Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 525
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Watawala wa Waislamu Wanaogopa kwamba Watafuata baada ya Kuanguka kwa Dhalimu wa Ash-Sham!
Baada ya Kukombolewa Damascus, Ukombozi wa Palestina Utakuwa chini ya Bendera ya Khilafah Rashida kwa Idhini ya Mwenyezi Mungu.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Sudan ilifanya Jukwaa la Kila Mwezi la Masuala ya Ummah, mnamo siku ya Jumamosi, tarehe 5 Jumada Al-Akhir 1446 H sawia na tarehe 7 Disemba 2024 M lenye kichwa: “Wingi wa Majeshi na Wanamgambo ni Ishara ya Kuangamia kwa Dola, kwa hivyo ni ipi Njia ya Kutokea?”
Asharq Al-Awsat ilichapishwa mnamo tarehe 8 Disemba 2024: (Utawala wa Assad umeanguka: Upinzani wa Syria umetangaza leo, Jumapili, kwamba umeikomboa Damascus na kuupindua utawala wa miaka 24 wa Rais Bashar al-Assad. Taarifa ya upinzani kwenye televisheni ya taifa ilisomeka: “Sifa zote ni za Mwenyezi Mungu, mji wa Damascus umekombolewa na dhalimu Bashar al-Assad amepinduliwa.” Upinzani uliongeza kuwa wafungwa wote wameachiliwa huru.)
Ripoti kuhusu jibu la swali lililotolewa na Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata bin Khalil Abu Al-Rashtah, Mwenyezi Mungu amhifadhi, kuhusu matukio ya Syria na kuanguka kwa utawala wa Assad.
Kisimamo jijini Copenhagen Kusherehekea Kuanguka kwa Utawala wa Assad!
Maandamano mbele ya Bunge kupinga Ziara ya Abdel Fattah Al-Sisi nchini Denmark!
Kwa imani katika qadhaa ya Mwenyezi Mungu (swt) na kutaka malipo Yake, Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Jordan inamuomboleza Mbebaji Da’wah katika safu zake: Hajj Mustafa Abdullah Al-Issa Al-Jaber Al-Aboushi (Abu Anas) Aliyefariki kwenda kwenye rehema za Mwenyezi Mungu Mtukufu asubuhi ya leo, Jumanne, 3/12/2024, akiwa na umri wa miaka 80.