Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
| H. 28 Dhu al-Hijjah 1447 | Na: H 1447 / 091 |
| M. Jumapili, 14 Juni 2026 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Je, Erdogan Anasubiri Mayahudi Waipige Mabomu Ankara Kabla ya Kuhamasisha Jeshi Lake?!
(Imetafsiriwa)
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan, katika hotuba aliyotoa wakati wa mkutano wa kundi la wabunge wa Chama cha Haki na Maendeleo katika Bunge la Uturuki, alisema: "Tunafahamu vyema lengo kuu la udanganyifu wa 'Ardhi iliyo Ahidiwa', na Mungu akipenda, hatutaruhusu kamwe." Alifafanua kwamba usalama wa Uturuki hauanzii katika mkoa wa Hatay kusini mwa Uturuki, bali Aleppo, Damascus, na Beirut. Aliendelea: "Ikiwa uonevu wa Israel hautasimamishwa, gharama haitalipwa na eneo hilo pekee, bali na wanadamu wote." Erdoğan alizisihi dola kuu duniani kuchukua msimamo wazi dhidi ya umbile hilo la Kizayuni, akisema: "Kuirudisha Israel katika kufuata sheria sio tena jukumu la baadhi ya nchi tu, bali ni jukumu la pamoja linalowaangukia wanadamu wote."
Erdogan anazungumzia umbile la Kizayuni, akilielezea katika hotuba hiyo hiyo kama umbile dogo, lakini wakati huo huo anadai kwamba kulidhibiti na kukabiliana nalo kunahitaji nguvu za kimataifa na wanadamu wote! Huku akiangalia shughuli za umbile la Kizayuni katika eneo hilo na akifahamu matarajio yake ya upanuzi na ya kibiblia, anaangalia na kulaani tu bila kuchukua hatua yoyote! Na licha ya kuzingatia usalama wa Aleppo, Damascus, na Beirut kama usalama wa Ankara, na licha ya kushuhudia jinsi Wazayuni walivyoshambulia Beirut, Damascus, Aleppo, na miji mengine, pia amebaki kimya!
Na kwa hakika, hii inatukumbusha kauli zilizotolewa na viongozi wa Iran kwa miaka mingi, wakizungumzia kulifuta umbile la Kizayuni kutoka kwenye ramani na kukomesha uwepo wake ndani ya dakika nane ikiwa lingeshambulia Iran. Waliendelea kusubiri, kutazama, na kutishia hadi umbile la Kizayuni liliposubutu kushambulia, kuua, kuharibu, na kuanzisha shambulizi kali dhidi ya Iran.
Je, Erdoğan anasubiri nchi yake ipate hatima hiyo hiyo kama Iran kabla ya kuihami? Je, haoni na kusikia njama za Kiyahudi na vitisho vyao vya mara kwa mara vya kuvamia eneo hilo na kushambulia Uturuki na Misri baada ya Iran? Au anajiona kuwa mwerevu na mjanja zaidi kuliko wale waliopata matokeo ya kumtegemea mkoloni kafiri na usaliti wao kwa ummah na nchi yao?
Umbile la Kiyahudi ni umbile lenye saratani linaloamini tu katika mantiki ya nguvu, haliweki ahadi au makubaliano, na matarajio yake huko Mesopotamia na uundaji upya wa Mashariki ya Kati yanatangazwa na kuonekana, kwa hivyo vitisho havifanyi kazi kwake bila ya viwanja vya vita.
Zaidi ya hayo, masuala ya Ummah wa Kiislamu hayawezi kugawanywa, wala hayawezi kutazamwa kupitia lenzi ya utaifa au uzalendo. Ummah wa Kiislamu ni Ummah mmoja; vita vyake ni vimoja, na amani yake ni moja. Kinachoipata Gaza au Jerusalem kinaipata Damascus, Ankara, Cairo, na Islamabad. Kanuni msingi ni kwamba majeshi ya Uturuki, Misri, Syria, na majeshi yote ya Waislamu yanapaswa kuhamasika kunusuru ardhi yoyote ya Kiislamu, popote pale ilipo. Kwa mtawala yeyote kusubiri hadi Mayahudi wabishe mlangoni kwake na kuangusha kiti chake cha enzi ni upumbavu mtupu.
Inatosha kwa maneno na hotuba tupu, Erdogan! Kama wewe ni mkweli, hamasisha jeshi lako kuling'oa umbile la Kizayuni na kuuondolea Ummah maovu yake. Vyenginevyo, waachie viongozi na waanzilishi wenye ikhlasi wazungumze neno lao na kutangaza Khilafah Rashida kwa njia ya utume, ili kuendeleza njia ya Makhalifa waongofu wa Waislamu na kuiregesha kama Khilafah ya izza, tamkini, na ukombozi.
[لِلَّهِ الْأَمْرُ مِن قَبْلُ وَمِن بَعْدُ وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنصُرُ مَن يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]
“Amri ni ya Mwenyezi Mungu kabla yake na baada yake. Na siku hiyo Waumini watafurahi * Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum 30:4-5]
Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.muslimworld.today |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) muslimworld.today |



