- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:
Matembezi ya Ukombozi: “Kwa Netanyahu na Watumishi wake: Khilafah ni Bishara Njema ya Mtume wetu (saw), ambayo inaunganisha Umma na kuangamiza “Ndoto ya Israel Kubwa.”
Mnamo Ijumaa, 22 Agosti 2025, matembezi makubwa yalifanyika katika mji mkuu, Tunis, kutoka Msikiti wa Al-Fath kufuatia swala ya Ijumaa. Matembezi hayo yaliandaliwa na Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia chini ya kichwa, “Kwa Netanyahu na Watumishi wake: Khilafah ni Bishara Njema ya Mtume wetu (saw), ambayo inaunganisha Umma na kuangamiza “Ndoto ya Israel Kubwa.”
Wakati wa matembezi hayo, mabango yaliinuliwa, bango kuu likiwa na cha matembezi huku bango la pili, likiwa limeandikwa “Tamko la Netanyahu kuhusu Israeli ni sababu ya majeshi kuandamana, na chochote kando na hicho ni khiyana.” Bango la tatu liliandikwa, “Hakuna ndogo wala kubwa, kifo chenu ni ahadi ya Mwenyezi Mungu.” Wahudhuriaji waliimba miito katika muda wote wa maandamano hayo, ikiwemo, “La Ilaha illa Allah... Khilafah ni utawala wa Mwenyezi Mungu,” “La Ilaha illa Allah... Khilafah ni faradhi ya Mwenyezi Mungu,” na , “La Ilaha illa Allah... Khilafah ni ahadi ya Mwenyezi Mungu.” Pia waliimba kaulimbiu nyengine, kama, “Netanyahu, sikiliza, sikiliza... Khilafah yetu itaregea. Ewe Amerika, sikiliza, sikiliza... Khilafah yetu itaregea. Ewe Mzayuni, sikiliza, sikiliza... Khilafah yetu itarejea.” “Enyi majeshi ya Waislamu, jihad iko Palestina,” na “Watawala wameiuza Palestina ... kwa vyeo na mamilioni.”
Matembezi hayo yalipita katika barabara kuu za mji mkuu zinazoelekea Barabara ya Al-Thawra, ambapo yalihitimishwa mbele ya Ukumbi wa Michezo wa Manispaa kwa hotuba iliyotolewa na mmoja katika mashababu wa Hizb ut-Tahrir. Aliutahadharisha Umma wa Kiislamu dhidi ya matamshi ya Netanyahu kuhusiana na ndoto ya “Israel Kubwa” ya kuziunganisha nchi nyengine za Kiarabu kwenye umbile lao potovu, kama vile Misri, Jordan, Lebanon, Syria na Saudi Arabia baada ya kuikalia kwa mabavu Gaza na kutwaa Ukingo wa Magharibi. Netanyahu alighurika na misimamo ya watawala wa Waislamu walioyafunga majeshi ya Umma, wakang'ang'ania kulinda umbile lao, na hata kumsaidia katika kuwaangamiza ndugu zetu. Ni wajibu wa Ummah wa Kiislamu kukabiliana na mtu huyu jeuri kwa majeshi yake, vifaru na vikosi vyake vyote vilivyomo ndani yake, kwa kuchukua hatua na kumpa somo Netanyahu, na Trump nyuma yake, somo litakalowasahaulisha ndoto zao za kishetani na kutimiza bishara njema ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), Dola ya Khilafah Rashida, ambayo itaiokoa Gaza, itaikomboa Palestina na kuunganisha Ummah.
Hivyo, Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia inaendelea na wito wake wa wazi wa kupambana katika mazingira haya magumu yanayowakabili watu wa Gaza, ambao wanakabiliwa na njaa, mashambulizi ya mabomu, na mambo mengine ya kutisha makubwa, pamoja na Waislamu wengine wanaokandamizwa, inaendelea na wito wake kwa wenye ikhlasi katika majeshi ya Misri, Jordan, Uturuki, Pakistan, na majeshi mengine yenye nguvu kunusuru ulinganizi wa Uislamu na kusimamisha dola yake, ambayo itaiokoa Gaza, kuikomboa Palestina, kusimamisha hukmu ya Mwenyezi Mungu duniani, na kubeba ujumbe Wake wa uongofu kwa walimwengu.
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Tunisia
Ijumaa, 28 Safar Al-Khair 1447 H sawia na 22 Agosti 2025 M
- Picha za Amali ya Matembezi -
https://muslimworld.today/sw/index.php/dawah/tunisia/4899.html#sigProId1480cfb6ff
- Alama Ishara za Amali -
#طوفان_الأقصى
#الجيوش_إلى_الأقصى
#الأقصى_يستصرخ_الجيوش
#AksaTufanı
#OrdularAksaya
#ArmiesToAqsa
#AqsaCallsArmies
Kwa maelezo zaidi tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut tahrir / Wilayah Tunisia:
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia
Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia
Tovuti Rasmi ya Jarida la Tahrir
Ukurasa wa Facebook wa Jarida la Tahrir