Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
| H. 24 Dhu al-Hijjah 1447 | Na: H 1447 / 088 |
| M. Jumatano, 10 Juni 2026 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mtoto Aliyeuawa Shahidi, Kuhesabiwa kwa Waathiriwa Kutaisha Lini? Watu wa Damu hiyo Watainuka Lini Kuwalipiza Kisasi?
(Imetafsiriwa)
Wizara ya Afya ya Palestina ilisema kwamba vikosi vya uvamizi vilifyatua risasi kwenye gari moja lililokuwa limebeba raia wa Palestina katika mji wa Hebron katika Ukingo wa Magharibi wa kusini unaokaliwa kimabavu, na kusababisha kifo cha kishahidi cha mtoto mchanga wa miezi saba Sam Abu Hikal huku akiwa mikononi mwa mamake. Mamake na babake pia walijeruhiwa.
Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, katikati ya ukali wa vita dhidi ya Gaza, dunia imekimbilia kuwahesabu waathiriwa. Pumzi zilishikiliwa huku idadi ikiongezeka kwa kasi, makumi kwa makumi, hatimaye kufikia makumi ya maelfu ya mashahidi. Lakini baada ya wadhamini na wapatanishi kuingilia kati na miili ya wale waliouawa kutoka kwa umbile la Kiyahudi kukabidhiwa, dunia ilisahau kazi yake ya kuwahesabu mashahidi.
Ukingo wa Magharibi unashiriki maumivu ya Gaza kama vile unavyoshiriki uvamizi. Shahidi baada ya shahidi anapanda daraja. Baba anauawa shahidi mlangoni mwa hospitali huku akimsubiri mtoto wake aje duniani. Wanawake na watoto wanauawa. Mtoto machanga Sam ni shahidi mwengine ambaye ameondoka kwenda Peponi kabla hata ya kutamka neno “Mama.” Lakini umbile la Kiyahudi halijui chochote ila chuki, inayoshajiishwa na marabi kutoka katika maandiko yao na kuingizwa akilini mwa wanajeshi wao: muueni kila Mpalestina, waangamizeni, na viuueni vijusi vilivyo tumboni mwa mama zao.
Hivi kwa nini maafisa na askari wa majeshi ya Waislamu wanabaki bila kujali? Muna nini kwamba, mnapoambiwa mtembee katika njia ya Mwenyezi Mungu, mnakwamilia vikali ardhini? Muna nini kwamba, mnapoambiwa msimame na kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa, mnajifunika nguo zenu? Ni lini mtaacha kuichukulia damu ya mashahidi wetu kama takwimu tu na kuanza kuhisi uzito wa imani iliyo juu ya mabega yenu? Wallahi, mnawajibika, na kila tone la damu litasimama dhidi yenu katika Siku kubwa ambapo nyoyo zitazidiwa na macho yatatazama kwa hofu. Kisha hakuna mtawala wala afisa atakayeweza kukushufaieni. Mtakufa, na malaika watazichukua roho zenu, na mtaambiwa:
[وَلَقَدْ جِئْتُمُونَا فُرَادَىٰ كَمَا خَلَقْنَاكُمْ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَتَرَكْتُم مَّا خَوَّلْنَاكُمْ وَرَاءَ ظُهُورِكُمْ وَمَا نَرَىٰ مَعَكُمْ شُفَعَاءَكُمُ الَّذِينَ زَعَمْتُمْ أَنَّهُمْ فِيكُمْ شُرَكَاءُ لَقَد تَّقَطَّعَ بَيْنَكُمْ وَضَلَّ عَنكُم مَّا كُنتُمْ تَزْعُمُونَ]
“Nanyi mlitujia wapweke kama tulivyo kuumbeni mara ya kwanza. Na mkayaacha nyuma yenu yote tuliyo kupeni, na wala hatuwaoni hao waombezi wenu, ambao mlidai kuwa ni washirika wa Mwenyezi Mungu kwenu. Yamekatika makhusiano baina yenu, na yamekupoteeni mliyo kuwa mkidai.” [Surah Al-An‘am: 94].
Basi jitokezeni kwenye heshima ya dunia hii na Akhera, na kumbukeni maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ انفِرُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الْأَرْضِ أَرَضِيتُم بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الْآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ * إِلَّا تَنفِرُوا يُعَذِّبْكُمْ عَذَاباً أَلِيماً وَيَسْتَبْدِلْ قَوْماً غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّوهُ شَيْئاً وَاللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ]
“Enyi mlio amini! Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache. * Kama hamwendi atakuadhibuni adhabu chungu, na atawaleta watu wengine, wala nyinyi hamtamdhuru chochote. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.” [Surah At-Tawbah: 38–39].
Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.muslimworld.today |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@muslimworld.today |