Kamanda wa Jeshi Tunayemhitaji
- Imepeperushwa katika Uchambuzi
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Pamoja na mabadiliko katika amri ya jeshi la sita kwa ukubwa duniani, mjadala ulizushwa ndani, nchini Pakistan, na kiulimwengu, juu ya dori ya taasisi yenye nguvu ya kijeshi na mkuu wake wa jeshi. Mengi yamejadiliwa kuhusu urithi wa wakuu wa jeshi, waliomtangulia Jenerali Syed Asim Munir, Mkuu wa Jeshi wa Kumi na Saba wa jeshi la nyuklia, la tisa kwa nguvu zaidi duniani.