Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
| H. 27 Jumada II 1447 | Na: 18 / 1447 |
| M. Alhamisi, 18 Disemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Wakati Dola ya Kibaniani Inapozivua Niqab Kwenye Nyuso za Mabinti wa Kiislamu, Warithi wa Muhammad Bin Qasim Wako Wapi Ndani ya Jeshi la Pakistan?
(Imetafsiriwa)
Mnamo Jumatatu, 15 Disemba 2025, katika sherehe moja, Waziri Mkuu wa jimbo la India la Bihar, Nitish Kumar, aliichana niqab kutoka kwa daktari mmoja Muislamu, Nusrat Parveen. Baada ya kufanya hivyo, alicheka kana kwamba kuichana niqab hiyo kutoka kwa uso wa mwanamke wa Kiislamu ilikuwa ni mzaha. Ilhali, Mayahudi walipomfunua mwanamke mmoja wa Kiislamu na kumdhihaki hali yake, Swahaba aliyekuwepo alimuua Myahudi huyo; na Mayahudi walipomuua shahidi Swahaba huyo baadaye, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alizingira kabila lote, akawakamata na kuwafunga wote, na alikuwa akitoa hukumu juu yao, lakini hatimaye, baada ya maombezi, adhabu ndogo ilitolewa: kabila lote lilifukuzwa Madina. Lakini leo hakuna dola ya kulinda heshima ya Dkt. Nusrat Parveen na kumpa Baniani huyu muovu, Nitish Kumar, funzo.
Watawala wetu, baada ya kuisukuma jihad nyuma, wameweka mzigo wote wa ukiukaji wa heshima na utakatifu kwenye kauli tupu, ya kawaida: “Tunalaani!” Hata kama kulaani huko kutawafikia maelfu, hakuna hata unywele mmoja unaotikisika kwenye dola ya Kibaniani kwa sababu yake. Laana zina athari tu wakati adui anajua kwamba kuendelea baada ya laana kutasababisha hatua za kisiasa, kiuchumi, na kijeshi. Lakini watawala wetu, baada ya kuisalimisha Kashmir—mshipa wa uhai wa Pakistan—pia wamesalimisha mito mitatu, na wameipa dola ya Kibaniani iliyo kwenye Mstari wa Udhibiti amri ya kusitisha mapigano. Kwa nini dola ya kuchukiza ya Kibaniani isisubutu kucheza na heshima ya Waislamu?
Hili sio tukio la kwanza kufanywa na dola ya Kibaniani. Nchini India, siku baada ya siku, chini ya sera kali ya Hindutva, matukio yanatokea kama vile kubomolewa kwa nyumba za Waislamu; mauaji na vurugu kwa jina la kukamata nyama ya ng'ombe; marufuku dhidi ya niqab; kubomolewa kwa misikiti; kunyimwa uraia na kubatilishwa kwa uraia; kufungwa kwa biashara; kunyakua mali za waqf; na unyanyasaji wa mabinti wa Kiislamu. Kwa kifupi, katika ngazi ya serikali na jimbo, ajenda ya kimpangilio ya Hindutva inawalenga Waislamu.
Baniani Baniya ametiwa ujasiri wa kufanya haya yote na watawala wa Pakistan wenyewe, huku, kuanzia mwaka wa 2002 wakati wa enzi ya Musharraf, msako mkali ulianza kwenye kambi za jihad za Kashmir chini ya amri ya Marekani. Jihad ya Kashmir ilikubaliwa kama ugaidi. Utiifu ulifanywa mbele ya mpango wa Marekani wa kuifanya dola ya Kibaniani kuwa polisi wa kikanda. Ima iwe ni Aman ki Asha au uhuru wa biashara, mchakato huu umeendelea tangu wakati huo hadi leo. Kama mwanajeshi mkuu wa Pakistan angeweka mkono wake juu ya vichwa vya mabinti wa Kiislamu katika dola ya Kibaniani na kuwaona kama mabinti zake mwenyewe, dola ya Kibaniani isingesubutu hata kuwagusa binti zetu, sembuse kuwaangalia kwa jicho ovu. Lakini ole wao, hawakupata hata uwezo wa kulaani.
Katika hatua hii, hadith ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) inatekelezeka kikamilifu:
«إِذَا تَبَايَعْتُمْ بِالْعِينَةِ، وَأَخَذْتُمْ أَذْنَابَ الْبَقَرِ، وَرَضِيتُمْ بِالزَّرْعِ، وَتَرَكْتُمُ الْجِهَادَ، سَلَّطَ اللَّهُ عَلَيْكُمْ ذُلًّا، لَا يَنْزِعُهُ حَتَّى تَرْجِعُوا إِلَى دِينِكُمْ»
“Mnapofanya miamala ya ‘inah (ya riba), na mkakamata mikia ya ng'ombe, mukaridhika na kilimo, na kuachana na jihad, Mwenyezi Mungu atakusalitini kwa udhalilifu; hataiondoa kwenu hadi mtakaporudi kwenye dini yenu.” (Sunan Abu Dawud, Musnad Ahmad)
Enyi Maafisa wa Vikosi vya Jeshi la Pakistan!
Iwe ni operesheni ya Swift Retort ya 27 Februari 2019 au Bunyan al-Marsus ya Mei 2025, ni wazi kwenu kama mwanga wa mchana kwamba mnaweza kulazimisha dola ya Kibaniani kusugua pua yake kwenye vumbi. Lakini udhaifu wenu ni kwamba uongozi wenu hutatua mambo na dola ya Kibaniani kwa kiwango ambacho Amerika inaruhusu pekee. Hata katika Operesheni ya Bunyan al-Marsus mnamo Mei 2025, waliweka sifa ya mafanikio yenu kwenye mapaja ya Rais Trump, na mbele ya Trump wanainama kwa namna hiyo—huku wakikuzuieni kuifundisha dola ya Kibaniani funzo zaidi, kuikomboa Kashmir, na kurudisha mito mitatu kupitia kusitisha mapigano—kana kwamba haikuwa baniani baniya aliyepigwa, bali sisi.
Uongozi huu umefunga fikra zake na uwezo wenu ndani ya mipaka iliyochorwa na Waingereza, ingawa msimamo mzima wa Amerika umefichuliwa wazi mbele yenu nchini Afghanistan, Iraq, na Gaza. Mnaweza kuwalinda mabinti wa Umma huu pale tu mtakapojikomboa kutokana na uongozi huu uliofungwa minyororo na ushawishi wa Marekani.
Mambo haya hayawezi kuendelea kwa njia ambayo kila mmoja wa viongozi wenu, anafuata maagizo ya Marekani, anabaki anashughulika sana katika kuunga mkono dola ya Kibaniani na Mayahudi; kwamba mpiganaji wa kimsalaba Trump anaendelea kuimba rozari ya jemadari wa jeshi; kwamba “kimsingi” yuko tayari kukutumeni kwa ajili ya ulinzi wa Mayahudi; kwamba kila aina ya kupitiliza kunakofanywa na dola ya Kibaniani kunakabiliwa tu kwa subira, kujizuia, na uvumilivu—huku mkisimama tu na kutazama mandhari hiyo.
Dada zenu wanakuiteni. Serah ya Mtume (saw) iko mbele yenu. Katika historia yote, Waislamu wamekusanya majeshi kwa wito wa dada mmoja tu—iwe ni Muhammad bin Qasim aliyekwenda katika nchi ya India kuwalinda dada zake, au Khalifa Harun al-Rashid akijibu kilio cha “Wa Mu‘tasimah.” Lakini sasa uongozi wa majeshi ya Waislamu uko mikononi mwa watu wasiojali hisia ambao hawasikii kilio cha kina dada wala hawaguswi na miili ya Waislamu waliokufa.
Kwa hivyo je mtawaacha mabinti wa Ummah kwenye huruma ya baniani baniya hadi lini? Uondoeni uongozi huu, na muipe nusrah Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamishwa Khilafah, ili mupate heshima kubwa ya kuwa mlinzi wa mbele wa Ghazwah-e-Hind, ambayo Abu Hurairah (ra) alisema kuihusu:
«وَعَدَنَا رَسُولُ اللَّهِ ﷺ غَزْوَةَ الْهِنْدِ، فَإِنْ أَدْرَكْتُهَا أُنْفِقْ فِيهَا نَفْسِي وَمَالِي، وَإِنْ قُتِلْتُ كُنْتُ مِنْ أَفْضَلِ الشُّهَدَاءِ، وَإِنْ رَجَعْتُ فَأَنَا أَبُو هُرَيْرَةَ الْمُحَرَّرُ»
“Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ alituahidi vita vya Hind. Iwapo nitavipata, nitatoa nafsi yangu na mali yangu humo. Nikiuawa, nitakuwa miongoni mwa mashahidi bora; na nikirudi, basi nitakuwa Abu Hurairah, aliye huru (kutokana na dhambi).” (Al-Mustadrak ‘ala al-Sahihayn)
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Pakistan |
Address & Website Tel: +(92)333-561-3813 http://www.hizb-pakistan.com/ |
Fax: +(92)21-520-6479 E-Mail: htmediapak@gmail.com |



