Jumapili, 23 Safar 1447 | 2025/08/17
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan: Mwaliko wa Kuhudhuria Mkutano na Waandishi wa Habari

Sisi, katika Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan, tuna furaha kuwaalika ndugu zetu katika vyombo vya habari, wanasiasa, na wale wenye hamu na mambo ya umma kuhudhuria kwenye mkutano na waandishi wa habari, ambapo msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan atatoa hotuba kwa anwani: "Wito kwa Watu wa Sudan: Ikamateni Darfur ili Isijiunge na Kusin"

Soma zaidi...

Mbwa Mwitu Hapaswi Kulaumiwa kwa Uvamizi wake ikiwa Mchungaji ndiye Adui wa Kondoo

Watoto watatu walifariki katika Jimbo la Khartoum baada ya kupokea dozi ya chanjo ya ukambi. Wizara ya Afya imefungua uchunguzi kuhusu dhurufu za vifo vyao. Sudan Tribune iligundua kuwa watoto wawili walikufa ndani ya saa moja baada ya kupokea chanjo ya ukambi, huku mtoto wa tatu akifa siku tisa baada ya kusaidiwa kupumua katika Hospitali ya Al-Balak mjini Omdurman. (Sudan Tribune, Agosti 5, 2025)

Soma zaidi...

Mahusiano ya Kigeni ni Jukumu la Dola Pekee, kwa kuwa Dola Pekee ndiyo iliyo na Haki ya Kuchunga Mambo ya Ummah Kivitendo

Baadhi ya vyombo vya habari viliripoti kuwa wajumbe kutoka Muungano wa Vyama na Mavuguvugu ya Sudan Mashariki, wakiongozwa na Sheiba Dirar na kuandamana na kundi la watu mashuhuri, walikutana na Rais wa Eritrea Isaias Afwerki mnamo Jumamosi, 2 Agosti 2025, afisini kwake huko Adi Halo, ambapo wajumbe hao walijadiliana naye hali ya sasa ya Sudan kwa jumla, kwa kuzingatia changamoto zinazoikabili Sudan Mashariki. Ujumbe huo pia ulisisitiza umuhimu wa uratibu na nchi jirani ili kusaidia utulivu wa nchi na kukabiliana na migogoro ya kisiasa na usalama.

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan Yaandaa Kisimamo Mbele ya Msikiti Mkongwe jijini Port Sudan cha Kuinusuru Gaza

Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan imeandaa kisimamo mbele ya Msikiti Mkongwe jijini Port Sudan leo, Ijumaa, 7 Safar 1447 H sawia na tarehe 1 Agosti 2025 M, baada ya swala ya Ijumaa. Wanachama wa Hizb waliinua mabango yenye alama ishara: “Angusheni viti vya utawala vinavyozuia kusonga kwa majeshi kuinusuru Gaza.”

Soma zaidi...

Hotuba Iliyotolewa na Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Sudan Mbele ya Msikiti Mkongwe jijini Port Sudan mnamo Ijumaa tarehe 1/8/2025 M

Je, hili linaweza kuwaziwa kutoka kwenu?! Vipi mnaweza kula, kunywa na kulala na hali ndugu zenu mjini Gaza wanauawa, wanahamishwa na kuwekwa njaa na Mayahudi wanaokalia kimabavu eneo la Isra ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)?! Dhambi liko juu ya shingo zetu sote ikiwa hatutawanusuru ndugu na dada zetu wa Gaza. Hatutaweza kuwanusuru isipokuwa majeshi ya Umma yasonge, kwani wao ni watoto wenu na ndugu zenu, na hakuna kitakachowaondoa Mayahudi isipokuwa dola ya Waislamu; Khilafah.

Soma zaidi...

Serikali ya Muungano Msingi ni Hatua ya Juu katika Kuharakisha Mpango wa Amerika wa Kutenganisha Darfur

Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), kupitia muungano wao unaoitwa Muungano Msingi wa Sudan "Ta'sis," ulitangaza mnamo Jumamosi, 26/7/2025, uteuzi wa Rais na Makamu wa Rais wa Baraza la Rais, na Waziri Mkuu, ambayo ina maanisha kuundwa kwa serikali sambamba katika mamlaka inayoendeshwa na jeshi kutoka mji wa Port Sudan, mashariki mwa nchi.

Soma zaidi...

Serikali ya “Matumaini” Yageuka Jinamizi kwa Wananchi kwa Kuporomoka kwa Pauni ya Sudan!

Katika hotuba yake baada ya kula kiapo cha kuwa Waziri Mkuu, Kamil Idris alisema: “Kauli mbiu yetu ni matumaini, na dhamira yetu ni kufikia usalama, ustawi, na maisha ya utulivu kwa kila raia wa Sudan!” Katika taarifa yake ya kwanza kwa vyombo vya habari, alitangaza kuwa atatoa muda na juhudi zake kuhakikisha maisha ya heshima kwa kila Msudan.

Soma zaidi...

Mwaliko wa Kuhudhuria Kikao cha Kisiasa

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan inafuraha kuwaalika wanahabari, wanasiasa, na wote walio na hamu na masuala ya Umma kuhudhuria na kushiriki katika kikao kipya cha kisiasa, ambacho kitamwalika Ustadh Muhammad Jami' (Abu Ayman), Msaidizi wa Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan.

Soma zaidi...

Taarifa ya Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Sudan katika Mkutano na Waandishi wa Habari Uliofanyika Jumamosi, 19/07/2025, jijini Port Sudan “Hakuna Serikali Inayoleta Matumaini Isipokuwa chini ya Uislamu na Dola yake ya Khilafah”

Mnamo Jumatatu, 19/05/2025, Mwenyekiti wa Baraza la Utawala, Abdel Fattah Al-Burhan, alitoa uamuzi wa kumteua afisa wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kamal Idris kuwa Waziri Mkuu kuunda serikali ya kitaalamu. Siku hiyo hiyo, Al-Burhan pia alitoa uamuzi wa kufutilia mbali agizo la hapo awali lililowapa wanachama wa Baraza Kuu usimamizi wa wizara na vitengo vya serikali ya kifederali.

Soma zaidi...

Mwaliko wa Kuhudhuria Mkutano na Waandishi Habari

Kwa ndugu na dada zetu waheshimiwa katika vyombo vya habari, ikiwa ni pamoja na magazeti, redio, na runinga, sisi, katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, tuna furaha kukualikeni kuhudhuria mkutano na waandishi wa habari wenye kichwa: Hakuna Serikali inayoweza Kutoa Matumaini Isipokuwa chini ya Uislamu na Dola yake ya Khilafah.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu