Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
| H. 7 Dhu al-Hijjah 1447 | Na: H 1447 / 083 |
| M. Jumapili, 24 Mei 2026 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Je, Sio Wakati wa Ummah Kuwekeza Utajiri Wake Katika Kujenga Maslahi na Nguvu Zake Wenyewe?
(Imetafsiriwa)
Utajiri na rasilimali za Ummah zinaendelea kufujwa ili kutajirisha Magharibi, huku ndani ya nchi, zikitumika kwa anasa zinazowaweka Waislamu mbali na mfumo wa maisha wa Kiislamu. Mnamo Alhamisi, 21/5/2026, Mamlaka Kuu ya Burudani ya Saudi Arabia ilitangaza muungano mpya wa Saudi Arabia na Misri unaolenga kujenga mfumo jumuishi wa matukio makubwa katika eneo hilo, unaounganisha nchi hizo mbili kwenye njia moja ya kuvutia wasanii na nyota wa kimataifa! Wakati huo huo, mnamo Jumatano, 20/5/2026, nchi za Baraza la Ushirikiano la Ghuba (GCC) na Uingereza zilitangaza makubaliano ya kihistoria na makubwa ya biashara huria yenye thamani ya takriban dolari bilioni 5, na kuifanya Uingereza kuwa taifa la kwanza la G7 kusaini makubaliano kama hayo na kambi ya Ghuba.
Hivyo, watawala wa Waislamu wanaendelea kufuja utajiri wa Ummah wa Kiislamu. Jana tu, tuliwashuhudia wakihitimisha mikataba yenye thamani ya mamia ya mabilioni ya kununua bidhaa kutoka kwa makampuni ya Magharibi kwa bei zinazozidi thamani ya soko la makampuni hayo. Pia tuliona wakitumia fedha za utajiri huru kuzinusuru kampuni za Magharibi zilizo karibu kufilisika. Mikataba hii na mengine haina maana nyengine isipokuwa kuingiza pesa za Ummah katika uchumi wa Magharibi, ambao sasa umekumbwa na hofu ya kuporomoka kusikotarajiwa—mporomoko ambao unaweza kuwa na madhara makubwa zaidi kuliko ya awali.
Njia sahihi ya kuchukua hatua ingekuwa ni kutumia fedha hizi katika kukuza uwezo wa kiuchumi na kijeshi wa nchi za Waislamu, ili ziweze kujitegemea katika teknolojia inayodhibitiwa na Magharibi, na kuunda fursa za kazi ambazo zingezuia “uhamaji wa wataalamu” unaoendelea—jambo linalosukumwa na ugumu wa kiuchumi, kuzuiwa kwa maisha ya umma, na kutengwa kutoka nyanja ya kisiasa.
Hapa tunarudia swali: Je, sio wakati sasa wa Ummah wa Kiislamu kuwekeza utajiri wake katika kujenga maslahi na nguvu zake wenyewe?
Hakika, kwa jina la Mwenyezi Mungu wakati umewadia, na tunaamini uko karibu, Mwenyezi Mungu akipenda. Haijalishi Magharibi na vibaraka wake wanajaribu kiasi gani kuvuruga Ummah kwa sera za kutoa nguvu, kuzielekeza kwenye burudani na kueneza mambo yasiyo na maana. Hata hivyo, Uislamu, pamoja na wema wake, hadhi, na historia yake tukufu, unaishi ndani kabisa ya Ummah. Mwenyezi Mungu (swt) asema [وَاللَّهُ مُتِمُّ نُورِهِ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ] “Na Mwenyezi Mungu atakamilisha nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia.” [As-Saf: 8].
Mhandisi Salah Eddine Adadah
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.muslimworld.today |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) muslimworld.today |



