Jumanne, 13 Muharram 1447 | 2025/07/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  10 Muharram 1447 Na: HTY- 1447 / 01
M.  Jumatano, 02 Julai 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Haya ndiyo Matendo ya Umoja wa Mataifa... Mutaendelea Kuwahadaa Wananchi Mpaka Lini? Ni Kipi Kipya? Yako wapi Mabadiliko, Ee Wizara ya Ujenzi na Mabadiliko?
(Imetafsiriwa)

Mnamo Jumapili, tarehe 29/6/2025, jijini Sana'a, Waziri wa Masuala ya Kijamii na Leba, Samir Baja'ala, alifanya mkutano na kamati za maandalizi ya Kongamano la Vyama vya Ushirika la 2025, litakaofanyika mapema Julai 2025. Mkutano huo ulihudhuriwa na Ali Al-Razami, Katibu Mdogo wa Wizara ya Sekta ya Maendeleo na Nasser Al-Kahili, Mkurugenzi wa Afisi ya Masuala ya Kijamii na Afisi ya Leba katika Sekretarieti Kuu.

Kongamano hili linadhihirisha wazi kwamba Wizara haina ruwaza ya iliyozaliwa kabla wala mipango iliyopangwa tayari inayosubiri kutekelezwa. Badala yake, wito wa kongamano hili la vyama vya ushirika unaenda sambamba na maadhimisho ya kila mwaka ya Siku ya Ushirika Duniani, inayoadhimishwa na Muungano wa Kimataifa wa Ushirika, ambayo hufanyika Jumamosi ya kwanza ya Julai kila mwaka. Kaulimbiu ya mwaka huu ni "Ushirika: Uongozi Jumuishi na Masuluhisho Endelevu kwa Ulimwengu Bora."

Wito wa kusherehekea Siku ya Ushirika ulianza kwa Azimio 47/90 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lililotolewa mnamo tarehe 16/12/1992. Maadhimisho hayo yalianza mwaka 1995, kuadhimisha miaka mia moja tangu kuanzishwa kwa Muungano wa Kimataifa wa Ushirika mnamo mwaka 1895 M.

Nini kinaendelea, Ee Wizara ya Ujenzi na Mabadiliko?! Je, huu ni ujenzi wako, unaotoka Umoja wa Mataifa katika maelezo yake yote?! Mabadiliko yapo wapi?! Huu ndio umekuwa utaratibu wa watangulizi wako, wizara zilizofuata, kwa miongo sita, zikifadhiliwa na kuelekezwa na Umoja wa Mataifa kufanya mambo yanayomkasirisha na kumchukiza Mwenyezi Mungu, na kutoa wito wa fikra ambazo si za imani ya Kiislamu, ambazo sisi hatuna hisa wala ushawishi ndani yake! Mnapoteza pumzi zenu. Jaribio la ushirika nchini Yemen limeshindikana kwa sababu si la fikra za Uislamu. Tunasema haya kwa mujibu wa amri ya kuamrisha mema na kukataza maovu. Ee Serikali ya Mabadiliko na Ujenzi na wale wote wanaosimama nyuma yenu mnaelekea kwenye njia ya makosa, basi ufanyeni Uislamu kuwa ndio dira yenu, kama alivyoamrisha Mwenyezi Mungu.

Amkeni enyi watu wa Imani! Maangamivu na kuporomoka kwa watu hutokea wakati kuna mkanganyiko kati ya mifumo inayotekelezwa juu yao na imani yao au hata kugongana nayo waziwazi. Vipi wale wanaoasi maamrisho ya Mwenyezi Mungu na kutenda madhambi yake, wanaomfuata kila mlinganiaji, watafanikiwa na kuwa na furaha maishani?! Je, ni mifumo mingapi ya kifisadi imetekelezwa kwenu katika miongo sita iliyopita?! Na jueni kwa yakini kabisa kwamba hamtaepuka muozo, kuinuka, au kuwa na furaha mpaka mifumo ya Uislamu itekelezwe juu yenu katika siasa, uchumi, jamii, na sera za kigeni. Na hilo litatokea tu ndani ya dola ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal: 24]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 735417068
http://www.muslimworld.today
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu