Afisi ya Habari
Amerika
| H. 28 Jumada I 1447 | Na: 06 / 1447 H |
| M. Ijumaa, 19 Disemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ukandamizaji Unaoongezeka wa Marekani dhidi ya Mashirika ya Kiislamu - Toleo la Texas
(Imetafsiriwa)
Katika hatua ya kushangaza wiki hii, Gavana wa Texas Greg Abbott alitangaza Baraza la Mahusiano ya Kiislamu na Kiamerika (CAIR) na Ikhwan al-Muslimin kama “mashirika ya kigaidi ya kigeni.” Tangazo lake linaharamisha makundi haya kumiliki mali huko Texas na kuidhinisha hatua za kisheria za serikali dhidi ya vyama vinavyohusiana nayo. Ingawa Abbott aliweka uamuzi huo kama msimamo dhidi ya “misimamo mikali,” hatua hiyo inawakilisha ongezeko kubwa la ulengaji unaoendelea wa mashirika ya Kiislamu na inaangazia mgogoro mkubwa wa uhuru wa kuzungumza, ukandamizaji wa serikali, na unafiki katika jinsi Amerika inavyowatendea raia wake Waislamu.
Licha ya tangazo la Abbott kutokuwa na mamlaka yoyote ya Federali, linafanya kazi kama tishio la kiishara, likimpa Mwanasheria Mkuu wa Texas mamlaka ya kushtaki mashirika yanayodaiwa kuhusishwa na CAIR au Ikhwan al-Muslimin - bila kufafanua vigezo vya “ushirika” au taratibu za utekelezaji.
Hatua ya Abbott inafuatia miezi kadhaa ya mashambulizi ya mitandao ya kijamii na uchunguzi wa serikali wa mipango ya Waislamu, ikiwa ni pamoja na maendeleo ya Jiji la Epic karibu na Dallas, ambayo aliyaita “uwanja wa sharia” na kufanyiwa uchunguzi mwingi. Hatua hizi zinaonyesha muundo wazi wa kulenga jamii na mashirika ya Kiislamu chini ya kivuli cha sheria, huku wakati huo huo wakichochea hisia za chuki dhidi ya Uislamu kwa manufaa ya kisiasa.
Hapo awali, Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio na Seneta Ted Cruz walizungumzia kuhusu juhudi zinazoendelea za kuorodhesha Ikhwan al-Muslimin na CAIR kama mashirika ya kigaidi - mchakato waliouunda kuhusu wasiwasi wa usalama wa taifa. Kauli kama hizo zinaimarisha muundo wa muda mrefu ambapo mashirika na jamii za Kiislamu hutendewa kama maadui kwa kutetea tu kadhia za Kiislamu au kupinga sera ya kigeni ya Marekani.
Kwa miongo kadhaa, Waislamu nchini Marekani wamekuwa wakichunguzwa, kuorodheshwa, kuhesabiwa kuwa wahalifu, na kutishiwa chini ya pazia la kupambana na ugaidi na usalama wa taifa. Maneno ya chuki dhidi ya Uislamu kutoka kwa tawala zilizopita, zote mbili za Democrat na Republican, yamesababisha uhalifu wa chuki dhidi ya jamii ya Waislamu. Zaidi ya hayo, juhudi hizi zimeongezeka katika kipindi cha miaka miwili iliyopita hasa kutokana na ukosoaji wa jamii za Waislamu dhidi ya mauaji ya halaiki mjini Gaza na propaganda za Kizayuni zinazoshawishi mabadiliko ya sheria zinazochochea hatua kali za kukandamiza upinzani.
Mnamo Agosti 2025, tulitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu ongezeko hili dhidi ya makundi ya Waislamu na badala ya yanayojiri sasa tunawakumbusha wasomaji wetu yafuatayo:
Hili sio tu kuhusu Udugu wa Kiislamu au CAIR pekee bali linaathiri mashirika yote ya Kiislamu na jamii zetu kwa wakati mmoja. Kulenga mashirika ya Kiislamu kwa sababu za kisiasa - hasa yale yanayotetea kadhia za Kiislamu au utawala wa Kiislamu - hakuwezi kutazamwa kwa kutengwa na muundo mpana wa uadui dhidi ya Uislamu.
Mtume (saw) na Maswahaba (ra) walikabiliwa na marufuku ya kisiasa kama hiyo, uhamisho, na kampeni za uzushi mjini Makka - si kwa ajili ya vurugu, bali kwa ajili ya kulingania Uislamu.
Uislamu unatulazimisha sisi Waislamu kuilinda Dini yetu, kusema ukweli, na kujiandaa kwa pamoja kwa ajili ya ustawi wa Ummah. Sisi Waislamu nchini Amerika lazima tusimame imara pamoja kwenye Haki, kuunganisha sauti zetu, kuteteana, na kukataa vitisho vinavyokusudiwa kutunyamazisha na kutufanya tufiche Dini yetu.
Mwenyezi Mungu (swt) anatukumbusha:
[إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ]
“Hakika Waumini ni ndugu” [Al-Hujurat: 10]
[وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاء بَعْضٍ يَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُقِيمُونَ الصَّلاَةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَيُطِيعُونَ اللّهَ وَرَسُولَهُ أُوْلَـئِكَ سَيَرْحَمُهُمُ اللّهُ إِنَّ اللّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ]
“Na Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki walinzi. Huamrisha mema na hukataza maovu, na hushika Sala, na hutoa Zaka, na humt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao Mwenyezi Mungu atawarehemu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mtukufu Mwenye nguvu, Mwenye hikima.” [At-Tawbah: 71].
Sisi, kutoka Hizb ut Tahrir, tunayashajiisha mashirika ya Kiislamu kuwa walinzi wao kwa wao. Hili halihusu shirika moja pekee. Hili linahusu kubakia hai kwa kitambulisho chetu cha Kiislamu nchini Amerika. Jibu letu lazima liwe ni umoja, uwazi, na ustahamilivu. Huu ni mtihani kwa nguvu yetu ya pamoja.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Amerika
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Amerika |
Address & Website Tel: |



