Kukipokonya Silaha Chama cha Iran na Dori ya Mamlaka ya Lebanon!
- Imepeperushwa katika Lebanon
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Makubaliano ya kusitisha mapigano ya tarehe 27/11/2024, kati ya umbile la Kiyahudi na mamlaka za Lebanon, chini ya usimamizi wa moja kwa moja wa Marekani, yaliweka msingi wa kisiasa wa kukipokonya silaha chama cha Iran na mirengo mengine ya Palestina nchini Lebanon. Hii haikuwa kutokana na kutaka "amani" kutoka Marekani, bali ni kuhakikisha usalama wa umbile la Kiyahudi katika maandalizi ya kuondoa uwezo mdogo uliobaki wa Waislamu wa kupigana nao, hasa baada ya matukio ya Kimbunga cha Al-Aqsa.