Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
| H. 12 Jumada II 1447 | Na: HTS 1447 / 63 |
| M. Jumatano, 03 Disemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Wamzuru Katibu Mkuu wa Chama cha Wanasheria katika Jimbo la Al-Jazirah
(Imetafsiriwa)
Mnamo Jumanne, 2 Disemba 2025, ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, ukiongozwa na Mhandisi Mahdi Muhajir, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, na akifuatana na Ustadh Omar Ibrahim, pia mwanachama wa Hizb ut Tahrir, na Mhandisi Walid Kamil, walimtembelea Ustadh Imad Ismail Muhammad Ahmad, Katibu Mkuu wa Chama cha Wanasheria katika Jimbo la Al-Jazirah, afisini kwake Wad Madani. Majadiliano yalilenga kampeni ya Hizb ya kutibua mpango wa Amerika wa kuitenganisha Darfur. Kufuatia kauli ya mkuu wa ujumbe huo, Katibu Mkuu aliipongeza hizb kwa juhudi zake kubwa za kusimamisha Khilafah. Alisema kwamba anakubaliana na pendekezo la Hizb ut Tahrir kwamba Chama cha Wanasheria kipokee juhudi zake, na kwamba milango yao iko wazi kwa hilo.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |



