Jumapili, 17 Jumada al-thani 1447 | 2025/12/07
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Wewe Ndiye Uliyewaletea Waislamu Njaa, Masoud Pezeshkian!

Iran ilitangaza kufilisika kwa benki yake kubwa zaidi ya kibinafsi, Benki ya Ayandeh, ambayo ina matawi 270 nchini Iran, baada ya madeni yake kupanda zaidi ya dolari bilioni tano, na kinachoshangaza ni ukosoaji wa rais wa Iran Masoud Pezeshkian kuhusu kushindwa kwa utawala akisema: “Tuna mafuta na gesi lakini tuna njaa”!

Soma zaidi...

Watawala wa Pakistan, Watu wa Trump, Wawateka nyara Mashababu wa Hizb ut Tahrir ili Kuhakikisha Kujisalimisha kwa Palestina

“Jenerali kipenzi cha Trump,” Asim Munir, amejibu kwa udhalimu kampeni yenye nguvu ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan, ambayo kwayo inataka uhamasishwaji wa haraka wa Vikosi vya Jeshi la Pakistan ili kuikomboa Palestina. Majambazi wa Asim Munir wamewateka nyara matetezi watano, kutoka Lahore, Karachi na Peshawar, na mahali walipo hapajulikani. Udhalimu wa Asim Munir unatarajiwa. Asim Munir hawezi kutenda, sembuse kufikiria, nje ya maagizo ya Trump katika suala lolote, iwe kuhusu Gaza, Kashmir, Afghanistan au rasilimali kubwa za madini za Pakistan.

Soma zaidi...

Watawala wa Waislamu Hawana Sifa za Kulinda Heshima ya Waislamu!

Vyombo vya habari viliripoti kwamba Rais wa Marekani Donald Trump alicheza densi kwenye zulia jekundu kwenye uwanja wa ndege nchini Malaysia mnamo Jumapili, 26/10/2025, alipopokewa na Waziri Mkuu wa Malaysia. Idadi ya Wamalaysia, wanaume na wanawake, walipunga bendera za Marekani na kucheza muziki wa kienyeji ili kumkaribisha mhalifu huyo muuaji ambaye mikono yake imejaa damu ya Waislamu wa Gaza.

Soma zaidi...

Ziara ya Asim Munir jijini Cairo ni Hatua ya Kutekeleza Ruwaza ya Trump kwa Mashariki ya Kati

Katika utekelezaji wa ruwaza ya Trump kwa Mashariki ya Kati, ambayo inatazamia kupandishwa cheo kwa umbile la Kiyahudi ndani ya ulimwengu wa Kiislamu baada ya usawazishwaji mahusiano, na kujumuishwa kwa serikali zote zilizopo katika ulimwengu wa Kiislamu ndani ya kile kinachoitwa ruwaza ya Mikataba ya Abraham, uhusiano wa hivi karibuni kati ya vibaraka wa Amerika katika ulimwengu wa Kiislamu umefanyika, kwa lengo la kutimiza ndoto za Trump katika eneo hilo.

Soma zaidi...

Kumwalika Adui wa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, na Waumini Ni Sawa na Kualika Ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na Msiba: Mche Mwenyezi Mungu, Ewe Waziri Mkuu wa Malaysia!

Hizb ut Tahrir / Malaysia inalaani vikali mwaliko uliotolewa na Waziri Mkuu wa Malaysia, Dato’ Seri Anwar Ibrahim, kwa Rais wa Marekani, Donald Trump — ambaye mikono yake imejaa damu ya Waislamu wa Gaza — kuja nchini Malaysia kuhudhuria Mkutano wa 47 wa ASEAN jijini Kuala Lumpur. Mwaliko huu si tu ishara ya aibu ya kidiplomasia isiyo na msimamo wa kimaadili; ni aibu kubwa kwa hadhi ya Ummah huu, usaliti unaojeruhi dhamiri ya kila Muislamu ambaye bado ana heshima karibu na moyo wake, hasa zaidi watu wa Palestina.

Soma zaidi...

Tafakari Muhimu Kuhusu Taarifa ya Chama cha Maimamu nchini Uholanzi

Taarifa ya Chama cha Maimamu nchini Uholanzi (VIN) inadai kwamba ushiriki wa kisiasa ndani ya jamii za Ulaya ni “njia inayoruhusiwa na halali,” na kwamba ushiriki unaweza hata wa kupendekezwa au wa lazima kulingana na hali. Msimamo huu unahitaji kuzingatiwa kwa makini, kwani unaegemezwa juu makisio ambayo hayaakisi vya kutosha uhalisia wa mfumo wa kisekula.

Soma zaidi...

Watawala wa Pakistan wanaogopa mwamko wa Kiislamu unaoongezeka miongoni mwa Waislamu wa Pakistan na, kupitia utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Utendakazi, wanajaribu—bila mafanikio—kuusimamisha kwa kuigeuza Pakistan kuwa “dola ngumu zaidi.”

Mwenendo mkali na wa kikatili wa watawala dhidi ya mkutano wa TLP umesababisha mawimbi ya wasiwasi katika duara za kidini za Pakistan na kumshangaza kila Muislamu mwenye ufahamu. Hata hivyo, mbinu hii ya kiimla ya watawala wa Pakistan si kitendo cha pekee au kisicho cha kawaida; bali ni sehemu ya msururu wa hatua mfululizo ambazo watawala wamechukua katika siku za hivi karibuni, hatua zilizozidi wakati watawala wa Pakistan walipokubali kutekeleza mpango wa Trump pamoja na watawala wa nchi za Kiarabu na zengine za Kiislamu, mpango ambao lengo lake ni kulinda uwepo wa Mayahudi kutokana na upinzani wa Waislamu wa Palestina.

Soma zaidi...

“Vita vya Burqa” vya Wananchi Ni Mwangwi wa Kisasa wa Ukoloni wa Ulaya, Uliotumika Kupuuza Mauaji ya Halaiki mjini Gaza na Kumvua Mwanamke wa Kiislamu Kitambulisho Chake cha Kiislamu

Vita vya hivi karibuni vya watu wengi kutoka kwa vyama vya kidemokrasia na serikali za mrengo wa kulia vinavyotaka kupigwa marufuku kwa burqa sasa vinajumuisha Australia, Italia na Ureno. Mataifa haya ni sehemu ya kundi kubwa la nchi adui za Ulaya ambazo tayari zimepiga marufuku burqa. Ufaransa, Ubelgiji, Denmark, na Uswizi zinatekeleza marufuku ya kitaifa katika maeneo yote ya umma, huku Uholanzi na Ujerumani, zikiwa na marufuku ya sehemu inayolenga muktadha maalum kama vile shule au afisi za serikali. Nchini Uingereza, mjadala unalenga wafanyikazi, ambapo chama cha mrengo wa kulia cha Mageuzi cha Uingereza kinasema kwamba burqa kama hizo zinazuia uoanishwaji, mawasiliano, na usalama, zikiziita “nembo za mgawanyiko.”

Soma zaidi...

Mayahudi Hawaheshimu Maagano Wala Hawawezi Kuaminiwa, Na Wapatanishi Si Waaminifu

Umbile la Kiyahudi limekiuka makubaliano ya kusitisha mapigano dhidi ya Gaza zaidi ya mara 80, na kusababisha mashahidi wengi na majeraha, pamoja na kubomolewa kwa nyumba na uharibifu wa mali. Waziri mkuu wa umbile la Kiyahudi hata alijisifu kwamba aliangusha tani 153 za mabomu kwenye Ukanda wa Gaza kwa siku moja.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu