Watoto Wapendwa wa Ash-Sham Wafariki Baada ya Boti za Wakimbizi Kuzama. Je, Tunapoteza Wangapi Zaidi Bila Khilafah?!
- Imepeperushwa katika Kitengo cha Wanawake Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
BBC iliripoti mnamo tarehe 23 Septemba 2022 kwamba wakimbizi wahamiaji 71 walipatikana katika mashua inayozama nje ya pwani ya Syria. Makumi wameripotiwa kufariki. Watu 20 kati ya walionusurika walipelekwa katika jiji la Tartus kutibiwa hospitalini. Wanawake na watoto wa Lebanon, Syria na Wapalestina walikuwa miongoni mwa watu 120 hadi 150 waliokuwemo ndani.



