Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi: Ustadh Hassan Nouair
- Imepeperushwa katika Tunisia
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Tunisia inaomboleza kifo cha mmoja wa watu wake miongoni mwa Wabebaji Da’wah, Ustadh Hassan Nouair, aliyefariki dunia leo, Ijumaa, tarehe 24 Dhu al-Hijjah 1446 H, sawia na 20/06/2025 M, baada ya mapambano na maradhi ambayo yalidhoofisha mwili wake lakini hayakuzima moto wa ujumbe wake wala azma yake ya kufanya kazi katika safu za wale wanaojitahidi kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kwa kusimamisha Khilfah Rashida kwa njia ya Utume.