Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
| H. 12 Jumada II 1447 | Na: H.T.L 1447 / 14 |
| M. Ijumaa, 05 Disemba 2025 |
Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi
Marwan Al-Khatib (Abu Muhammad)
[مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَىٰ نَحْبَهُ وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً]
“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab 33:23]
(Imetafsiriwa)
Hizb ut Tahrir / Wilayah Lebanon inamuomboleza:
Mwanachuoni mtukufu, khatib, sheikh, mwandishi, na mshairi, Marwan al-Khatib (Abu Muhammad),
aliyefariki leo, Ijumaa, 14 Jumada al-Akhir H sawia na 5 Disemba 2025 M, akiwa na umri wa miaka 60, katika Kambi ya Nahr al-Bared kaskazini mwa Lebanon.
Mwanachuoni huyu mtukufu, Sheikh, na mwanafasihi alikuwa mfano bora wa mtu aliyejitolea kalamu na maandishi yake kuelezea masuala yanayowakabili Waislamu.
Miongoni mwa mapendekezo mengi, hakuona suluhisho la masuala haya zaidi ya Khilafah na bendera ya Uqab. Hivyo alijiunga na Hizb ut Tahrir katika ulinganizi wake wa kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume. Uandishi wake ulikuwa umejaa sifa za kifasihi na kina cha kifikra, na kumfanya apate jina la “Mshairi wa Fikra.” Alikuwa mtaalamu wa kujaza mandhari ya fasihi na mawazo ya kina na kadhia nyeti aliyoitetea kwa imani isiyoyumba hadi kifo chake, alipobaki imara katika kujitolea kwake kwa kadhia hiyo. Mwenyezi Mungu amjumuishe miongoni mwa wale aliozungumza kuwahusu (swt):
[وَمَن يُطِعِ اللَّهَ وَالرَّسُولَ فَأُولَٰئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاءِ وَالصَّالِحِينَ وَحَسُنَ أُولَٰئِكَ رَفِيقاً]
“Na wenye kumt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume, hao wa pamoja na wale alio waneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii, na Wakweli, na Mashahidi, na Watu wema. Na uzuri ulioje kuwa pamoja na watu hao!” [An-Nisa 4:69], na ayafanye aliyoyaandika kwa mkono wake wa kulia katika kueneza da’wah na kuunusuru Uislamu kuwa nuru katika Kitabu Chake Siku ambayo mali wala watoto havitafaa kitu, isipokuwa kwa yule atakayemjia Mwenyezi Mungu kwa moyo uliosalimika. Jicho linabubujika machozi na moyo unahuzunika, na tunasikitishwa sana na kuondoka kwako, Abu Muhammad, na tunasema tu yale yanayomridhisha Mola wetu Mlezi, Mwenyezi Mungu Mtukufu: رَاجِعُونَ “Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na hakika kwake yeye tutaregea.”
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Lebanon
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Lebanon |
Address & Website Tel: 009616629524 http://www.tahrir.info/ |
Fax: 009616424695 E-Mail: ht@tahrir.info |



