Al Waqiyah TV: Enyi Watawala katika Nchi za Waislamu ... Je, Hamuoni Aibu?!
- Imepeperushwa katika Al-Waqiyah TV
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Al Waqiyah TV: Enyi Watawala katika Nchi za Waislamu ... Je, Hamuoni Aibu?!
Al Waqiyah TV: Enyi Watawala katika Nchi za Waislamu ... Je, Hamuoni Aibu?!
Mwaka mzima umepita tangu kuanza kwa Kimbunga cha Al-Aqsa na vita vikali vilivyofuata huko Gaza. Tangu tarehe 7 Oktoba mwaka jana, watu wa Gaza wamevumilia mitihani mikubwa, wakiishi katika machungu, mateso, na majanga yasiyohesabika.
Al Waqiyah TV: Mihemo ya Walio Imara... Mahojiano ya Moja kwa Moja kutoka Barabara za Gaza!
Takriban watu 40,000 wameuwawa mjini Gaza katika kipindi cha miezi 10 iliyopita, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, huku serikali za ulimwengu, zikiwemo nchi za Waislamu zikitazama kama watazamaji pekee wa mauaji haya ya umwagaji damu, bila ya dhamira yoyote ya kisiasa ya kukomesha mauaji hayo. Hakika, tawala nyingi za ardhi za Kiislamu kwa miongo kadhaa zimeimarisha mkono wa uvamizi wa Kiyahudi kupitia mikataba yao ya amani, kuhalalisha mahusiano ya kidiplomasia, na ushirikiano wa kiuchumi na umbile hili la mauaji ya halaiki.
Wanawake wa Kiislamu kutoka sehemu mbalimbali za dunia wameelekeza wito kwa wana wa majeshi ya Kiislamu kutekeleza wajibu wao wa Kiislamu katika kuwalinda Waislamu wa Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) kutokana na uchafu wa umbile la kiyahudi linaokalia kwa mabavu, na kukomboa kila shubiri ya ardhi hii iliyobarikiwa kutoka kwa makucha ya uvamizi huu wa kikatili.
Filamu ya Hali Halisi “Kutoka Moyoni mwa Gaza!”
DVD “Enyi Umma; Kilio Wanacholia Wafungwa wa Dhamiri nchini Uzbekistan!”
Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir yaandaa Tufani ya Twitter kwa kichwa: “Enyi Umma; Kilio Wanacholia Wafungwa wa Dhamiri nchini Uzbekistan!” ili kuwanusuru wabebaji ulinganizi wenye ikhlasi wanaonyanyaswa na utawala dhalimu wa Uzbekistan.
Vyombo vya usalama nchini Uzbekistan vimewakamata tena wanachama 23 wa Hizb ut Tahrir na kuendelea na taratibu za kesi zao Mei 9 mwaka huu kwa mashtaka yale yale waliyoshtakiwa wakati wa enzi ya dhalimu aliyefariki Karimov, ambayo kwayo walitumia karibu miaka 20 jela na mateso tangu 1999 - 2000 M.
Hizb ut Tahrir inatoa pongezi na baraka zake za dhati kwa Umma wa Kiislamu, wenye kulemewa na majeraha na kustahamili shinikizo la moja kwa moja na lisilo la moja kwa moja la kikoloni. Kwa mnasaba huu, tunawataja makhsusi watu wetu wenye subira mjini Gaza Hashim na kwa jumla katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, tukimuomba Mwenyezi Mungu azifanye siku za Idd hii kuwa chanzo cha utulivu wa nyoyo zao.