Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
| H. 12 Jumada II 1447 | Na: HTY- 1447 / 12 |
| M. Jumatano, 03 Disemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
[وَإِنْ تَتَوَلَّوْا يَسْتَبْدِلْ قَوْماً غَيْرَكُمْ ثُمَّ لَا يَكُونُوا أَمْثَالَكُمْ]
“Na mkigeuka atawaleta watu wengine badala yenu, nao hawatakuwa kama nyinyi.” [Muhammad:38]
Mapambano Dhahiri ya Kikoloni huko Hadramawt juu ya Mafuta
Na Kuegemea Upande Wowote Ni Hasara Katika Dunia Hii na Akhera
(Imetafsiriwa)
Mnamo Jumamosi, 29/11/2025, vikosi vya jeshi vya Kikosi cha Ulinzi cha Hadramawt chenye uhusiano na Amr bin Habrish Al-Ali viliingia katika vituo vya mafuta vya Petro Masila katika Bonde la Hadramawt, vikinyanyua kauli mbiu ya kulinda vituo vya mafuta, huku vikiwaondoa wale waliokuwa hapo vikosi vya kawaida vya jeshi vilivyokuwa na uhusiano na Baraza la Octet.
Kitendo cha Amr bin Habrish Al-Ali kilikuja kama hatua ya kuzuia jambo lililopangwa usiku; huku Baraza la Mpito, linaloungwa mkono na Abu Dhabi, likifanya kazi ya kumwondoa kutoka wadhifa wa Rais wa Muungano wa Makabila ya Hadramawt, baada ya jaribio la awali la Baraza la Mpito kufeli mnamo Machi 2025.
Zaidi ya hayo, mnamo 29 Novemba 2025, watu kutoka makabila ya Hadramawt walisukumwa kumteua Khaled Muhammad Al-Kathiri kama rais wao, akimrithi Amr bin Habrish Al-Ali, baada ya kubadilishana vitisho kati ya Ibn Habrish na Abu Ali Al-Hadhrami, kamanda wa Vikosi vya Usalama vya Hadramawt kutoka Abu Dhabi. Na siku moja kabla ya uhamasishaji wa watu wengi katika mji ulio karibu wa Seiyun katika maadhimisho ya miaka 58 ya kuondoka kwa wanajeshi wa Uingereza kutoka Aden! Mnasherehekea maadhimisho ya uhuru wa gani, na kwa sura gani, wakati mkoloni huyo Uingereza bado anatengeneza mipango kote Yemen?
Matukio huko Hadramawt yalibadilika mara moja; mnamo tarehe 27 Novemba, Rashad Al-Alimi alimfuta kazi gavana wa Hadramawt, Mabkhout bin Madi, ambaye alielekea Imarati, na kumteua Salem Al-Khanbashi badala yake. Na karibu na hapo, mnamo tarehe 22/11/2025, uamuzi wa waziri ulitolewa ukimtenga Petro Masila, mwendeshaji wa Sekta 5 katika jimbo jirani la Shabwa, “ambalo linamiliki 30% ya hisa za Sekta 5,” na kuikabidhi kwa kampuni ya Marekani ya Jannah Hunt chini ya kifuniko cha kampuni ya Singapore-China yenye ushiriki wa wenyeji chini ya meza. Al-Bahsani, mjumbe wa Baraza la Rais la Octet na gavana wa zamani wa Hadramawt, alimpongeza Al-Khanbashi kwa kuchukua wadhifa huo na kulaani uvamizi wa Petro Masila na Amr bin Habrish Al-Ali.
Enyi Watu Wetu nchini Yemen kwa jumla na haswa katika Hadramawt: Amr bin Habrish Al-Ali alikuwa karibu na mwanzilishi wa Muungano wa Makabila ya Hadramawt, akimiliki pasipoti ya Saudia, na hadhi yake ilipanda kwa usaidizi kutoka Riyadh katika enzi ya Salman bin Abdulaziz. Aliitembelea, ambapo alipokelewa na Waziri wa Ulinzi Khalid bin Salman. Anatekeleza mipango ya watawala wa Al Saud na nyuma yao Amerika. Kuhusu Baraza la Mpito, ni uundaji wa Imarati yenye nia mbaya, ambayo inamfuata bwana wake Uingereza, mkoloni wa zamani wa Yemen. Wanawafanya Waislamu wa Yemen kuwasha vita ambavyo hatuna ngamia wa hisa, lakini tunawatumikia makafiri wakoloni! Muislamu anawezaje kuinua silaha dhidi ya ndugu yake Muislamu huku, kinyume chake, adui yetu halisi, umbile la Kiyahudi, likiendelea kuwachinja ndugu na dada zetu mjini Gaza huku sisi tukipigana wenyewe kwa wenyewe? Akili ziko wapi?!
Pande zote mbili ni vibaraka wanaotekeleza mipango ya Wamagharibi makafiri katika ardhi zetu. Kwa hivyo wafukuzeni Waarabu wote wa Riyadh na Abu Dhabi kutoka Yemen; wao ni wachafu kabisa, na wao ni vibaraka wa kikanda wa washindani wa kweli wa kimataifa dhidi ya Yemen, wakifuatana na vibaraka wa ndani wanaofuata maagizo yao. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:
[وَلَا تَرْكَنُوا إِلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا فَتَمَسَّكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّهِ مِنْ أَوْلِيَاءَ ثُمَّ لَا تُنصَرُونَ]
“Wala msiwategemee wanao dhulumu, usije ukakuguseni Moto. Wala nyinyi hamna walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, wala tena hamtasaidiwa.” [Hud:113].
Riyadh hailinganii Dini – baada ya kuregesha masanamu kwake – wala Abu Dhabi, ambayo imeanzisha mahekalu ya Kibaniani. Riyadh inalingania Washington, na Ibn Salman huyu ametelekeza ukarimu wa Mwenye Kurehemu na akawa mgeni wake. Na Abu Dhabi inalingania London, na Mohammed bin Zayed ni mtumwa wake, amedhalilishwa katika ziara zake za mara kwa mara Downing Street. Hakuna kheri kwa wale wanaozilingania wala kwa wale wanaolinganiwa kwazo. Jueni kwamba kheri yote ipo katika kumtii Mwenyezi Mungu, ambaye amekuamrisheni kuhukumu kwa Uislamu, kama alivyosema (swt):
[إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّهِ أَمَرَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ]
“Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu tu. Yeye ameamrisha msimuabudu yeyote isipo kuwa Yeye tu. Hiyo ndiyo Dini Iliyo Nyooka. Lakini watu wengi hawajui.” [Yusuf:40]. Na Yeye (swt) amesema:
[وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَمْراً أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ وَمَن يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالاً مُّبِيناً]
“Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapo kata shauri katika jambo lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi hakika amepotea upotofu ulio wazi.” [Al-Ahzab:36].
Na Mtume Wake (saw) amekupeni bishara njema katika zama zenu baada ya utawala dhalimu ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, aliposema (saw):
«تَكُونُ النُّبُوَّةُ فِيكُمْ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ مُلْكًا عَاضًّا فَيَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ مُلْكًا جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ ثُمَّ سَكَتَ»
“Utume utabaki miongoni mwenu kwa muda anaotaka Mwenyezi Mungu ubakie, kisha atauondoa atakapotaka kuuondoa, kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya utume, na itabakia kwa muda anaotaka Mwenyezi Mungu ibaki, kisha ataiondoa atakapo kuiondoa, kisha utakuwepo ufalme unaouma, na utabakia kwa muda anaotaka Mwenyezi Mungu ibaki, kisha Ataiondoa atakapotaka kuiondoa. Kisha kutakuwa na ufalme wa kidhalimu, na utabaki kwa muda wote ambao Mwenyezi Mungu anataka ubaki, kisha Atauondoa atakapotaka kuuondoa. Kisha kutakuwa na Khilafah kwa njia ya Utume.” Kisha akanyamaza.
Na hii hapa Hizb ut Tahrir anakulinganieni muisimamishe.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Yemen
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Yemen |
Address & Website Tel: 735417068 http://www.muslimworld.today |
E-Mail: yetahrir@gmail.com |



