Kushutumu kwa Watawala wa Waislamu Mradi wa Kuwahamisha Watu wa Gaza hakufuti Upeo wa Aibu wa Usaliti wao
- Imepeperushwa katika Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Usaliti wa watawala wa Waislamu, na majeshi yao, kwa watu wa Gaza, na Palestina yote, kwa zaidi ya miaka 78 ya kukaliwa kwa mabavu Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, na umbile la Kiyahudi, ni fedheha kubwa. Haiwezi kufutwa kwa shutuma tu za kuhamishwa. Watawala hawa wameficha usaliti wao mkubwa katika kipindi cha miezi kumi na tano iliyopita. Nchi kadhaa zimeelezea kukataa mipango ya kuwahamisha watu wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina kutoka Ukanda wa Gaza, hivi karibuni Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, ambaye alisema mnamo Jumatatu, 10 Februari, "Hakuna mtu anayeweza kuwasukuma watu wa Palestina kuelekea Nakba mpya ya uhamisho." Erdogan alisisitiza kwamba "ukaliaji kimabavu wa 'Israel' lazima ubebe gharama ya ujenzi mpya wa Gaza peke yake," akionya dhidi ya "jaribio lolote la kuwalazimisha watu wa Palestina Nakba mpya ya uhamisho."



