Mashambulizi ya "Warefu Tisa" yatamalizwa tu kwa Utekelezaji wa Adhabu za Sharia chini ya Dola ya Khilafah
- Imepeperushwa katika Sudan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Habiba Al-Amin, mwandishi wa habari wa tovuti ya Kush News, alishambuliwa vikali na wanachama wa genge la "Warefu Tisa" katika eneo la kivuko kwenda Port Sudan alipokuwa akiregea kutoka kwenye uangaziaji wa habari akiwa na wenzake kadhaa. Hili ni moja tu ya matukio mengi ya uporaji, ujambazi na mauaji katika miji inayodaiwa kuwa salama, kama vile Omdurman, Khartoum, na sasa mji mkuu wa utawala, Port Sudan. Hii ni miji iliyo chini ya udhibiti wa serikali na vyombo vyake vya usalama.