Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 22 Safar 1447 | Na: HTS 1447 / 15 |
M. Jumamosi, 16 Agosti 2025 |
Hotuba ya Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan katika Mkutano na Waandishi wa Habari mnamo Jumamosi, 22 Safar 1447 H sawia na 16/08/2025 M, yenye kichwa:
“Wito kwa Watu wa Sudan... Ikamateni Darfur Ili Isiungane na Kusini”
(Imetafsiriwa)
Mnamo Jumamosi, 26/7/2025, Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vilitangaza kuundwa kwa serikali sambamba na serikali iliyopo nchini Sudan, katika mji mkuu wa Darfur Kusini (Nyala). Hatua hii ya RSF ni hatua ya juu katika kutenganisha eneo la Darfur, ambalo inalidhibiti, isipokuwa sehemu za mji wa El Fasher, ambao mzingiro wa kukandamiza umewekwa juu yake kwa zaidi ya mwaka mmoja, na kuanzisha mashambulizi mfululizo dhidi yake ili kuuangusha, ili eneo zima la Darfur liwe chini ya udhibiti wake.
Enyi watu wetu wa Sudan:
Mchakato wa Amerika wa kutenganisha Darfur ulianza miaka mingi iliyopita. Pia ilishikilia faili la Sudan Kusini hadi ilipojitenga na Kaskazini. Sasa, inaendelea na matukio yale yale yaliyotenganisha Kusini, ili kutenganisha Darfur. Ilianza hili kivitendo kwa kutia saini kile kinachoitwa makubaliano ya amani mnamo tarehe 14 Julai 2011, ambapo ililipatia eneo la Darfur upanuzi wa uhuru wa kujitawala. Suala la uhuru wa kujitawala daima litakuwa mwanzo wa kweli wa mchakato wa kugawanyika. Ingawa, yaani, Amerika, iliunda makubaliano haya, haikuyachukulia kuwa ni makubaliano ya mwisho. Wakati huo, Naibu msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Mark C. Toner, alisema baada ya kutiwa saini kwa makubaliano hayo: “Makubaliano haya ni hatua nzuri kuelekea suluhisho la kudumu la mgogoro wa Darfur.”
Kinachothibitisha kuwa Amerika ndiyo iliyoitenganisha Sudan Kusini na inataka kuyachana mabaki ya Sudan ni kauli za Omar al-Bashir, katika mahojiano yake na Shirika la Sputnik la Urusi, yaliyochapishwa mnamo tarehe 25/11/2017, ambapo alisema: “Masuala ya Darfur na Sudan Kusini yalipata usaidizi na kuungwa mkono na Amerika, na chini ya shinikizo lake, Sudan Kusini ilitenganishwa,” na akaongeza: “Sasa tunayo taarifa kwamba juhudi za Amerika ni kuigawanya Sudan katika nchi tano,” ambapo inathibitisha kwamba Amerika ndiyo iliyoitenganisha Sudan Kusini, na sasa inatafuta kuitenganisha Darfur.
Endapo itafaulu – Mwenyezi Mungu aepushie mbali – itayachana maeneo mengine ya Sudan moja baada ya jengine, na itafanya hivyo kwa kuchora mipaka ya nchi tano ndani ya nchi yenu kwa damu yenu na ya watoto wenu, kama ilivyofanya hapo awali kwa kutenganisha kusini kwa damu ya milioni 2 ya watu wenu, na kama inavyofanya sasa kutenganisha Darfur kwa damu ya mamia ya maelfu yenu. Kwa hiyo inukeni, enyi watu wa Sudan, ili kutibua mpango huo, waondoeni vibaraka na wanafiki, na sahihisheni mwenendo wa maisha yenu.
Enyi watu wa Sudan:
Muumini hang’atwi mara mbili kutoka kwenye shimo moja. Tumeng’atwa kutoka kwenye shimo la Amerika kwa kuitenganisha Sudan Kusini. Je, tutairuhusu kutenganisha Darfur? Imepokewa kutoka kwa Bukhari na Muslim kutoka kwa Abu Hurayrah, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kwamba Mtume (saw) amesema:
«لَا يُلْدَغُ الْمُؤْمِنُ مِنْ جُحْرٍ وَاحِدٍ مَرَّتَيْنِ» “Muumini hang’atwi mara mbili kutoka kwenye shimo moja.”
Hakuna nchi ambayo ingeruhusu maeneo yake kuchanika, kwa sababu katika umoja kuna nguvu, na katika mgawanyiko kuna udhaifu na udhalilifu. Basi vipi tunaweza kuruhusu hili wakati Uislamu umelifanya suala la umoja wa ummah na umoja wa umbo lake kuwa suala nyeti, ambalo linahitaji hatua za uhai au kifo? Kutoka kwa Urfajah, amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akisema:
«مَن أتاكُمْ وأَمْرُكُمْ جَمِيعٌ علَى رَجُلٍ واحِدٍ، يُرِيدُ أنْ يَشُقَّ عَصاكُمْ، أوْ يُفَرِّقَ جَماعَتَكُمْ، فاقْتُلُوهُ»
“Atakayekujieni na hali mambo yenu yameshikana chini ya mtu mmoja, akitaka kuwatenganisha au kuwagawanya kundi lenu, basi muuweni.”
Enyi Waislamu:
Vipi munaweza kukaa kimya juu ya mgawanyiko wa nchi yenu na musichukue hatua, na musifanye umoja wa nchi yenu kuwa suala nyeti, kama Mtume wenu (saw) alivyokuamuruni? Je, munamtii nani? Je, mutaitii Marekani, mkoloni kafiri au kipenzi chenu Al-Mustafa (saw)? Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[وَما آتاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَما نَهاكُمْ عَنْهُ فَانْتَهُوا وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقابِ]
“Na anacho kupeni Mtume chukueni, na anacho kukatazeni jiepusheni nacho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.” [Al-Hashr: 7]. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[وَأَطِيعُوا اللَّهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَاحْذَرُوا فَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَاعْلَمُوا أَنَّمَا عَلَىٰ رَسُولِنَا الْبَلَاغُ الْمُبِينُ]
“Na mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume, na tahadharini. Na ikiwa mtageuka basi jueni ya kuwa juu ya Mtume wetu ni kufikisha ujumbe tu ulio wazi.” [Al-Ma’idah: 92].
Enyi Wanahabari:
Misheni yenu ni kubwa: kunyanyua ufahamu wa watu juu ya hatari za kugawanyika. Zifanyeni kalamu zenu na taasisi za vyombo vya habari kuwa jukwaa la ufahamu, kufichua njama za makafiri wakoloni na vibaraka wao, ambao huwasaidia kutekeleza njama zao dhidi ya nchi yetu na umoja wake. Nyinyi ni waaminifu katika kusema haki na kusimama dhidi ya batili. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[قُلْ جَاءَ الْحَقُّ وَمَا يُبْدِئُ الْبَاطِلُ وَمَا يُعِيدُ] “Sema: Kweli imefika, na uwongo haujitokezi, wala haurudi.” [Saba: 49].
Enyi Wanasiasa:
Kuhifadhi umoja wa nchi hii ni jukumu lenu la msingi kama viongozi, machifu na viongozi wa watu. Msimamo wenu dhidi ya miradi ya kugawanya na kutenganisha ndio ulinzi. Msiwe wasaidizi wa mkoloni kafiri, asije akatekeleza njama zake kupitia kwenu. Mwenyezi Mungu (swt) anasema:
[وَلَا تَرْكَنُوا إِلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا فَتَمَسَّكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّهِ مِنْ أَوْلِيَاءَ ثُمَّ لَا تُنصَرُونَ]
“Wala msiwategemee wanao dhulumu, usije ukakuguseni Moto. Wala nyinyi hamna walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, wala tena hamtasaidiwa.” [Hud: 113].
Enyi Wanachuoni, Enyi Warithi wa Manabii!
Jukumu lenu la kuwaongoza viongozi na watawala kuelekea kwenye haki na uongofu ni kubwa. Msiwe vibaraka wao, kwa kutoa fatwa wapendavyo, wala msikae kimya juu ya kusema haki, bila kujali matokeo. Mtume (saw) amesema: «مَنْ كَتَمَ عِلْمًا أَلْجَمَهُ اللَّهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ بِلِجَامٍ مِنْ نَارٍ» “Mwenye kuificha elimu, Mwenyezi Mungu atamtia hatamu siku ya moto Siku ya Kiyama.” Mnajua kuwa kuacha umoja na hadhi ya Ummah ni dhambi kubwa.
Enyi Maafisa na Wanajeshi:
Nyinyi mulioapa kulinda umoja wa nchi yenu, munawezaje kuruhusu ichanike huku mukitazama?! Mwenyezi Mungu atakuulizeni juu ya ahadi muliyoitoa. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[وَأَوْفُوا بِالْعَهْدِ إِنَّ الْعَهْدَ كَانَ مَسْئُولاً] “Na timizeni ahadi. Kwa hakika ahadi itasailiwa.” [Al-Isra: 34]. Msiruhusu Darfur kujitenga. Muliiacha Sudan Kusini hapo awali. Ondoeni dhambi kutoka katika shingo zenu, simameni dhidi ya njama ya Amerika, na hamasisheni jeshi kutibua mpango wa kuichana nchi yenu.
Jueni kwamba maafa haya ya giza na njama zinazoendelea za makafiri wakoloni hazitapata tiba isipokuwa kwa kurudi kwenye Uislamu mtukufu, itikadi na mifumo ya maisha. Hili linaweza kupatikana tu kwa kusimamisha Dola ya Kiislamu, Khilafah.
Hili linaweza kupatikana tu kwa kutoa nusrah (msaada wa kimada) kwa Hizb ut Tahrir, ili iweze kuisimamisha kama Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ili kuwatokomeza kwayo makafiri na kuunganisha ardhi za Waislamu. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal: 24].
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |