Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 1 Rabi' I 1447 | Na: HTS 1447 / 17 |
M. Jumapili, 24 Agosti 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Waitembelea Idara ya Muongozo na Ushauri katika Jimbo la White Nile
(Imetafsiriwa)
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan – Mji wa Rabak, White Nile, uliitembelea Idara ya Muongozo na Ushauri mnamo Jumapili, 1 Rabi' al-Awwal 1447 H sawia na tarehe 24 Agosti 2025. Ujumbe huo ulikutana na mkuu wa Sekretarieti katika Jimbo la White Nile, Sheikh Abdul Mubara Mahmoud Al-Mahmoud. Ujumbe huo uliongozwa na Dkt. Ahmed Muhammad Fadl Al-Sayyid, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, na alifuatana na Ustadh Faisal Madani, mwanachama wa Hizb ut Tahrir.
Baada ya kujitambulisha, mkuu wa ujumbe huo alieleza kuwa ziara hii inakuja ndani ya muundo wa kampeni iliyozinduliwa na Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan ya kuzuia kujitenga kwa Darfur, akiangazia hatari ya mpango huo kwa umoja wa nchi, ikizingatiwa kuwa ni suala la hatari ambalo lahitaji hatua za uhai au kifo.
Pia aliitaja kampeni iliyozinduliwa na hizb kutibua mpango wa kuitenga Sudan Kusini, akiashiria maafa na masaibu yaliyoikumba Sudan kutokana na kujitenga kwake, na jinsi Marekani ilivyofanikiwa katika hilo, na sasa inataka kuitenganisha Darfur.
Ujumbe huo pia ulijadili kuzingirwa kwa mji wa El Fasher na silaha ya njaa inayotumiwa dhidi ya watu wetu huko El Fasher, Deling, Kadugli na Gaza, ukitoa hadith za Mtume (saw) ambazo zinahimiza umoja baina ya Ummah.
Sheikh Abdul Mahmoud alikubaliana na kauli ya ujumbe huo na kusisitiza kuwa wanaunga mkono umoja wa Ummah hata ikiwa itamaanisha kutumia silaha. Alisisitiza kwamba mimbari ziko wazi kwenu, na kwamba tutawaelekeza maimamu wa misikiti na wanachama wetu wote kuzungumzia kuhusu suala hili nyeti.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |