Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
H. 27 Dhu al-Hijjah 1447 | Na: 1446/16 |
M. Jumatatu, 23 Juni 2025 |
Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi
Ndugu Basheer Qassila
[مِنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُمْ مَنْ قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُمْ مَنْ يَنْتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً]
“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab 33:23]
(Imetafsiriwa)
Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Tunisia inaomboleza mmoja wa watu wake waliojitolea na wabebaji wa da'wah: mzee na kaka, simba wa da'wah, Basheer Qassila, ambaye alifariki mnamo Jumapili, tarehe 26 Dhul-Hijjah 1446 H, sawia na 22 Juni 2025 M, baada ya kupambana na maradhi yaliyomdhoofisha mwili wake lakini katu hayakuzima moto wa ujumbe wake wala azma yake ya kufanya kazi pamoja na safu akijitahidi kurudisha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.
Katika safari yake yote, alivumilia giza la magereza na ugumu wa maisha, lakini alibaki imara.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amkubali miongoni mwa watu wema, aipandishe daraja yake juu juu kabisa, na awape subira, nguvu na faraja familia yake, wapenzi wake na maswahaba zake.
[إِنَّا لِلّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]
“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqarah: 156]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Tunisia |
Address & Website Tel: 71345949 / 21430700 http://www.ht-tunisia.info/ar/ |
Fax: 71345950 E-Mail: tunis@htmedia.info |