Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
| H. 29 Jumada II 1447 | Na: H 1447 / 038 |
| M. Jumamosi, 20 Disemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Unafiki wa Magharibi; Kati ya Kulaani Tukio la Sydney, na Kimya Juu ya Mauaji katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina
(Imetafsiriwa)
Bado hakuna kiongozi hata mmoja wa nchi au kiongozi wa Magharibi au wa Kiarabu ambaye hajashutumu tukio la Sydney, ambapo watu kumi na tano waliuawa kwa kupigwa risasi kufuatia shambulizi lililolenga tamasha la Mayahudi la Hanukkah jijini Sydney. Hata hivyo hatujaona azma mithili ya hiyo katika kulaani jinai za umbile la Kiyahudi katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina katika kipindi cha miaka miwili iliyopita. Kama kawaida, rai jumla ya umma imepotoshwa, na kupuuzwa kabisa nia ya tukio hilo, kwani kila mtu alijikita kukemea kitendo hicho, bila kujali sababu iliyowafanya washambuliaji hao wawili kuwafyatulia risasi washerehekaji.
Wakati nchi za Magharibi zikichochea kampeni yake ya vita vya kimsalaba dhidi ya Uislamu na Waislamu, Rais wa Marekani Donald Trump ametumia vibaya tukio hilo kwa kuongeza mafuta zaidi kwenye moto, mnamo Jumanne tarehe 16 Disemba 2025, kwa kutoa wito kwa mataifa ya dunia kuanzisha vita vya kimataifa dhidi ya kile alichokiita “ugaidi mkali wa Kiislamu.” Trump vile vile alitangaza katika tafrija moja ya Hanukkah katika Ikulu ya White House, “Mataifa yote lazima yasimame pamoja dhidi ya nguvu ovu za ugaidi mkali wa Kiislamu na tunafanya hivyo.” Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese alibainisha kwamba watu hao wawili wenye silaha, mwanamume mmoja na mwanawe, walichochewa na “itikadi ya chuki.”
Waziri Mkuu wa umbile la Kiyahudi alihimiza dola za Kimagharibi kuzidisha juhudi zao za kupambana na chuki dhidi ya Mayahudi na kulinda jamii za Mayahudi, akisema mnamo Jumanne 16 Disemba, “Ninazitaka serikali za Magharibi zifanye kile kinachohitajika kupambana na chuki dhidi ya Mayahudi na kutoa usalama unaohitajika na usalama kwa jamii za Kiyahudi duniani kote. Watashauriwa vyema kuzingatia maonyo yetu ... nataka hatua haraka iwezekanavyo.”
Ili kufafanua mambo zaidi ya matamko ya kilaghai ya wanasiasa, tunathibitisha yafuatayo:
Kwanza: Hakuna ugaidi katika Uislamu, kama inavyodaiwa na nchi za Magharibi na kiongozi wa muungano wa Vita vya Msalaba, Trump, kwani Uislamu ni risala (ujumbe) wa Mwenyezi Mungu na rehema kwa watu wote. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):
[وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا كَافَّةً لِلنَّاسِ بَشِيرًا وَنَذِيرًا وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ]
“Na hatukukutuma ila kwa watu wote, uwe mbashiri, na mwonyaji. Lakini watu wengi hawajui.” [Surah Saba: 28] na neno pekee linalovuliwa kutokana na “ugaidi” linaloonekana katika Quran Tukufu linakuja katika muktadha wa kupigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu (swt) dhidi ya maadui wa Mwenyezi Mungu (swt), kutoka miongoni mwa makafiri na wahalifu, ili kunyanyua Neno la Mwenyezi Mungu (swt) kuwa juu kabisa, ambapo Mwenyezi Mungu (swt) amesema:
[وَأَعِدُّوا لَهُمْ مَا اسْتَطَعْتُمْ مِنْ قُوَّةٍ وَمِنْ رِبَاطِ الْخَيْلِ تُرْهِبُونَ بِهِ عَدُوَّ اللَّهِ وَعَدُوَّكُمْ وَآخَرِينَ مِنْ دُونِهِمْ لَا تَعْلَمُونَهُمُ اللَّهُ يَعْلَمُهُمْ]
“Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi walio fungwa tayari-tayari, ili kuwatishia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu, na wengineo ambao hamwajui, lakini Mwenyezi Mungu anawajua.” [Surah Al-Anfal 8:60].
Zaidi ya hayo, Uislamu unachukulia kuua mtu asiye na hatia kuwa ni jinai kubwa miongoni mwa madhambi makubwa, Mwenyezi Mungu (swt) amesema,
[مِنْ أَجْلِ ذَلِكَ كَتَبْنَا عَلَى بَنِي إِسْرَائِيلَ أَنَّهُ مَنْ قَتَلَ نَفْسًا بِغَيْرِ نَفْسٍ أَوْ فَسَادٍ فِي الْأَرْضِ فَكَأَنَّمَا قَتَلَ النَّاسَ جَمِيعًا وَمَنْ أَحْيَاهَا فَكَأَنَّمَا أَحْيَا النَّاسَ جَمِيعًا]
“Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote.” [Surah Al-Maidah:32].
Kwa hiyo, vipi kuhusu umbile la Kiyahudi ambalo, kwa uungwaji mkono kamili wa muungano wa Makruseda, liliua zaidi ya watu elfu sabiini wasio na hatia, katika muda usiozidi miaka miwili?!
Pili: Kile ambacho Trump anakiita “ugaidi wa Kiislamu” hakina uhusiano wowote na Uislamu na Waislamu. Trump anajua vyema kwamba ugaidi anaouzungumzia ni uundaji wa nchi yake na vyombo vyake vya usalama, na kuundwa kwa serikali vibaraka zinazofanya kazi chini ya amri yake katika Ulimwengu wa Kiislamu, ili kutekeleza kazi chafu inayotakwa na dola hizo, na kisha kuihusisha kwa uwongo na Uislamu na Waislamu. Haya yanafanywa kwa lengo la kupotosha sura ya Uislamu na kuwatenganisha watu nao, kwa kuhofia kwamba wanadamu wataachana fikra ya kimada ya Kimagharibi ambayo imewafanya kuwa duni na kuwachosha, ili kuikumbatia Dini kubwa ya rehema, Uislamu.
Tatu: Kuhusisha Uislamu na Waislamu kuwajibika kwa tukio la Sydney, na kuwatuhumu watu waliokuwa na silaha kwa chuki dhidi ya Mayahudi, ni kukimbia ukweli na kupuuza sababu halisi ya tukio hilo. Sababu ya msingi ni unafiki na undumakuwili unaofanywa na nchi za Magharibi. Wamagharibi hawaoni tatizo kwa umbile la Kiyahudi kuua zaidi ya watu elfu sabiini wasio na hatia katika muda usiozidi miaka miwili, na umbile la Kiyahudi linaendelea kuua hata baada ya kutia saini hati na mikataba inayowajibisha kusimamisha umwagaji damu, kwa dhamana ya Magharibi yenyewe. Kwa hivyo, anayehusika na tukio hili ni Magharibi yenyewe. Ni nchi za Magharibi ambazo zimeendelea kuunga mkono umbile la Kiyahudi, bila ya kikomo, kufanya mauaji makubwa, ambayo humsukuma hata mtu mwenye akili timamu na mvumilivu kabisa kwenye hasira na kupoteza utulivu.
Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.muslimworld.today |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) muslimworld.today |



