Mapinduzi ya Niger na Upotezaji Endelevu wa Dira wa Majeshi ya Waislamu
- Imepeperushwa katika Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Alhamisi iliyopita, Walinzi wa Rais nchini Niger walifanya mapinduzi dhidi ya serikali hiyo, kwani walitangaza katika taarifa iliyopeperushwa na runinga kwamba walikuwa wamemfukuza Rais wa Niger Muhammad Bazoum, na kuunda Baraza la Kitaifa kwa ajili ya Ulinzi wa Nchi linaloongozwa na Jenerali Abd al-Rahman Chiani, na punde tu Jeshi liliwafuata kwa kutangaza uungaji mkono wake kwa viongozi wa mapinduzi.



