- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:
Amali za Kuhuisha Ibada za Dhu al-Hijjah za Mwaka 1447 H
Katika kuhuisha ibada za Dhul-Hijjah na kwa heshima ya Sunnah tukufu ya Mtume, Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan iliandaa maandamano ya takbira na tahlil mnamo Jumatatu, ya kwanza ya Dhul-Hijjah 1447 H. Maandamano yalianza kwenye lango la afisi ya hizb mjini Port Sudan, yakipita kwenye njia kuu, na kufikia Soko Kuu, ambapo yalifikia kilele chake katika ua wa Hoteli ya Al-Haramain, mahali pa mikutano ya kisiasa ya mji huo. Wakati wa maandamano hayo, umati mkubwa wa watu ulijiunga, wakipiga takbira na tahlil pamoja na ndugu zao, wakionyesha furaha yao kwa amali ya hizb na kusifu amali hii ya kipekee nchini, kwa mujibu wa maelezo yao.
Hizb iliandaa sherehe jijini Khartoum kuadhimisha Idd al-Adha. Mnamo Jumamosi, siku ya nne ya Idd al-Adha, sawia na 30 Mei 2026, afisi ya Hizb ut Tahrir/Sudan katika mji mkuu ilijaa watu wenye nia njema kutoka kwa vijana, wafuasi, na wanachama wa hizb waliofurika kutoka miji mitatu ya mji mkuu (Khartoum, Bahri, na Omdurman). Ustadh Ibrahim Othman Abu Khalil, msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan, alitoa hotuba ya kugusa moyo, akimpongeza Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata bin Khalil Abu Rashta, na mashababu wa hizb duniani kote, na kutoa salamu kwa Ummah mzima wa Kiislamu wakati wa Idd al-Adha. Katika hotuba yake, msemaji huyo alizungumzia hali halisi ya kisiasa na kijeshi na athari za vita vya Marekani vya kubuniwa kati ya vibaraka wake wawili nchini Sudan. Alifichua mpango wa kihalifu wa Amerika wa kutenganisha Darfur na juhudi zake za kuimarisha vibaraka wake wa kijeshi na kisiasa madarakani. Abu Khalil alionya kwamba mpango huu hautakoma hadi kusimamishwa kwa Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.
Katika mji mkuu wa utawala wa Port Sudan, mashababu wa Hizb ut Tahrir walikutana ili kubadilishana salamu kwa mnsaba huu uliobarikiwa katika afisi ya hizb mnamo Jumamosi, tarehe 13 ya Dhu al-Hijjah 1447 H, siku ya nne ya Idd al-Adha, sawia na 30 Mei 2026. Watoaji tahania walisikiliza hotuba ya Ustadh Nasser Ridha, mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan, ambapo alituma salamu kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata bin Khalil Abu Rashta, kwa mkuu wa Afisi Kuu ya Habari, kwa wakuu wa afisi za vyombo vya habari duniani, kwa wabebaji wote wa da’wah, na kwa umma mzima wa Kiislamu. Kisha mashababu wakabadilishana pongezi na kutuma salamu kwa ndugu zao, wabebaji ulinganizi, wakimwomba Mwenyezi Mungu awape uthabiti na kuwapa wanadamu Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo wanaifanyia kazi.
Katikati ya mazingira ya furaha na udugu wa kweli, mashababu wa Hizb ut Tahrir walikusanyika katika afisi ya hizb mjini Al-Qadharif mnamo Jumamosi, tarehe 13 Dhul-Hijjah 1447 H, siku ya nne ya Idd al-Adha, ili kubadilishana salamu na baraka kwa ajili ya tukio hilo. Waliunganishwa na roho ya Mwenyezi Mungu, bila uhusiano wa kifamilia kati yao, bali kwa sababu moja: kadhia muhimu inayowakabili Waislamu—kuregesha maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamishwa kwa Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume. Furaha ya Idd haikuwafanya wasahau mateso ya Ummah wa Kiislamu, kuanzia Sudan hadi Gaza iliyojeruhiwa, hadi Iran, ambayo imetelekezwa na watawala wa Waislamu, kwa uvamizi unaoendelea wa umbile la Kiyahudi dhidi ya Lebanon na nchi zengine za Kiislamu. Kadhia hizi zote, na nyenginezo, ziliimarisha azma yao ya kuregesha Ummah katika izza yake ya zamani, na walimwomba Mwenyezi Mungu awape Ummah nguvu na kuharakisha kusimamishwa kwa Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume.
Katika mji wa Al-Ubayyid, mashababu wa Hizb ut Tahrir walifanya mkutano wa salamu za Idd mnamo Ijumaa, siku ya tatu ya Idd al-Adha 1447 H, nyumbani kwa ustadh Ahmed Wada'a, mwanachama wa Hizb ut Tahrir. Ujumbe wa pongezi kutoka kwa mwanachuoni mkubwa na amiri wa Hizb ut Tahrir, Ata bin Khalil Abu Rashta, na ujumbe ulitolewa na Ibrahim Othman (Abu Khalil), msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan, ulisomwa kwa waliohudhuria, na mwitikio ulikuwa mzuri sana. Katika miji ya Kosti na Rabak katika Jimbo la White Nile, Ustadh Abdullah Adam Muhammad Raji Allah alifungua nyumba yake huko Al-Jazira Aba, akikaribisha kampeni ya da'wah na wafuasi wake Ijumaa asubuhi, siku ya tatu ya Idd al-Adha 1447 H. Mashababu walibadilishana salamu katika hafla hii na kujadili sababu za msingi za vita vinavyoendelea nchini Sudan na matukio yanayoendelea duniani kote, ambayo wanaamini yanatangaza tukio muhimu ambalo, Mungu akipenda, litabadilisha ulimwengu mzima. Wakati wa hotuba zao, mashababu waliimarisha kujitolea kwao kufanya kazi kwa bidii ili kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Pia walitoa salamu zao za Idd kwa amiri wa Hizb, mwanachuoni mkubwa Ata bin Khalil Abu Rashta, wanachama wa afisi yake, vitengo vyote vya hizb, ndugu zao katika Wilayah ya Sudan, wabebaji da'wah duniani kote, na Waislamu kwa jumla.
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan
Jumatano, 17 Dhu al-Hijjah 1447 H, sawia na 3 Juni 2026 M

- Sehemu ya Amali za Kuhuisha Ibada za Dhu al-Hijjah za Mwaka 1447 H -
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
https://muslimworld.today/sw/index.php/dawah/sudan/5396.html?print=1&tmpl=component#sigProId32e2ad7ab5

Kwa Maelezo Zaidi, Tafadhali Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
