Jumapili, 23 Safar 1447 | 2025/08/17
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

“Siku ya Uhuru” ya 78 Pakistan Itakuwa Huru Kupitia Kuanzishwa kwa Khilafah Rashida

Chini ya mfumo wa sasa wa kimataifa, kile kinachoitwa uhuru si kitu zaidi ya usanii wa mchezo wa kuigiza, kwan maana ukombozi wa kweli (tahrir) uko pale tu dola inapoweza kupanga mambo yake ya ndani na mahusiano ya nje kwa mujibu wa itikadi yake. Watu wanaoamini “La ilaha illa Allah Muhammadur RasulAllah” kamwe hawatakombolewa kikweli mpaka watabikishe katika ardhi yao mfumo wa Kiislamu wa utawala, uchumi, jamii, elimu, na mahakama, pamoja na sera ya kigeni yenye msingi wa Da‘wah na Jihad. Hii ndiyo maana halisi ya uhuru, na katika suala hili, Pakistan bado haijakombolewa!

Soma zaidi...

Kashmir Haiwezi Kukombolewa Bila Kubadilisha Uongozi Unaopoteza Fursa ya Dhahabu ya Kuikomboa Kashmir, kwa ajili ya Kumfurahisha Trump

Leo, tarehe 5 Agosti 2025, miaka sita imepita tangu kuunganishwa kwa lazima kwa Kashmir Inayokaliwa kimabavu na Raja Dahir wa zama hizi, Modi. Kulingana na makubaliano yaliyofikiwa nchini Marekani, kuisalimisha Kashmir ilikuwa ni usaliti wa wazi wa uongozi wa kisiasa na kijeshi wa Pakistan wa wakati huo, serikali ya Bajwa-Imran. Miezi michache tu baadaye, Jenerali Bajwa aliendeleza usaliti huu kwa kutia saini makubaliano ya kusitisha mapigano, na Dola ya Kibaniani kuhusiana na Kashmir. Hata hivyo, usaliti huu dhidi ya Waislamu wanaodhulumiwa na wanyonge wa Kashmir uliendelea hata zaidi ya hapo.

Soma zaidi...

Njia ya Kujiondolea Dhambi ya Kuwatelekeza Waislamu wa Palestina, ni Kujitahidi Mchana na Usiku Kusimamisha Khilafah Rashida, na Kukusanya Majeshi

Kwa vile majeshi ya Waislamu hayakusonga kuinusuru Gaza, baba mwengine aliyedhulumiwa, Abu Umar, aliuawa shahidi, alipokuwa akiwatafutia watoto wake chakula. Alipokuwa akingoja kupokea msaada, risasi ya mdunguaji Myahudi muoga ilipenya kichwa chake. Yule rafiki aliyeuleta mwili wake alikuwa na njaa kwa siku tano, na akarudi kutoka kwenye kizingiti cha mlango wa shahada, labda kuuawa shahidi hivi karibuni. Hili sio tukio moja pekee. Makumi ya matukio kama haya yanashuhudiwa moja kwa moja kila siku, na Umma wa bilioni mbili.

Soma zaidi...

Usaliti wa Watawala wa Pakistan na Kukumbatia Kwao Uhalalishaji wa Mahusiano: Utangulizi wa Kujiunga na Mkataba wa Khiyana wa Abraham na Kutumikia Maslahi ya Amerika ya Trump na Umbile la Kiyahudi

Marekani ya Trump sasa inajitahidi kuunda "Mashariki ya Kati Mpya," ambayo inatumikia maslahi ya Marekani katika kanda hiyo, shauku kuu ikiwa ni kuhakikisha amani, usalama, na upanuzi wa kambi ya kijeshi ya Amerika katika Ulimwengu wa Kiislamu, inayojumuishwa ndani umbile la Kiyahudi. Inatafuta kuliweka umbile la Kiyahudi kama mamlaka kuu katika eneo hilo kisiasa, kiuchumi, na kimfumo. Licha ya haya yote, vibaraka wa Amerika ya Trump wamekimbilia kutekeleza mradi huu, na kutumikia maslahi ya bwana wao.

Soma zaidi...

Kati ya Usaliti wa Palestina na Kashmir na Utumwa kwa Amerika Asim Munir Anafanya Nini Mbele ya Firauni Wa Zama Zetu, Trump?

Katika wakati ambapo Amerika inapigana vita dhidi ya jirani Muislamu, Iran, kwa kutumia mkono wake mchafu katika eneo hilo, umbile la Kiyahudi, Rais wa Marekani, Donald Trump, alimkaribisha Mkuu wa Majeshi wa Pakistan mnamo Jumatano, 18 Juni 2025, kwa chakula cha mchana katika mkutano ambao haujawahi kushuhudiwa katika Ikulu ya White House. Kinachotia shaka kuhusu mkutano huu, na muda wake, ni kwamba ni mara ya kwanza kwa rais wa Marekani kumkaribisha mkuu wa jeshi la Pakistan katika Ikulu ya White House, bila ya kuwepo kwa afisa yeyote mkuu wa kiraia wa Pakistan, kuashiria umuhimu wa mkutano huo, na unyeti wa mada yake.

Soma zaidi...

Katikati ya Tabasamu za Idd na Machozi ya Gaza: Wito kwa Maafisa na Wanajeshi

Huku Waislamu wakijiandaa kukaribisha Idd al-Adha na kusherehekea pamoja na watoto wao na wenza wao katika siku hizi za sherehe, tunaelekeza ujumbe huu makhsusi kwa wanajeshi na maafisa wanyoofu wa jeshi la nyuklia la Pakistan, na majeshi mengine ya Ummah kwa jumla. Tunawakumbusha katika siku hizi kwamba wamewatelekeza watu wao wenyewe, wanawake, watoto, wazee, na wanaume katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina na Gaza, na hawakujitokeza kuwanusuru licha ya kuwa na uwezo wa kufanya hivyo.

Soma zaidi...

Farauni wa Washington Afanya Maangamizu Makubwa Gaza, Kwa Usaidizi Kamili wa Viongozi wa Kijeshi na Kisiasa wa Waislamu na Mayahudi. Jibu Pekee la Kisharia ni Uhamasishaji wa Majeshi ya Waislamu. Enyi Waislamu! Songeni kwa ajili ya Faradhi ya Kishar

Bila jeshi hata moja la Waislamu kumzuia, Trump alitimiza ahadi yake ya kufanya maangamizi makubwa Gaza. Kamera zimenasa picha za sehemu za miili ya waumini zikipaa angani, juu ya majengo marefu, kutokana na kukithiri kwa mashambulizi ya makombora. Madaktari wa uokoaji wanafunikwa macho na kupigwa risasi. Watoto, wanawake, wazee na waliojeruhiwa wanauawa shahidi kwa kulipuliwa mahema yao. Sera ya njaa ya Amerika, iliyotekelezwa na wafuasi wake, umbile la Kiyahudi, imeongeza mateso hadi kiwango cha baa la njaa. Sasa imedhihirika kwa kila mtu kwamba Firauni wa Washington anafanya maangamizi makubwa kwa Gaza, kwa usaidizi kamili wa kijeshi na uongozi wa kisiasa wa Waislamu na Mayahudi.

Soma zaidi...

Watawala Vibaraka Wamefichua Udanganyifu wa Ubwana wa Kitaifa na Maslahi ya Kitaifa. Ni Hoja Gani iliyopo ya Kuzuia Kukomeshwa kwa Mfumo wa uliopo Sasa?

Mnamo tarehe 11 Februari 2025, taarifa kwa vyombo vya habari ilitolewa kwenye tovuti ya Mahakama ya Upeo ya Pakistan, ambayo ilifichua mabaki ya udanganyifu wa ubwana wa kitaifa. Taarifa hiyo kwa vyombo vya habari ilisema kuwa Jaji Mkuu na maafisa wengine wa mahakama walikutana na ujumbe wa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) na kuwaeleza kuhusu masuala ya Mahakama ya Upeo. Katika taarifa hiyo, Jaji Mkuu alithibitisha kuwa Mahakama ya Upeo inakamilisha ajenda ya kikao cha Kamati ya Kitaifa ya Mahakama ya Utungaji Sera (NJPMC) katika wiki ya mwisho ya Februari. Hata aliwaalika wajumbe wa wakoloni pia kutoa mapendekezo yao katika suala hili.

Soma zaidi...

Enyi Majeshi! Chagueni kati ya Watawala hawa ambao ni Watiifu kwa Trump, na Khalifa Rashid ambaye ataikomboa Gaza na Palestina nzima kupitia Nguvu za Kijeshi!

Mnamo Jumanne 4 Februari 2025, akiwa ameketi ubavuni mwa muuaji wa Gaza, Benjamin Netanyahu, Rais Trump wa Marekani alitangaza, "Marekani itauchukua Ukanda wa Gaza, na tutafanya kazi nayo pia." Tamko la kiburi la Trump kuhusu Gaza ni kofi kwenye uso wa watawala wa Waislamu, ambao wametekeleza kwa utiifu amri ya Marekani, na kuzuia vikosi vya majeshi ya Waislamu kupigana na umbile la Kiyahudi, na hivyo kuruhusu mauaji ya Waislamu nchini Palestina. Watawala wa sasa wa Waislamu, kama wale waliotangulia, wanajifunza kwamba Marekani haiwajali wao, au viti vyao vya khiyana. Marekani itaendelea kuwadhalilisha na kuwashusha hadhi mbele ya dunia na watu wao wenyewe. Kwa hakika, kushiriki katika mfumo wa dunia unaoongozwa na Marekani, na kushikamana na sheria za kimataifa na taasisi za kimataifa, si chochote ila unyenyekevu na utiifu kwa Marekani na rais wake. Hata hivyo watawala hawa hawajali. Hata hivi sasa wanakimbilia kumfurahisha na kumtuliza bwana wao, Amerika, wakijaribu kuwasilisha kwake "mpango wa amani wa Waarabu" wao wenyewe.

Soma zaidi...

Kuanguka kwa Khilafah Kunaashiria Wito wa Kuhuishwa Kwake

Mnamo tarehe 3 Machi 1924, sawia na 28 Rajab 1342 H, kikundi kidogo cha wasaliti wa Kituruki, wakiongozwa na Mustafa Kemal, walivunja urithi wa zaidi ya karne 13 za umoja wa Waislamu. Kuanzia wakati huo na kuendelea, Waislamu walipoteza paa lao juu ya vichwa vyao na wakawa mayatima. Leo, miaka 104 ya hijria imepita tangu tukio hili la kusikitisha. Baada ya kuanguka kwa Khilafah, makafiri waligawanya ulimwengu wa Kiislamu katika maeneo madogo yaliyojitenga. Waliweka vikwazo vya usafiri kati ya maeneo haya, yakihitaji pasipoti na visa, na kuharibu majeshi yetu, silaha, rasilimali, ardhi, uwezo wa binadamu, na teknolojia-kila kitu.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu