Jumatatu, 10 Dhu al-Qi'dah 1447 | 2026/04/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Kwa kukosekana Khilafah, Watoto wa Ummah wetu nchini Iraq Wanaanikwa kwa Hofu za Utaifa

Mnamo tarehe 29 Septemba 2022, shirika la Habari la ‘Arab News’ liliripoti juu ya mashambulizi ya droni yaliyoanzishwa na Iran kwa kile kinachoitwa mawakala wa waasi wa Kikurdi katika eneo hilo. Milipuko ilitokea katika mji wa Irbil, Kurdistan ya Iraq na kushambulia shule moja iliyokuwa imejaa wanafunzi. Waandishi wa habari katika eneo la tukio walisambaza picha za watoto wa shule waliotapakaa damu katika eneo la Kurdistan kaskazini mwa Iraq.

Soma zaidi...

Je, Huduma za Usalama na Huduma ya Kijasusi ya Kijeshi Zinatoa Kinga kwa Wahalifu Miongoni mwa Wanachama wao?!

Katika mfano hatari, na uhalifu kamili wa kulaaniwa, jana, Jumamosi 15/10/2022, kundi la shabiha (wanamgambo) mjini Ramallah wanaohusishwa na vyombo vya usalama; kati ya mfanyikazi, watoto wake na mshirika wake wa karibu, anayejulikana kwa jina na cheo, waliwashambulia idadi ya wafanyikazi wa Hizb ut Tahrir kwa visu na marungu mbele ya Msikiti wa Saad bin Muadh mjini Ramallah

Soma zaidi...

Tangazo la Algiers... Umakinishaji wa Orodha za Mamlaka Zilizoharibika, Kung'ang'ania Udanganyifu, na Jitihada ya Kufufua Shirika Linalopaswa Kuzikwa

Huku mashambulizi ya umbile la Kiyahudi dhidi ya watu wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina yakizidi, mauaji, kuzingira na kunyanyasa, na huku makundi ya walowezi yakiharibu na kuwashambulia watu, na uvamizi wao kwa Al-Aqsa umeongezeka kwa kasi na ujeuri, na huku watu wa Palestina na watoto wao wakikabiliana na umbile la Kiyahudi kwa uthabiti, ushujaa, na ujasiri wote, makundi yanakusanyika nchini Algeria chini ya usimamizi wa serikali ya Algeria kutia saini makubaliano mapya ya maridhiano chini ya jina “Tangazo la Algiers!”

Soma zaidi...

Waislamu wa Pakistan Wapinga Vikali Usalimishaji wa Kashmir kwa Dola ya Kibaniani. Uongozi wowote Mpya wa Kijeshi Lazima Utangaze Jihad kwa ajili ya Ukombozi wa Kashmir, Kuthibitisha Utiifu wake kwa Uislamu na Waislamu

Mkuu wa Wanajeshi ya Pakistan (COAS) Jenerali Qamar Javed Bajwa mnamo tarehe 8 Oktoba 2022, Jumamosi, alihutubia gwaride la kufuzu kwa Kozi ndefu ya 146 katika Chuo cha Kijeshi cha Pakistan. Hotuba hiyo hakika haikumstahiki mkuu wa jeshi ambalo ni la sita kwa ukubwa zaidi duniani, linalochukuliwa kuwa la tisa kwa nguvu zaidi, linalomiliki makombora ya nyuklia na balestiki.

Soma zaidi...

Watoto wa Afghanistan na Unafiki wa Kimagharibi

Tangu utawala wa Marekani uondoke Afghanistan na serikali ya Taliban kuchukua madaraka, maamuzi ya nchi za Magharibi yalianza kuongezeka, hasa baada ya kundi la Taliban kuchukua maamuzi ambayo Magharibi inayaona kuwa hayaendani na hadhara na mtindo wake wa maisha, kama vile kulazimisha niqab kwa wanawake na kutenganisha madarasa kati ya wanaume na wanawake, pamoja na maamuzi mengine.

Soma zaidi...

Mkuu Mstahiki wa Jeshi ni Yule Anayekataa Kuitegemea Marekani, Anatoa Nusrah kwa ajili ya Kusimamisha Tena Khilafah na Kuhamasisha Kuikomboa Kashmir Iliyokaliwa

Jenerali Bajwa kwa sasa yuko jijini Washington, akifanya mikutano ya kuagana na mabwana zake. Ajenda yake ni kuhakikisha kwamba Pakistan inasalia ndani ya mtego wa utumwa wa Marekani baada yake, anapofanya mazungumzo thabiti pamoja na Pentagon na maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.

Soma zaidi...

Kuwa "Mzayuni Mkubwa" Kunamaanisha kuwa kama Putin na Kusaidia Uvamizi Kikatili na Haramu

Katikati ya uchumi unaofeli, mfumko wa bei wa tarakimu mbili, viwango vya rehani vinavyoongezeka, bili za juu za kawi, mabadiliko ya kodi, kupanda kwa deni, mgogoro wa pesa za mfuko wa pensheni, vita nchini Ukraine, sarafu inayoshuka thamani, ongezeko la uhamiaji na idadi inayodidimia ya wapiga kura, Waziri Mkuu mpya wa Uingereza (na labda nusu ya baraza lake la mawaziri) alipata wasaa wa kujitokeza kwenye hafla ya kando ya CFI kwenye dhifa ya kongamano lao la chama ambapo alijitangaza kwa fahari kuwa "Mzayuni mkubwa."

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu