Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Uzbekistan

H.  29 Jumada II 1447 Na: 1447 / 06
M.  Jumamosi, 20 Disemba 2025

Maombolezo ya Rakhmatov Shukhratjon
Mmoja wa Wanaume Waliotikisa Misingi ya Utawala wa Ukandamizaji wa Karimov

(Imetafsiriwa)

Kwa huzuni na majonzi makubwa, tunaomboleza kwa Ummah mzima wa Kiislamu, na hasa kwa Waislamu wa nchi yetu, kifo cha ndugu yetu Rakhmatov Shukhratjon, ambaye alisalimisha roho yake kwa Muumba wake jana, Ijumaa, 19/12/2025.

Ndiyo, leo tumeshuhudia ndugu yetu Rakhmatov Shukhratjon Turaevich, ambaye alivumilia mateso ya utawala dhalimu wa Karimov, ambao ulishangaza ulimwengu kwa mateso yake, ukamataji, utesaji, na kuuwa wanachama wa Hizb ut Tahrir, ambao walitaka kuushinda utawala wa ukafiri kupitia kusimamisha Khilafah Rashida, ambayo inatabikisha Uislamu kama mfumo kamili wa maisha, katika safari yake ya kuelekea Akhera.

Ndugu yetu Shukhratjon alizaliwa mwaka wa 1975 katika eneo la Kashkadarya. Alitumia karibu nusu ya maisha yake katika magereza ya utawala wa Uzbekistan kati ya 1999 na 2022. Alikuwa mfano wa kuigwa, anayejulikana kwa ujasiri wake, azma, imani isiyoyumba, ukweli, na uthabiti katika kusema ukweli. Alitumia karibu robo karne gerezani katika magereza ya Chirchik, Zangyuta, Navoi, Jaslyk, na Almalik nchini Uzbekistan. Hata wakati wa kifungo chake katika magereza maarufu ya Jaslyk na Zarafshan, maarufu kwa mauaji na mateso, aliendelea kuwa jasiri na mzungumzaji, akijivunia ujasiri wake, na kuwahofisha wauaji wa utawala dhalimu wa Karimov. Alikuwa miongoni mwa wa kwanza kuvunja hadhi ya dhulma na ukandamizaji kwa neno la haki. Shujaa katika uwanja wa vita vya mapambano, na mswaliji mcha Mungu katika swala kwa Mola wake. Ndugu yetu alikuwa mfano hai wa Quran, akitembea juu ya ardhi. Aligusa nyoyo za wengi na akawa mfano hai wa unyenyekevu kwa waumini na nguvu dhidi ya makafiri. Mwishoni mwa maisha yake, Mwenyezi Mungu, kwa neema Yake, alimbariki kwa mwisho mwema. Ndugu yetu kipenzi, Shukhratjon, aliondola dunia hii mbali na mahali alipozaliwa, akiwa amehama kwa ajili ya Mola wake Mlezi. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«...إِنَّ الرَّجُلَ إِذَا مَاتَ بِغَيْرِ مَوْلِدِهِ قِيسَ لَهُ مِنْ مَوْلِدِهِ إِلَى مُنْقَطَعِ أَثَرِهِ فِي الْجَنَّةِ»

“Anapokufa mwanadamu mahali pengine kuliko pale alipozaliwa, atapimiwa nafasi peponi sawa na umbali kati ya mahali alipozaliwa na mahali alipofia.”

Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) amjaalie neema hii ndugu yetu, na tunamuomba (swt) amrehemu, amsamehe, na amjaalie daraja ya mashahidi. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) awape familia yake na wapendwa wake uvumilivu na faraja. Mwishowe, tunasema tu yale yanayomridhisha Mola wetu (swt):

[إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ] “Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na hakika kwaye yeye tutaregea.” [Al-Baqarah: 156].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Uzbekistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uzbekistan
Address & Website
Tel: 

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.