio hili chungu lilitokea katika siku iliyobarikiwa ya mwezi mtukufu, siku ambayo mahujaji hufanya ibada zao, siku ambayo Mwenyezi Mungu ameifanya kuwa siku ya furaha kwa Waislamu. Lakini watu wa ardhi iliyobarikiwa, na wanawake wake huru, hawajui furaha wala raha siku hii. Damu yao imemwagika katika Ukingo wa Magharibi, Gaza, na Al-Quds; nyumba zao zimebomolewa; ardhi zao zinachukuliwa; na miti yao inang'olewa kwa ajili ya makaazi kujengwa mahali pao. Wafungwa wao, wale wanaoingia gerezani, wamepotea, na wale wanaoondoka ni wale waliozaliwa hivi karibuni, wanaopitia mateso, uhalifu, ukiukaji wa heshima, kunyimwa chakula na matibabu. Ukandamizaji na kunyongwa kuna lazimishwa juu yao ili kuwalazimisha kutoka majumbani mwao. Masra ambayo Mwenyezi Mungu ameiunganisha na Msikiti Mtukufu ambapo mahujaji hufanya ibada zao masiku haya, unafanywa kuwa wa Kiyahudi, na juhudi zinaendelea kulazimisha mgawanyiko wa kihekalu ndani yake. Hakika, mipango ya kuubomoa na kujenga hekalu linalodaiwa kwenye magofu yake inatangazwa waziwazi, na makundi ya walowezi wanaunajisi asubuhi na jioni, wakifanya sala zao na ibada za Talmud katika nyua zake na kuinua bendera zao huko.
Mnawezaje kufurahia maisha huku watu wa Ardhi hii Iliyobarikiwa wakiteseka?! Mnawezaje kufurahia maisha huku wanawake huru wakidhalilishwa, wakishambuliwa, na kuvuliwa stara yao, wakiomba msaada bila mtu wa kujibu kilio chao?! Muko na shida gani?! Je, mumependezwa na kustarehe na maisha haya ya kidunia?
Enyi watu wenye nguvu na ulinzi, Enyi majeshi ya Waislamu: Hali imefikia hatua muhimu, na umbile hili lisilo na mamlaka limezidi katika uhalifu wake. Hakuna hata mmoja wenu anayeweza kutoa udhuru, si mbele ya Mwenyezi Mungu wala mbele ya waja Wake. Baada ya ukatili na unyama huu wote, ambao wanadamu, wala miti, wala mawe hayajaepushwa, bado mnabaki kuwa watiifu?! Kama hamtainuka kwa hasira kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kwa ajili ya kile kilicho kitakatifu, basi mtainuka kwa hasira na kutenda kwa ajili ya nini?! Je, hakuna miongoni mwenu atakayeutetea Uislamu na Waislamu, na kuwa kama Aws na Khazraj waliomnusuru Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na kula kiapo cha utiifu kwake katika zama kama hizi?! Ewe Mola, tupe maanswari kama maanswari wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), ambayo kupitia wao Dini itaimarishwa, vilio vya wale wanaotafuta msaada vitajibiwa, na kupitia wao bishara njema za Mtume wako (saw), zitatimizwa kwa kusimamishwa kwa Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.
Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.muslimworld.today |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@muslimworld.today |