Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
| H. 16 Dhu al-Hijjah 1447 | Na: HTS 1447 / 124 |
| M. Jumamosi, 06 Juni 2026 |
Mwaliko wa Kuhudhuria na Kushiriki katika Kikao cha Kadhia za Umma
(Imetafsiriwa)
Tunafuraha, kama Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, kuwaalika wanahabari, wanasiasa, na wote walio na hamu na masuala ya umma kuhudhuria na kushiriki katika Kikao cha kila mwezi cha Kadhia za Umma, ambacho mwezi huu kitafanyika katika afisi ya Hizb jijini Khartoum baada ya kukatizwa kwa muda mrefu kwa zaidi ya miaka mitatu kutokana na vita.
Kikao cha mwezi huu kitakuwa na kichwa:
Mizizi ya Usekula katika Siasa za Sudan na Namna ya Kuing’oa
Wazungumzaji katika kikao watakuwa:
1. Dkt. Ahmed Abdel Fadil – Mwanachama wa Hizb ut Tahrir
2. Ustadh Abdullah Hussein – Mwanachama wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan
Mwendeshaji: Ustadh Munzir Abdul Raouf – Mwanachama wa Hizb ut Tahrir
Tarehe: Jumamosi, 20 Dhu al-Hijjah 1447 H, sawia na 06/06/2026 M
Wakati: 11:00 a.m.
Mahali: Afisi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, Khartoum Mashariki, magharibu mwa makutano ya barabara ya Al-Mak Nimir na barabara ya 21 Oktoba.
Kuhudhuria kwenu ni heshima kwetu na kunaakisi hamu yenu kwa kadhia za Umma wenu.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |



