Ijumaa, 07 Safar 1447 | 2025/08/01
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Heshima yote ni kwa Mwenyezi Mungu

(Imetafsiriwa)

Habari:

Bunge la Seneti mnamo Alhamisi lilipitisha azimio kwa kauli moja, kulaani tukio la mauaji ya wenza mchana kweupe kwa maagizo ya Jirga kwa jina la kile kinachoitwa “mauaji ya heshima” huko Balochistan. Lilisema mauaji haya ya kinyama hayawezi na hayapaswi kufunikwa na hoja yoyote ya kitamaduni, kikabila, au kimila kwa kisingizio cha kile kinachojulikana kama ghairat au “heshima.” Kwa kweli ni uhalifu ambao umelivunjia heshima taifa. Jaribio lolote la kuhalalisha uhalifu kama huo kwa msingi wa “desturi au heshima” halikubaliki kabisa, kama ilivyo kwa mchakato mzima wa kulaumiwa kwa mwathiriwa. (radio.gov.pk)

Maoni:

Hivi majuzi, video moja ya kutisha ya mauaji imeenea sana mtandaoni, na kuibua wimbi la hasira na mjadala wa umma. Tukio hilo, lililoripotiwa kutokea siku tatu kabla ya Idd al-Adha 2025 mwezi wa Mei, linaonyesha mwanamke akiongozwa kwenye eneo la jangwa na kupigwa risasi, kwa madai ya uhalifu ambao huenda amefanya au hakufanya. Video hiyo ilipozidi kuvutia, ilizua tafrani kwenye vyombo vya habari, huku watu wengi wakitoa maoni yao. Jambo lililosisitizwa zaidi ni kwamba haya yalikuwa mauaji yaliyofanywa kwa jina la heshima—kwa kusikitisha kupotosha na kutumia vibaya maana yenyewe ya neno hilo.

Balochistan, jimbo kubwa na lenye rasilimali nyingi zaidi nchini Pakistan, mara nyingi huangaziwa kwa sababu za kusikitisha. Mabomu, utekaji nyara, na tuhuma za usaliti ni simulizi za mara kwa mara zinazohusiana na ardhi hii. Bado chini ya vichwa hivi vya habari kuna ugonjwa zaidi wa kimfumo. Licha ya kuwepo kwa taasisi za serikali—kutoka kwa urasimu hadi idara ya mahakama—utawala wa sheria bado haujapatikana kwa wengi. Mahakama Kuu ya Balochistan, inayoongozwa na Jaji Mkuu, ni sehemu ya mfumo mkubwa wa mahakama wa Pakistan na inakusudiwa kutoa haki katika jimbo hilo. Lakini kwa kweli, mara nyingi imewaangusha watu ambao imekusudiwa kuwasaidia, na hivyo watu hawana imani na Mfumo wa Mahakama. Familia nyingi bado zinaomba majibu—zikitafuta wapendwa wao ambao walitoweka bila maelezo au walipatikana wamekufa kando ya barabara. Vilio hivi vyenye kudai haki visivyojibiwa vinaonyesha jinsi mfumo ulivyo dhaifu na usivyo na tija.

Chini ya Khanate ya Kalat, Balochistan ilisimamiwa kupitia sheria ya Kiislamu, pamoja na vikwazo fulani. Masuala ya kimahakama yalisimamiwa na Makadhi (majaji wa Kiislamu), wakati maeneo ya makabila yaliendeshwa chini ya mamlaka ya Sardar, ambao, wakiongozwa na Makadhi na Jirga, walitoa haki iliyokita mizizi katika Sharia na desturi za kienyeji (rawaj). Muda mrefu kabla ya utawala wa kikoloni, mifumo ya haki ya ndani ilikuwepo katika eneo hilo. Jirga—pia inaitwa Majlis, Shura, au Panchayat katika maeneo mengine—ilitumiwa kutatua matatizo kupitia majadiliano na makubaliano ya jumuiya. Viongozi kama vile Sultan Bahlol Lodhi na Sher Shah Suri waliunga mkono mila hizi na walishiriki katika mabaraza haya kusuluhisha migogoro. Kwa kuwasili kwa Waingereza, hata hivyo, kiini cha miundo hii ya jadi ilibadilishwa kwa udhibiti wa kikoloni. Waingereza walianzisha Jirga, wakiwateua machifu wa vijiji na viongozi wa makabila kama majaji katika kesi zinazohusu uhalifu mdogo, migogoro ya ndoa, uzinzi na migogoro ya ardhi au mifugo. Wanachama hawa walichaguliwa na kusajiliwa na Wakala wa Kisiasa, na adhabu yoyote iliyozidi miaka saba ilihitaji uthibitisho kutoka kwa Wakala kwenda kwa Gavana Mkuu (A.G.G.). Katika mambo mazito zaidi—hasa yale yanayohusu utiifu kwa Waingereza—hukumu ilipitishwa na Shah-i-Jirga, “Baraza Kuu” la Sarda wakuu.

Kwa hivyo, mfumo ambao hapo awali uliundwa kwa ajili ya maelewano ya jumuiya ulipotoshwa hatua kwa hatua. Uamuzi ulizidi kuendeshwa na hisia, kisasi, na ubaguzi wa kitamaduni. Fahamu tukufu ya heshima (ghairat) ilitumiwa kama silaha, ikapotoshwa na kuwa uhalali wa vitendo vya unyanyasaji ambavyo havikuwa na mfanano wowote na haki ambayo mifumo hii ilikusudiwa kuisimamia. Shutuma zinazotokana na hoja za maafisa juu yake kuwa ni kinyume na katiba ya Pakistan lakini sababu halisi ya tatizo ni katiba isiyo ya Kiislamu na kukosekana kwa utabikishaji wa Uislamu.

Mwenyezi Mungu (swt) asema katika Surat Fatir:

[مَن كَانَ يُرِيدُ الْعِزَّةَ فَلِلَّهِ الْعِزَّةُ جَمِيعًا]

“Mwenye kutaka utukufu basi utukufu wote uko kwa Mwenyezi Mungu.[Fatir: 10]

Heshima pekee inayostahili kuuwa au kuuwawa kwa ajili yake ni heshima kwa Mwenyezi Mungu na Sheria yake. Katiba ya Dola ya Khilafah itakuwa na mfumo wa Kimahakama ambao umetungwa kwa mujibu wa Quran na Sunnah na watu ambao watakuwa wakiisimamia hawatakuwa watumwa wa matamanio yao wenyewe. Kusimamishwa kwa Khilafah kwa njia ya utume ndiyo njia pekee ya kuuweka Umma wa Mtume Muhammad (saw) usikosewe au usikosee.

Khalifa Rashid wa Kwanza (Khalifa aliyeongoka), Abu Bakr as-Siddiq alisema, "وَالضّعِيفُ فِيكُمْ قَوِيّ عِنْدِي حَتّى أُرِيحَ عَلَيْهِ حَقّهُ إنْ شَاءَ اللهُ, وَالقَوِيّ فِيكُمْ ضَعِيفٌ عِنْدِي حَتّى آخُذَ الحَقّ مِنْهُ إنْ شَاءَ اللهُ" Mnyonge miongoni mwenu ni mwenye nguvu mbele yangu mpaka nimrudishie haki yake, Mwenyezi Mungu akipenda, na mwenye nguvu miongoni mwenu ni mnyonge mbele yangu mpaka nimpokonye haki isiyo yake Mwenyezi Mungu akipenda.” (Al-Tabari, Ibn Hisham).

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ikhlaq Jehan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu