Wilaya ya Al-Arish Mina, Warraq Mpya Kuwahamisha Wakaazi wake: Uwekezaji wa Lazima au Uhalifu wa Uhamishaji?
- Imepeperushwa katika Misri
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Siku hizi, mji wa Al-Arish unashuhudia sura mpya ya mateso wanayopata wananchi wa Misri mikononi mwa utawala unaowaona watu kuwa kikwazo tu kwa mipango yake ya uwekezaji na miradi yenye faida. Baada ya kimya cha miaka mingi na ahadi za uwongo kwamba wakaazi wa wilaya ya Mina kwamba hawatadhurika, watu walishangazwa kukuta matingatinga ya serikali yakiregea kubomoa nyumba na kung’oa wakao yao, bila kujali utakatifu wa nyumba, utu, au haki za watu, ambazo Mwenyezi Mungu (swt) amewapa katika ardhi na mali zao.



