Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  14 Jumada II 1447 Na: HTS 1447 / 64
M.  Ijumaa, 05 Disemba 2025

Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi
Dkt. Muhammad Al-Umda Hammad
[مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَىٰ نَحْبَهُ
وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً]
Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab 33:23]
(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, kwa nyoyo zilizoridhika na amri ya Mwenyezi Mungu, macho yanayobubujika machozi, na huzuni kubwa, inaomboleza mmoja wa mashababu wake aliyebeba ulinganizi wa kuregesha maisha kamili ya Kiislamu; kupitia kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, Mwenyezi Mungu amsamehe:

Dkt. Muhammad Al-Umda Hammad

Tulipokea habari za kifo chake jana, Alhamisi, tarehe 13 Jumada al-Akhar 1447 H sawia na tarehe 4 Disemba 2025, jijini Khartoum. Tunamwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amrehemu, amsamehe, na ampe Pepo ya juu zaidi.

Tunaomboleza kumpoteza kwake na kutoa rambirambi zetu za dhati kwa familia yake, watoto wake, ndugu zake, na wanachama wa dawah.

Jicho linamwaga machozi, na moyo unahuzunika, na kwa kweli tunasikitishwa sana na kuondoka kwako, Muhammad Al-Umda, lakini tunasema tu yale yanayomridhisha Mola wetu.

[إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]

“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqarah 2:156]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.