Ijumaa, 29 Jumada al-thani 1447 | 2025/12/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  20 Jumada II 1447 Na: 1447 / 11
M.  Alhamisi, 11 Disemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Bajeti za Jordan Ni Nakala Zinazorudiwa katika Ufisadi Wao
na Kuzishughulikia Kupitia Madeni Kuna Wiana na Dori ya Kiutendaji ya Serikali na Haijali Uchungaji wa Mambo ya Watu  
(Imetafsiriwa)

Serikali ilikadiria, katika Rasimu ya Sheria ya Bajeti Kuu ya mwaka 2026, mapato ya umma yangekuwa takriban dinari bilioni 10.931, 75% kati yake yakiwa ni kutokana na kodi, na dinari milioni 735 kutoka kwa ruzuku za kigeni. Waziri wa Fedha alisema kwamba kiasi cha matumizi ya sasa ni dinari milioni 11,456, huku matumizi makuu yakifikia dinari milioni 1,600 pekee. Kuhusu nakisi inayotarajiwa kwa mwaka 2026, inakadiriwa kufikia takriban 4.6% ya Pato la Taifa.

Bajeti hii imeshughulikiwa kwa miongo kadhaa katika mzunguko usio na rutuba, ambapo rasimu ya sheria inapelekwa kwa Kamati ya Fedha katika Baraza la Wawakilishi, ambalo linaijadili na vyombo husika, kisha linawasilisha mapendekezo yake ya pembezoni kwa Baraza la Wawakilishi. Kisha wabunge wanaendelea kujadili rasimu hiyo katika mandhari ya kiusanii ambayo hurudiwa katika kwa kila bajeti, ili kupata uungwaji mkono wakati wa uchaguzi, kwani Baraza hilo linatarajiwa kuipigia kura leo ili kuidhinisha bajeti kupitia vishawishi au vitisho. Kisha serikali inaendelea mbele kwa fahari kwa ushindi unaohakikishwa chini ya msemo: “Tuliwatusi sana nao wakajishindia ngamia.”

Rasimu ya Sheria ya Bajeti ya mwaka 2026 inaegemezwa juu ya takwimu zilizokadiriwa za mapato na matumizi, kama ilivyo kawaida katika mfumo wa uchumi wa kibepari. Kwa hivyo, bajeti hii ilitegemea makisio ya ukuaji wa uchumi ulioongezeka kufikia 2.9%, kulingana na madai ya serikali, yanayotokana na miradi midogo ya mitaji inayokadiriwa ambayo haipunguzi ukosefu wa ajira wala kushibisha njaa, kama vile mradi wa Kitaifa wa kuondoa chumvi kwenye maji, miradi ya reli, na miradi ya utafutaji na usafirishaji wa gesi, ambayo kwa kawaida hucheleweshwa kwa miaka mingi—lau hata itatekelezwa.

Data kutoka Wizara ya Fedha ilionyesha kuwa deni lote la umma la Jordan, ikiwemo madeni ya Mfuko wa Uwekezaji (Usalama wa Jamii), ambayo yalifikia dinari bilioni 11 na kutishia kupoteza akiba za watu, yaliongezeka hadi dinari bilioni 46.849 kufikia mwisho wa Agosti mwaka huu, na kuunda 119% ya Pato la Taifa. Hii ni asilimia kubwa sana kulingana na viashiria vya uchumi wa kibepari, na ni dalili ya kutoweza kwa serikali kulipa madeni yake au kutoweza kwake kukopa katika siku zijazo.

Kiasi cha riba kinachoitwa huduma ya madeni kilizidi dinari bilioni 3 na kufikia mara mbili ya mgao wa matumizi ya mtaji kiasi cha dinari bilioni 1.6, kutokana na programu tasa za Mfuko wa Fedha wa Kimataifa ambao serikali ya Jordan umejitolea kwake tangu 1989. Programu hizi zinategemea kutibu uchumi unaoyumba kwa mikopo zaidi na kuratibiwa kwake upya, zikisaidiwa na ukadiriaji wa uongo wa mashirika ya mikopo ya Marekani na Ulaya. Utulivu wa ukadiriaji wa mikopo ya Jordan katika “BB-“ unaiwezesha kukwama zaidi katika mikopo ya riba. Hivyo, takwimu za bajeti ya fedha ya mwaka 2026 zinaonyesha kwamba serikali inajiandaa kwa mwaka mkubwa zaidi wa malipo yanayopaswa kulipwa, sehemu kubwa zaidi ambayo ni dinari bilioni 7.3—zitatumika kulipa madeni na kuyahudumia.

Sera hii inalenga kuizamisha nchi katika mtego wa madeni ili iweze kuingiliwa kisiasa ili iendelee kwa mujibu wa dori ya  kiutendaji wa kikoloni na kujisalimisha kwa umbile la Kiyahudi, Amerika, na Ulaya, ambayo ni mpango wa Trump kwa Gaza. Hali ya kiuchumi imefikia kiwango cha kuzorota kiasi kwamba imesimama ukingoni mwa shimo, na kufanya kuanguka kuwezekane wakati wowote kwa uamuzi wa kisiasa kutoka kwa wakoloni wanaojificha Magharibi, kama utawala wa Trump ulivyofanya mwanzoni mwa muhula wake wa pili, kabla ya baadaye kuiregesha huku ikionyesha kijiti.

Tatizo la kiuchumi nchini Jordan haliko katika mifumo ya mbinu ya kuandaa bajeti yenye takwimu zake za mapato, matumizi, nakisi, na deni; badala yake, linazidi hilo hadi kwenye wazo ambalo bajeti inategemea na sera ya kiuchumi iliyopitishwa na serikali. Hatuwaoni wale wanaoshughulikia matibabu ya mgogoro huu wa kiuchumi wakishughulikia mzizi wa tatizo, isipokuwa kupitia masuluhisho ya viraka yanayoongeza muda wa tatizo na kuliregesha tena.

Hata hivyo, katika juhudi zetu za kusimamisha Dola ya Khilafah, tunaangalia suluhisho pekee msingi linaloweza kushughulikia tatizo la kiuchumi nchini Jordan na kanda hii, kwa sababu sera yake ya fedha imeunganishwa kwa karibu na Aqidah ya Kiislamu na hukmu za Sharia zinazohusiana na mfumo wa kiuchumi katika Uislamu, na si kwa mfumo wowote uliotengenezwa na binadamu kama vile ubepari.

Kwa hivyo, hakuna bajeti ya kila mwaka iliyowekwa, hakuna sheria iliyotungwa kwa ajili yake, na haiwasilishwi kwa Bunge la Kitaifa, kwa sababu mwenzake ni Bayt al-Mal (Hazina ya Dola). Mapato ya Bayt al-Mal si takwimu zilizokadiriwa wala zinazotarajiwa; badala yake, ni takwimu halisi zinazohusiana na fedha ambazo kwa kweli hukusanywa kwa mujibu wa hukmu za Sharia. Vile vile, matumizi ni matumizi halisi ambayo kwa kweli hutumika kulingana na hukmu za kudumu za Sharia ambazo hazibadiliki kadri miaka inavyopita.

Uislamu unaharamisha mikopo ya riba, kwani riba katika Uislamu ni vita vilivyotangazwa dhidi ya Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw). Uchumi wake hautegemei deni au kodi. Badala yake, msingi wa mfumo wa uchumi wa Kiislamu ni ugavi wa mali, sio mzunguko wa deni, na utambuzi wa uchungaji wa kweli kwa mambo ya watu na kuwainua kwa kuchangamsha utajiri katika uzalishaji na uchumi halisi, si katika masoko ya fedha na dhamana hewa. Ndani yake, mtawala anatekeleza utumiaji na uwekezaji wa rasilimali kwa sababu ni mali ya umma na chanzo kikuu ambacho mapato yake yanagawanywa kwa Ummah. Jordan imejaa rasilimali nyingi zilizozungumziwa na wataalamu wengi wa Jordan tangu miaka ya 1960, ambazo Hizb ut Tahrir ilizitaja wakati huo. Hata hivyo, sera ya serikali hii inalazimisha kutozitoa ili kuhifadhi hali halisi iliyoko kama hoja ya unyenyekeshwaji kisiasa.

Enyi Waislamu nchini Jordan... Enyi Watu wa Jordan:

Tatizo nchini Jordan si tatizo la deni kubwa, wala umaskini mkubwa na viwango vya ukosefu wa ajira. Badala yake, kimsingi tatizo si tatizo la kiuchumi. Tatizo msingi liko katika ukweli kwamba Jordan inatawaliwa na serikali hii. Kwani Jordan, kama umbo, ilikatwa na wakoloni makafiri kutoka asili yake na kisiasa na kiuchumi iliyofungwa nao. Kwa hivyo, matatizo ya Jordan hayatatatuliwa kimsingi isipokuwa kwa kuregea kwenye asili yake ya kijiografia kama sehemu ya Ash-Sham na Dola yake ya Kiislamu, ili nafasi yake ya kisiasa na kiuchumi iweze kuimarishwa kupitia kuunganishwa na mazingira yake kutoka ardhi za Waislamu, ambao rasilimali zao wakoloni makafiri wanazimezea mate.

[وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُرَىٰ آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَفَتَحْنَا عَلَيْهِم بَرَكَاتٍ مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ]

“Na lau kuwa watu wa miji wangeli amini na wakamchamngu, kwa yakini tungeli wafungulia baraka kutoka mbinguni na katika ardhi.” [Al-A‘raf:96]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu