Ijumaa, 07 Safar 1447 | 2025/08/01
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  28 Muharram 1447 Na: HTS 1447 / 07
M.  Alhamisi, 24 Julai 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Serikali ya Matumaini Yageuka Jinamizi kwa Wananchi kwa Kuporomoka kwa Pauni ya Sudan!

(Imetafsiriwa)

Katika hotuba yake baada ya kula kiapo cha kuwa Waziri Mkuu, Kamil Idris alisema: “Kauli mbiu yetu ni matumaini, na dhamira yetu ni kufikia usalama, ustawi, na maisha ya utulivu kwa kila raia wa Sudan!” Katika taarifa yake ya kwanza kwa vyombo vya habari, alitangaza kuwa atatoa muda na juhudi zake kuhakikisha maisha ya heshima kwa kila Msudan.

Sasa, inaingia mwezi wa tatu na baraza lake la mawaziri bado halijaundwa kikamilifu matumaini aliyoahidi yamegeuka kuwa jinamizi linalosumbua. Ilianza na kuporomoka kwa pauni ya Sudan dhidi ya sarafu nyenginezo, hasa dolari. Soko sambamba (jeusi) lilishuhudia kupanda kwa kasi, ambapo dolari ilivuka kizuizi cha pauni 3,000 za Sudan. Kuzorota huku kwa kiwango cha ubadilishaji wa fedha za ndani kumesababisha kupanda kwa bei ya mafuta na bidhaa muhimu, na hivyo kukaza maisha ya watu ambayo tayari ni magumu kutokana na vita na athari zake. Katikati ya hali hii ya janga, Waziri wa Fedha anatoa tu ahadi na hakikisho ambalo halishibi njaa wala kupunguza mateso!

Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, kwa kuzingatia mzozo huu wa kunyonga pumzi unaowakabili watu, tunafafanua ukweli ufuatao:

Kwanza: Miongoni mwa sababu za kimsingi ambazo zimepelekea, na zinazoendelea kusababisha hali hii mbaya ya kiuchumi:

A. Kuchapisha sarafu ya karatasi bila kuongemezwa thamani yake, kwa kisingizio cha ubadilishaji sarafu, ikifuatiwa na kukamilika kwa mchakato wa kubadilisha sarafu katika majimbo ya Gezira na Khartoum, miongoni mwa mengine.

B. Imethibitishwa kuwa baadhi ya sarafu za zamani ambazo zilibadilishwa zimevuja sokoni na kusambazwa tena, na hivyo kupunguza thamani ya nguvu ya ununuzi wa sarafu hiyo.

• C. Kuendelea kwa vita na kuongezeka kwa gharama zinazohusiana navyo, pamoja na uhalifu unaofanywa na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) ikiwa ni pamoja na kuharibu mitambo ya kuchapisha sarafu, kuiba mashini, na kutekeleza udanganyifu mkubwa wa fedha bandia za ndani.

Pili: Sharia imebainisha dhahabu na fedha kama msingi wa ubadilishanaji wa fedha, kwani zina thamani ya dhati inayohakikisha uthabiti wa ubadilishaji. Hata hivyo, serikali, kwa kufuata sera za makafiri wakoloni wa Magharibi hasa kuchapisha fedha za karatasi zisizo egemezwa thamani yake na kujisalimisha kwa maagizo ya IMF na Benki ya Dunia kupitia sera ya ubadilishanaji wa fedha kumeiingiza sarafu yetu katika mporomoko wa kila siku dhidi ya dolari, ambayo yenyewe ni karatasi na wino tu. Ni kutabanni kwa serikali sera hizi ndiko kumetufikisha kwenye mporomoko huu mbaya, licha ya utajiri mwingi unaoonekana na uliofichika wa Sudan.

Tatu: Tumempa kafiri mkoloni mamlaka na udhibiti juu yetu, licha ya uharamishaji madhubuti wa Sharia. Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

[وَلَنْ يَجْعَلَ اللهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلاً]

wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.” [Surat An-Nisa:141].

Wanaingilia mambo yetu kupitia kile kinachoitwa “makongamano ya amani,” ambayo kwayo Sudan Kusini ilitenganishwa, na sasa wanapiga ngoma za kongamano jijini Washington mwishoni mwa mwezi huu. Tunachohofia zaidi ni kwamba mgogoro huu unaweza kutengenezwa kimakusudi ili kulazimisha kukubali uovu wowote unaoweza kutokea kutokana na kongamano hilo hasa kuhusu uwezekano wa kujitenga kwa eneo la Darfur.

Kwa kumalizia, tunawaambia watu wetu wa Sudan: Ukandamizaji huu na uingiliaji wa wazi wa makafiri wakoloni katika maisha yetu – kupitia vibaraka wao wa ndani – utamalizwa tu na Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Basi inukeni na mufanye kazi na Hizb ut Tahrir, uongozi wa kweli na muaminifu, ili kuisimamisha.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا للهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Surat Al-Anfal :24]

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com
Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: « Mwaliko wa Kuhudhuria Kikao cha Kisiasa

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu