Ijumaa, 09 Muharram 1447 | 2025/07/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Vyombo vya Usalama katika Mji wa Al-Qadarif Vyawakamata Mashababu wa Hizb ut Tahrir vikiliunga mkono umbile la Kiyahudi!

Katika hotuba ya hadhara iliyotolewa na Mashababu wa Hizb ut Tahrir katika mji wa Al-Qadarif, kwenye soko la Al-Qadarif karibu na hospitali ya meno, mnamo siku ya Alhamisi, tarehe 23 Dhul-Hijjah 1446 H, inayolingana na 19/6/2025 M, Ustadh Awad Muhajir, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, alizungumza kuhusu uhalisia wa vita na umbile la Kiyahudi, furaha ya Waislamu kwa mashambulizi dhidi ya umbile hili, na kiu ya watu ya ushindi dhidi ya mkaaji huyu wa kimabavu wa ardhi tukufu—Masrah ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Alithibitisha faradhi ya kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo itaikomboa Palestina na ardhi nyenginezo za Kiislamu zinazokaliwa kwa mabavu. Hadhira iliitikia vyema hotuba hiyo, na kulikuwa na michangio tofauti tofauti kutoka kwa waliohudhuria.

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia: Matembezi ya Ukombozi: “Msafara wa Uthabiti Umesonga, Msafara wa Askari na Uanze!”

Matembezi yaliyohudhuriwa na umati mkubwa wa watu yalioandaliwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia yalitoka katika mji mkuu wa Tunis, baada ya swala ya Ijumaa, mnamo tarehe 20 Juni 2025 M kuanzia Msikiti wa Al-Fath chini ya kichwa: “Msafara wa Uthabiti Umesonga, Msafara wa Askari na Uanze!”

Soma zaidi...

Ni Dhambi Kubwa Kwa Ndege za Mayahudi Kuvuka Anga ya Tawala, Kuipiga Mabomu Iran na Kurudi Salama Bila Kutunguliwa na Tawala hizi Hata kwa Risasi Moja!

Trump alisema katika chapisho kwenye jukwaa la Kijamii la ‘Truth’: ["Iran na Israel wanapaswa kufanya makubaliano, na watafanya makubaliano, kama vile nilivyozifanya India na Pakistan kufanya." Aliendelea: "Vivyo hivyo, tutakuwa na AMANI, hivi karibuni, kati ya Israel na Iran! Miito mingi na mikutano inafanyika hivi sasa."(Sky News,15/6/2025). Mnamo Jumapili, msemaji wa jeshi la umbile la Kiyahudi alisema kupitia jukwaa la X kwamba "Israel ilitoa onyo kwa Wairan wanaoishi karibu na vinu vya nyuklia nchini Iran kuhama makaazi yao." Wakati huo huo, msemaji wa jeshi la 'Israel' alisema kuwa jeshi lilishambulia kituo cha nyuklia katika mji wa Isfahan, katikati mwa Iran. Tangu alfajiri ya Jumapili, Iran ilianza kurusha raundi mpya za makombora kwenye shabaha ndani ya 'Israel', na kusababisha vifo na makumi ya majeruhi, na kusababisha uharibifu mkubwa kwa nyumba na majengo. Kwa kujibu, Tehran imekuwa chini ya mashambulizi ya 'Israeli'. (Al Jazeera,15/6/2025).

Soma zaidi...

Pongezi kwa Idd Al-Adha Iliyobarikiwa 1446 H

Hizb ut Tahrir inatoa pongezi na baraka nyingi zaidi kwa Umma wetu mpendwa wa Kiislamu, wenye subira na wenye kukubali malipo licha ya maafa na majanga yote unaopitia, maafa na majanga ambayo ni mzigo mzito hata kwa kundi lililo imara zaidi la wanadamu, hususan watu wetu wenye subira mjini Gaza na katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, katika Sikukuu ya Idd ul-Adha. Tunamuomba Mwenyezi Mungu azijaalie siku za Idd hii kuwa ni utulivu katika nyoyo zao na wanyanyuliwe daraja mbele ya Mola wa walimwengu wote.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu