Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
H. 10 Safar 1447 | Na: BN/S 1447 / 01 |
M. Jumatatu, 04 Agosti 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mbele ya Serikali za Khiyana, Msikiti wa Al-Aqsa Unabadilishwa Kuwa Mahali Patakatifu kwa Mayahudi!!
(Imetafsiriwa)
Mbele ya macho ya watawala wa Waislamu, Mayahudi wamekuwa wakivamia eneo la Msikiti wa Al-Aqsa, uvamizi baada ya uvamizi, ambao wa hivi karibuni ulikuwa wa jana, Jumapili, ukiongozwa na adui wa Mwenyezi Mungu, Ben-Gvir na idadi kadhaa ya Mayahudi wenye itikadi kali, katika uvamizi mkubwa zaidi kuwahi kutokea katika msikiti huo.
Mbele ya macho ya Mfalme wa Jordan, Sisi, Erdogan, na watawala wengine, Mayahudi wanaingia kuunajisi Msikiti wa Al-Aqsa katika kumbukumbu ya kile wanachokiita “Kuvunjwa kwa Hekalu.” Ben-Gvir anatangaza kwamba “Israel itaimarisha udhibiti wake juu ya Jerusalem na Mlima wa Hekalu,” na anatangaza, siku ya madai ya kuvunjwa kwa Hekalu lao, udhibiti wa Msikiti wa Al-Aqsa kama mahali patakatifu kwa Mayahudi.
Kwa mtazamo kamili wa Umma wa Muhammad (saw), tawala za wasaliti zinatosheka na kutoa shutuma baada ya shutuma na kutoa kauli dhaifu zisizo na maana. Je, ni nini thamani ya kauli yao, “Israel haina mamlaka juu ya Msikiti wa Al-Aqsa”? Na kuna umuhimu gani wa kuutaka Umoja wa Mataifa kuingilia kati kukomesha mashambulizi na kuwawekea mipaka walowezi? Ijapokuwa suala hilo limekwenda zaidi ya mashambulizi hadi hatua za kivitendo za kuugeuza Msikiti wa Al-Aqsa kuwa sinagogi ambapo ibada zao hufanywa.
Enyi Umma wa Muhammad (saw), enyi Umma bora ulioletewa watu:
Watawala hawa vibaraka waliwapa Mayahudi hifadhi ili kuangamiza Ukanda wa Gaza, kuua watu wake, na kuua kwa njaa. Sasa wanawapa hifadhi ili kuugeuza Msikiti wa Al-Aqsa kuwa sinagogi la ibada na sala zao. Kwa hiyo, mutafanya nini?
Imedhihirika wazi mithili mwanga wa jua la adhuhuri kwamba Msikiti wa Al-Aqsa, al-Quds, na damu ya watu wa Ardhi Iliyobarikiwa itawaathiri wale tu wanaomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na kwamba wale wanaomtamani Mwenyezi Mungu, Mtume wake na Akhera ndio pekee watakaosukumwa na wao, na kwamba ni wale tu wanaomtumikia Mwenyezi Mungu lengo la kuwepo kwao ndio watakaotegemewa kuwanusuru.
Ni wale tu waliomuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu kutoka katika Ummah huu, ili wawe ala za kubomoa viti vya utawala na mikono ya khiyana kwa ajili ya kujenga jengo la Uislamu:
Wao ni ala za uharibifu kwa serikali ambazo zimekuwa mahiri tu katika ulaji njama, usaliti, na kutoa taarifa za kulaani. Wameuchana Ummah na kuuzuia kunusuru Gaza na Msikiti wa Al-Aqsa.
Ala za ujenzi kujenga jengo la Uislamu, kuunganisha Umma na kupeleka majeshi kuukomboa Msikiti wa Al-Aqsa na ardhi iliyobarikiwa, na kuwanusuru watu wa Gaza. Ukombozi wa al-Quds unategemea kuondolewa kwa tawala za vibaraka ili Umma wa Kiislamu uweze kudhibiti mchakato wake wa kufanya maamuzi. Wito wowote unaofeli kufanya hivyo ni kurusha tu vumbi machoni na kuchelewesha ukombozi na ushindi.
[فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ الْآخِرَةِ لِيَسُوءُوا وُجُوهَكُمْ وَلِيَدْخُلُوا الْمَسْجِدَ كَمَا دَخَلُوهُ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَلِيُتَبِّرُوا مَا عَلَوْا تَتْبِيراً]
“Na ikifika ahadi ya mwisho ili waziharibu nyuso zenu, na waingie Msikitini kama walivyo ingia mara ya kwanza, na waharibu kila walicho kiteka kwa uharibifu mkubwa.” [Al-Isra 17:7]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Ardhi ya Baraka-Palestina |
Address & Website Tel: 0598819100 www.pal-tahrir.info |
E-Mail: info@pal-tahrir.info |