Jumapili, 23 Safar 1447 | 2025/08/17
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Kauli za Netanyahu baina ya Uhalisia wa Umbile lake na Msimamo Unaofifia wa Serikali ya Misri

Kauli za Waziri Mkuu wa umbile la Kiyahudi, Benjamin Netanyahu, ambazo alizungumza moja kwa moja kuhusu kile kiitwacho “Israel Kubwa zaidi” na kuhusu mipango ya uhamishaji na upanuzi, zinafichua kwa mara nyengine tena itikadi iliyokita mizizi ndani ya nyoyo za viongozi wa umbile hili; itikadi ya khiyana, usaliti, na ulafi wa ardhi ya Waislamu. Matamshi haya si kuteleza kwa ulimi, bali ni tafsiri ya kivitendo ya mipango iliyoandikwa katika fikra ya kisiasa ya Kizayuni, na mipango inayotekelezwa uwanjani hatua kwa hatua.

Soma zaidi...

Mkataba wa Gesi na Umbile la Kiyahudi Ununuzi wa Utajiri wetu ulioibiwa na Msaada kwa Adui yetu Mnyakuzi

Katika kitendo kipya kinachojumuisha kiwango cha mporomoko na ubaraka ambao utawala wa Misri umefikia, ilitangaza kusainiwa kwa makubaliano makubwa na umbile la Kiyahudi ya kuagiza gesi asilia kutoka kwa uwanja wa Leviathan katika ardhi iliyonyakuliwa ya Palestina, kwa thamani inayokaribia dolari bilioni 35 hadi mwaka wa 2040. Chini yake, umbile la Kiyahudi linauza nje ya nchi karibu mita za ujazo 130 za gesi nchini Misiri, kutumika kukidhi mahitaji ya ndani na kusafirisha nje kupitia vituo vya kutengeneza gesi vya Misri. Makubaliano haya yamepigiwa debe kama "kuimarisha usalama wa nishati," huku kiuhalisia yakiwa ni usaliti kwa Ummah, kupuuza utajiri wake, muungano na adui yake, na msaada kwa uchumi wake unaodhoofika.

Soma zaidi...

Magereza ya Misri: Kati ya Mateso na Mauaji Pindi Heshima Inapokanyagwa Haki Huuawa!

Katika tukio jengine la mara kwa mara la uhalifu uliofichwa, kijana mmoja aitwaye Ayman Sabry alikufa ndani ya kituo cha polisi katika Jimbo la Dakahlia kutokana na mateso ya kikatili, ambayo yaliacha alama wazi kwenye mwili wake. Chini ya masaa 48 baadaye, kijana mwengine alikufa ndani ya Kituo cha Polisi cha Al-Saff katika Jimbo la Giza, huku kukiwa na ripoti thabiti za kutelekezwa kimakusudi, dhulma, na ukatili, na kuvigeuza vituo vya polisi kuwa sehemu za vifo cha polepole.

Soma zaidi...

Yeyote Anayezuia Mkate Usifike Gaza Hapaswi Kuzungumzia kuhusu Utu, Ewe Waziri wa Mambo ya Nje Rafah: Imo ndani ya Tundu la Uvamizi... au imo Ndani Mshiko wa Serikali ya Misri?!

Katika mandhari ambayo hakuna jicho linaloweza kukosa kuiona, watoto wa Gaza wanasimama kwenye vifusi vya nyumba zao, wakikimbilia tama la maji, kipande cha mkate, au dozi ya dawa, wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri anajitokeza mbele yetu akizungumzia "nia ovu" na "heshima ya sera ya kigeni," katika jaribio la kuiondolea serikali ya Misri dori yake halisi katika mzingiro wenye kunyonga pumzi uliolazimishwa juu ya Ukanda wa Gaza.

Soma zaidi...

Pindi Milango Inapofungiwa wenye Njaa na Kunusuriwa Kukanyimwa, Sura Hasiri ya Serikali ya Misri na Wapambe wake Inafichuliwa

Katika wakati ambapo Gaza inastahamili moja ya nyakati kandamizi na za kikatili zaidi katika historia, ambapo, pamoja na kuuawa kwa mashambulizi ya mabomu, watoto wanakufa kwa njaa, wanawake kwa huzuni, na wazee kwa magonjwa, Meja Jenerali Khaled Mewaghar, Gavana wa Sinai Kaskazini, alitoa matamshi ambayo yanakinzana na matakwa rahisi zaidi ya  maadili ya kiakhlaki na ya kibinadamu matakwa ya udugu wa Kiislamu. Alisema: “Ikiwa watu wa Gaza watafikia kiwango fulani cha njaa, wana chaguzi tatu: ima kwenda upande wa Israel na kukabili milio ya risasi, kujitupa baharini, au kuelekea Misri—jambo ambalo haliwezekani.”

Soma zaidi...

Kuzingirwa kwa Gaza ni Ushahidi wa Khiyana ya Serikali ya Misri

Gaza imeingia katika awamu ya tano njaa (awamu ya janga la njaa), kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa. Huku Waislamu kila mahali wakijaribu kuwanusuru ndugu zao kwa michango na kuanzisha misafara ya kuvunja mzingiro dhidi yao, nchi jirani zinatazama bila harakati yoyote—mbele yao zaidi ni Misri, ambayo ina mpaka na Gaza, lakini inadai kuwa haina usemi katika suala hilo na imeridhia kuchukua dori ya mpatanishi. Hivyo, je, kweli Misri haina uwezo wa kuwanusuru watu wa Gaza?!

Soma zaidi...

Enyi Wanazuoni wa Al-Azhar: Ikiwa hamtasema neno la haki leo... lini basi?!

Katika wakati ambapo sura za mauaji yanayofanywa na Mayahudi mjini Gaza zikiongezeka, na chakula, dawa, na maji vikizuiliwa kwa watoto, wanawake na wanaume, Al-Azhar ilitoa tamko la kulaani "jinai ya kuweka njaa" inayofanywa na umbile halifu la Kiyahudi. Taarifa hiyo ilifutwa baadaye! Basi je, inajuzu kilio dhidi ya dhalimu kifutwe?! Na je, sauti ya wanazuoni inaweza kukaa kimya dhidi ya mauaji?! Taarifa hiyo ilikuja ikiwa imejaa misamiati ya kibinadamu, yenye kuwavutia watu wenye dhamiri hai, jumuiya ya kimataifa, na dola zenye ushawishi, na kutoa wito wa kufunguliwa kwa vivuko na utoaji wa misaada. Umbile la Kiyahudi lilielezewa kuwa linafanya uhalifu wa njaa, likituhumiwa kwa mauaji ya halaiki na kuzuia misaada, na ilitoa wito kwa mashirika ya kibinadamu, Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa kusonga mbele kufungua vivuko, pamoja na kuwaombea dua watu wa Gaza kwamba Mwenyezi Mungu awanusuru na alipize kisasi kwa ajili yao.

Soma zaidi...

Hasira ya Watu wa Gaza kutoka Ng'ambo za Bahari Inataka Mzingiro Uvunjwe... Watu wa Misri na Jeshi lake Watakasirika Lini? Lini Hasira yao Itakuwa Moto wenye Kuteketeza Umbile la Kiyahudi na Tawala za Mamluki Zinazolilinda?

Wakati Gaza ikiwa inakufa kwa njaa, ikizingirwa kwa kimya cha aibu cha Waarabu na njama ya wazi ya kimataifa, kijana mmoja wa Kimisri kutoka ng'ambo, Anas Habib, alifunga milango ya ubalozi wa Misri nchini Uholanzi na kumwaga unga kwenye kizingiti chake. Alipiga kelele kwa jina la watu waliozingirwa wa Gaza na kuliita jeshi lake nchini Misri kuvunja mzingiro, kufungua kivuko, na kumaliza njaa ya kupangwa... Kilio kutoka nchi ya mbali kilisikika ndani ya nyoyo huru. Je, kuna yeyote kati ya watu wa Misri atakayejibu? Je, kuna ulinzi wowote katika nyoyo za watu wa jeshi la Kinana? Au kufuli zilizowekwa kwenye ubalozi wa Misri jijini The Hague ni za kikatili kidogo kuliko kufuli zilizowekwa kwenye utashi na silaha zao?!

Soma zaidi...

Kuitelekeza Gaza ni Doa katika vipaji vya Nyuso Zenu Enyi Wanajeshi wa Kinana na muhimu zaidi, ni Swali kutoka kwa Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama

Kila siku, mtoto mjini Gaza hufa kwa njaa, au mzee hupumua pumzi yake ya mwisho bila dawa, au mwanamke hufunga macho yake kwa mara ya mwisho kwa maumivu yasiyoweza kuvumilika kutokana na kiu au njaa. Kila saa mbingu hutokwa na machozi, mawe yanapiga kelele, na ardhi inawalaani wale waliowaacha peke yao. Hii ndiyo Gaza... Gaza, ambayo imezingirwa si tu kwa mipaka na vifaru, bali na uzio wa usaliti uliosukwa na viongozi wa majeshi, watawala wa khiyana, na kimya cha Umma wao.

Soma zaidi...

Kuhamishwa kwa Watu wa Arish ni Uhalifu wa Kisiasa Uliojificha kama Maendeleo

Wakati serikali ya Misri ikizungumzia "kuimarisha bandari ya Arish," kuigeuza kuwa bandari ya kimataifa na kuiunganisha na mradi mpya wa ukanda wa kiuchumi, uhalifu wa halisi unafanywa dhidi ya wakaazi wa kitongoji cha Al-Raisa huko Arish. Watu wanalazimishwa kuondoka majumbani mwao chini ya athari ya matingatinga, na nyumba zao zinabomolewa kinyume na matakwa yao kwa kisingizio cha manufaa ya umma. Wanakabiliwa na shinikizo la kisaikolojia na mazungumzo ambayo hayaendani na hadhi ya kibinadamu na yanakiuka kanuni za Kiislamu.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu