Tarehe 5 Agosti 2024 ni Siku ya Uasi wa Watu dhidi ya Dhalimu na Utawala wa Kidhalimu, ambao ungali Unaendelea; kinachojulikana kama 'Tangazo la Julai' ni Hati ya Usaliti wa Vyama vya Kisiasa vinavyounga mkono Marekani ili kuangamiza Uasi wa Watu
- Imepeperushwa katika Bangladesh
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Wananchi wakiwa wamekata tamaa sana, wamepita mwaka mmoja tangu kuanguka kwa Hasina katika uasi mkubwa dhidi ya dhalimu Hasina na utawala dhalimu mnamo Agosti 5, 2025. Kwa sababu baada ya kuanguka kwa dhalimu Hasina, vibaraka wa Marekani na vyama vya kisiasa vyenye uchu wa madaraka vimechukua mshiko wa kubainisha hatima ya watu na kuweka vikwazo katika kutekeleza matumaini na matarajio ya watu na wameendelea na majaribio yao maovu na kuteka nyara uasi huo. Kinachojulikana kama 'Tangazo la Julai' ni hatua isiyo na aibu ya jaribio hili ovu. Watu wamekataa utumwa wa Marekani na sarakasi za kisiasa kwa chuki. Yaliyo mbali na kuakisi matarajio ya watu, Tangazo hili la Julai halitambui hata matukio kama vile njama ya India huko Pilkhana na mauaji ya halaiki ya watu wanaopenda Uislamu huko Shapla Chattar.