Gaza Inavuna Mavuno Uchungu ya Baraza la Usalama na Uamuzi wa Baraza la Amani
- Imepeperushwa katika Palestina
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Siku chache baada ya uamuzi wa Baraza la Usalama, watu wa Gaza walianza kuvuna hasara yake; katika muda usiozidi masaa 24, mashahidi 34—wengi wao wakiwa watoto na wanawake—walikuwa wamepanda daraja hiyo hadi kufikia Alhamisi asubuhi, 20/11/2025, pamoja na makumi ya waliojeruhiwa kutokana na uzito wa njaa na kwenye makucha ya baridi kali. Damu hizi safi zilikuwa maana halisi ya uamuzi ulioipa Amerika usimamizi na mamlaka juu ya Ukanda wa Gaza, ikiruhusu kukata vichwa kama ilivyotaka. Ni uamuzi uliopuuza damu, utajiri, na ardhi za watu wa Palestina katika Ukingo wa Magharibi na kuachilia mkono wa Mayahudi kutumbukia ndani ya damu yetu, ambayo ilienea zaidi ya Gaza hadi Kambi ya Ain al-Hilweh nchini Lebanon.



