Ijumaa, 07 Safar 1447 | 2025/08/01
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  1 Safar 1447 Na: 1447/07
M.  Jumamosi, 26 Julai 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kuzingirwa kwa Gaza ni Ushahidi wa Khiyana ya Serikali ya Misri
(Imetafsiriwa)

Gaza imeingia katika awamu ya tano njaa (awamu ya janga la njaa), kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa. Huku Waislamu kila mahali wakijaribu kuwanusuru ndugu zao kwa michango na kuanzisha misafara ya kuvunja mzingiro dhidi yao, nchi jirani zinatazama bila harakati yoyote—mbele yao zaidi ni Misri, ambayo ina mpaka na Gaza, lakini inadai kuwa haina usemi katika suala hilo na imeridhia kuchukua dori ya mpatanishi. Hivyo, je, kweli Misri haina uwezo wa kuwanusuru watu wa Gaza?!

Tangu kuanza hujuma za Kiyahudi dhidi ya Gaza, serikali ya Misri imedai kuwa inatoa kila iwezalo kuwanusuru watu wetu wa Gaza na kukanusha kuwa na dori yoyote katika kufunga vivuko na kuizingira Gaza. Hata hivyo, ushahidi unadhihirisha ukweli wa uongo wake, na kwamba hali ya sasa isingeweza kutokea bila ya kushirikiana na Mayahudi hata kabla ya vita vyao dhidi ya Gaza. Mwanzoni mwa uvamizi huo, Ummah ulianza kuitaka Misri iingilie kati ili kuzuia umbile la Kiyahudi lisiwapige mabomu watu wetu mjini Gaza kwa roketi, lakini kila mtu alishtushwa kwamba iliwaruhusu hata kuwapiga mabomu Wamisri wenyewe kwenye kivuko cha Rafah, eneo la Al-‘Ajarah kusini mwa Rafah, na maeneo yaliyotawanyika huko Sinai. Wanajeshi walitazama makombora ya Mayahudi yakiwavuna kaka na dada zao mjini Gaza—au wanajeshi wenzao mpakani—bila harakati zozote kutoka kwa dola yao; kwa hivyo, vita hivi vilizinduliwa kwa matukio ya usaliti na utiifu.

Serikali ya Misri haikutosheka na kumwaga damu za Waislamu bali hata iliruhusu umbile la Kiyahudi kukikamata kivuko cha Rafah, ikipuuza masharti ya mkataba wa amani ambao imekuwa ikiutumia siku zote kuhalalisha kufeli kwake kuwanusuru watu wetu nchini Palestina. Hii haitokani na udhaifu wa jeshi la Misri, bali inatokana na khiyana, na ushahidi wa hili ni kwamba utawala huu haukuchukua msimamo wowote. Tukianzia, hata haukushutumu uvamizi wa Mayahudi wa kivuko hicho, wala haukuingilia kati kuuzuia kwa nguvu, au angalau kutumia njia yoyote ya shinikizo dhidi yao. Ilitosheka tu na kukanusha tuhuma ya kufunga kivuko hicho na kudai kwamba jambo hilo liko mikononi mwa umbile la Kiyahudi kikamilifu—kana kwamba inatambua haki ya umbile hili nyakuzi kudhibiti kivuko hicho!

Ni yakini kwamba mada hii haiwezi kujadiliwa bila kutaja Mkondo wa Suez, ambao unachukuliwa kuwa mojawapo ya njia muhimu zaidi za shinikizo kwa umbile la Kiyahudi na Amerika. Pia ni yakini kwamba Misri iliitumia kwa njia mbaya zaidi. Video zilienea zikionyesha manuari zilizobeba bendera za Amerika na umbile la Kiyahudi zikivuka humo. Misri ilidai haiwezi kuwazuia kuvuka mkondo huo kutokana na sheria za kimataifa—ikithibitisha kwa wote kwamba sheria hizi huonekana pale tu zinapotumikia maslahi ya mkoloni kafiri Magharibi!

Hapa nchini Misri, tunashuhudia matukio mabaya zaidi ya usaliti na utiifu unaofanywa na serikali hii iliyoundwa na ukoloni kuchukua nafasi ya mfumo wa Kiislamu. Tunaiona ikishiriki katika mauaji ya ndugu zetu mjini Gaza kwa kuwazingira, kuzuia misaada kuwafikia, na kuzuia juhudi zozote za kuvunja mzingiro juu yao kwa kutii amri za Mayahudi. Inawakamata wale wanaokusanya michango au kujaribu kufikia kivuko hicho ili kuvunja mzingiro. Unaona mojawapo ya matukio ya kustaajabisha zaidi: Wanaharakati wasio Waislamu wakiwasihi kwa machozi askari wa Kiislamu wawaruhusu kuingia kuwasaidia watu wetu huko Gaza. Tumeshuka kiwango duni kiasi gani?!

Enyi askari wa Misri, ardhi ya Kinana: Sisi, watu wa Misri tunakaribia kufa kwa huzuni tunapowaona ndugu zetu wa Gaza wakiuawa, na tunajua kwamba mnamiliki zana na silaha zinazowawezesha kuinusuru na kuikomboa Gaza na Palestina yote. Hivyo ikimbilieni heshima hii kubwa! Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi, naye ndiye Msaidizi wenu, na kamwe hatapoteza amali zenu.

[إِن يَنصُرْكُمُ اللّهُ فَلاَ غَالِبَ لَكُمْ وَإِن يَخْذُلْكُمْ فَمَن ذَا الَّذِي يَنصُرُكُم مِّن بَعْدِهِ وَعَلَى اللّهِ فَلْيَتَوَكِّلِ الْمُؤْمِنُونَ]

“Akikunusuruni Mwenyezi Mungu hapana wa kukushindeni, na akikutupeni ni nani, basi, baada yake Yeye ataye kunusuruni? Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu.” [Aal-i-Imran: 160]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 
http://hizb.net/
E-Mail:  info@hizb.net

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu