Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 5 Muharram 1447 | Na: HTS 1447 / 01 |
M. Jumatatu, 30 Juni 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ongezeko la Wanamgambo nchini Sudan Linasonga Kaskazini!
(Imetafsiriwa)
Tangu Ijumaa, tarehe 27/6/2025, vyombo vya habari vimeripoti kuwa Rais wa Eritrea Isaias Afwerki amekubali kutoa mafunzo kwa wapiganaji elfu 50 kutoka majimbo ya Kaskazini na Mto Nile katika mafunzo ya juu ya kijeshi, kulingana na ombi lililowasilishwa na mkuu wa Jimbo la Kaskazini, Mohamed Sayed Ahmed Al-Jakoumi, mkuu wa Upande wa Kaskazini wa Makubaliano ya Juba ya Amani ya Sudan.
Tulisubiri hadi Jumapili, tarehe 29/6/2025 ili kuona mwitiko wa serikali na msimamo wake kuhusu habari hii mbaya, na majibu yalikuja ya kushangaza, kwani mkuu wa Jimbo la Kaskazini alielezea chanzo cha uchunguzi wa habari kuwa jeshi na vyombo vya usalama vimepewa taarifa juu ya mafunzo ya vikosi hivi, na akasema: "Tuna uratibu pamoja nao, na hatuwezi kuchukua hatua yoyote bila idhini yao!
Tangazo hili linajiri wakati dalili za mgawanyiko wa Sudan zikitanda, huku Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vikidhibiti majimbo ya Darfur na kudokeza kutangaza serikali sambamba, na huku ueneo na ukabila ukitawala mijadala ya kisiasa na kujikita kwa kugawanya madaraka. Kwa wakati huu, Al-Burhan anaendelea kuinua kauli mbiu, "Wanamgambo kwa Kila Jimbo!" kuunda wanamgambo wapya kila asubuhi! Hata hatari zaidi, wanamgambo wanawapa mafunzo wanachama wao nje ya nchi - nchini Eritrea, na tangazo la Al-Jakoumi linakuja katika muktadha huu!
Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, kwa kuzingatia habari hii ya kushtua, tunathibitisha yafuatayo:
Kwanza: Tumeonya mara kwa mara juu ya hatari ya kuenea kwa wanamgambo wenye silaha, kwamba wao ni zana za uharibifu wa serikali, na mwanya wa uingiliaji wa wakoloni makafiri wanaotaka kuisambaratisha na kuichana Sudan kupitia hisia ya umajimbo na mielekeo ya ubaguzi wa rangi. Na hapa mandhari hii ya kipuuzi inakamilishwa na Sudan Kaskazini sasa nayo pia ikiwa na wanamgambo wake, sawa na maeneo mengine ya Sudan!
Pili: Uislamu umeharamisha kupigana chini ya bendera za kikabila na kijahilia. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:
«وَمَنْ قَاتَلَ تَحْتَ رَايَةٍ عُـمِّيَّةٍ، يَغْضَبُ لِعَصَبَةٍ، أَوْ يَدْعُو إِلَى عَصَبَةٍ، أَوْ يَنْصُرُ عَصَبَةً، فَقُتِلَ فَقِتْلَةٌ جَاهِلِيَّةٌ»
“Mwenye kupigana chini ya bendera ya ujinga, akionyesha hasira kwa kuunga mkono uasabiya, au kuwalingania watu kwenye uasabiya, au kunusuru uasabiya, kisha akauawa, kifo chake kitakuwa ni mithili ya kile cha zama za Jahiliya (kabla ya Uislamu).”
Tatu: Kuzungumzia kuhusu wanamgambo hawa au wale kuwa chini ya uongozi wa jeshi ni kurusha tu vumbi machoni. Siku zote huanza hivi, kisha huisha kwa balaa. Tuna mfano mbaya zaidi katika RSF kwa kuunda wanamgambo.
Nne: Kupitia matendo kama hayo, serikali inataka kuimarisha mpango wa mipaka ya damu, kutekeleza Sykes-Picot mpya ya Marekani ili kuchana mabaki ya Sudan iliyosalia.
Ni faradhi kwa jeshi kuanza mara moja kuunganisha vikosi vyote vya kijeshi vilivyoenea nchi nzima chini ya bendera yake pekee, kuvifanya jeshi moja lenye nguvu lenye uwezo wa kulazimisha mamlaka ya dola, na kisha kutoa nusrah kwa Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ili kuunganisha Umma, kwa msingi wa Uislamu mtukufu, kutabikisha hukmu za Uislamu, na kung'oa ushawishi wa wakoloni makafiri kutoka kwa nchi yetu na ardhi zote za Waislamu
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal:24]
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |